hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,442
Wakuu nina banda la kuku nimelijenga kwa miti na kukandika kwa udongo sasa usiku nikiwa nimelala anakuja mnyama anachimba na kuingia kisha anakamata kuku tena wale wakubwa kabisa anaondoka nao.
Cha kushangaza matukio yote hayo (kuchimba mpaka kuondoka na kuku) anayafanya ndani ya usiku mmoja tu tena bila ya mimi kushtuka yaani asubuhi ndo nakuta uharibifu huo. Amebomoa siku ya kwanza akasepa na mijogoo miwili, baada ya siku kama tatu akaja tena akachomoka na kuku mmoja mwenye watoto, kisha kesho yake akaja tena kwa spidi ya 5G akasepa na kuku watatu wakubwaa! Dah!!
Sasa katika kuuliza uliza wazoefu wanasema huyo ni nyegere na kumdhibiti kwake wanasema ni mapambano ya ana kwa ana tu au ufuge mbwa. Tangu hapo sijachukua hatua yoyote na wala hajaja tena mnyama huyo pamoja na kwamba nilikuwa kama nimemsusia alipovunja kwa mara ya mwisho sikuziba tena mashimo yale.
Sasa leo nikakumbuka kumbe kuna JamiiForums ambapo huwa tunapata suluhisho kwa mambo mbalimbali na ndomana nimeleta hoja hii wadau namdhibiti vipi mnyama huyu?