Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Hahahahahahahaah navuta picha kuku aliekatwa shingo anakuwaje hahahaha oYa anaruka ruka huYo mpaka sio vizuri
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] anakwambia "Mimi sindio Rais?"
 
Hii serikali mfugale anakuwa promoted kweli sijui sababu ni ipi?
 
Miradi ni maendeleo, kama hutaki miradi hamia ughaibuni.

Lakini jambo la msingi ili kupambana na Magu ilibidi kujipanga kisawasawa kama 2015.

Usione vinaelea vimeundwa, Chadema ya leo siyo ile ya 2015.
Kuna muda inabidi ukae kimya ili watu wasijue kichwani kwako pako wazi kiasi gani
 
Bado tu barabara ya kwenda mbinguni nadhani siku akiwakusanya maaskofu na Mashehe hii ndiyo itakuwa amri. Nawasilisha, huu mwaka jamani Lissu utatuumizia
 
Kweli maana kunakipindi maji ya ziwa yarivuka nakuja eneo la barabara hali ikawa mbaya sana usafiri ukawa kuunga paka upande mtubwi sehem ya kilomita 46
 
Nimegundua watu wengi wanauhafifu wa uelewa,Rais nikiongozi wa serikalI na shughuli za serikali zinaendelea,kama barabara hiko kwenye mpango wa kujengwa kwanini isijengwe??Watu wameona barabara tu,mbona hamsemi mishahara kwamba silipwe mpaka kampeni ziishe.
 
Kweli maana kunakipindi maji ya ziwa yarivuka nakuja eneo la barabara hali ikawa mbaya sana usafiri ukawa kuunga paka upande mtubwi sehem ya kilomita 46
Hiyo ni rushwa ya uchaguzi!Kama pameshafanyiwa feasibility study basi tayari barabara iko kwenye mpango!Na kama ina uharaka angeweza kumwelekeza tu Mfugale kwa utaratibu rasmi wa kiofisi!Lakini hii ya kusimama jukwaa la kampeni na kupiga simu kisha kuagiza barabara ijengwe ni rushwa,"rushwa"!!!!!!!!
 
Ni Africa tu tunaona hayo,ndio maana ikifika wananchi wakachoka basi kinanuka kweli kweli na walio madarakani wanatamani ardhi ipasuke waingie!
Haki ni neno dogo,ila limebeba dhamana kubwa sana!Unaweza usione leo au hata maisha yako yote,ila ukibahatika kukutana na madhara ya kupuuzwa kwake basi utatamani usage meno!
Tanzania sio kisiwa!
 
Hiyo ni rushwa alitakiwa awe ameijenga siku nyingi, hata kutoa ajira 13000 na kutoa bima ya afya wakati wa kampeni ni rushwa pia.
Watu wanakusanya tu hizo taarifa kwa ajili ya kuja kuzifanyia kazi baada ya uchaguzi
 
Alafu shughuri zake za ujenzi zinaanza Dec, 2020.


aaaaaaaaaaaaaaaaaaaah, tuache dharau wazeeeeeee
 
Nonsense. Kwani hiyo barabara tu ndio mbovu Tanzania hii. Tume ya uchaguzi haina maana ni vibaraka wake ndio wamejazana hapo.
 
Safi sana muheshimiwa Rais,JPM apendagi ulugwalugwa na tit for tat.
 
Tokea Nyerere, Mwinyi na Mkapa,Kikwete na sasa Magufuli ulishasikia au kuona Kiongozi tokea upinzani anakabidhiwa nchi?
Katika picha halisi, ni chama kimmoja,hadi katiba mpya iliopendekezwa na tume ya Warioba.
Uchaguzi kwa sasa ni kiini macho,heri Magufuli akaendeleza kazi zake.
 
Hapa unajaribu kusemaje?Kuwa huwa mnashindwa uchaguzi ila mabavu yanawabakiza madarakani?
Tambua kuwa haki huinua taifa na kustawisha amani na utulivu!Unaweza usiwe mkomavu wa kutosha kuelewa haya,ila ikifika wakati wananchi wakadai haki yao kwa namna nyingine,ndio hapo majuta huwa mjukuu!Mifano ipo mingi na hai!Wale wanaodhulumiwa haki yao wakichoka huwa ni suala la muda tu,na ndio hapo hata maadui inakuwa rahisi kupenyeza mambo yao!Mtu akifikia breaking point,ukampa silaha unategemea nini?Uasi hujengwa taratibu,pigieni chapuo uovu ila tambueni kuwa wanaodhulumiwa nao wana kipimo cha uvumilivu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…