Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii serikali mfugale anakuwa promoted kweli sijui sababu ni ipi?
DKT. Magufuli akiwa anaendelea na kampeni za uchaguzi 2020, amepita kijiji cha Nyehunge akiwa anaelekea Geita ambapo kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46. Alisimama kuongea na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, wakati anaielezea barabara hiyo ghafla aliomba simu yake na kumpigia mtu ambae baadae alijulikana ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS, Injinia Mfugale na mazungumzo yao yalikuwa hivi.
Magufuli: Hallo, Chief executive
Mfugale: Naam mheshimiwa Rais
Magufuli: Hujambo
Mfugale: Sijambo mheshimiwa
Magufuli: Uko wapi?
Mfugale: Niko Dar es Salaam TANESCO tunazungumzia habari ya Nyerere dam.
Magufuli: Haya, sasa mimi niko Nyehunge, kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46, hii barabara tumeshaifanyizia feasibility study na detail design, nimesimama hapa na wananchi, nataka hii barabara, mimi si ndio Rais?
Mfugale: Ndio mheshimiwa(Wananchi kicheko cha furaha)
Magufuli: Nyehunge Oyee, Unanielewa Chief? Basi hii barabara uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Huu ni mwezi wa ngapi? (Mfugale: Mwezi wa tisa). Haya uandae document zote kabla ya mwezi wa 12 haujafika na kandarasi apatikane, niulize hela nitazitoa wapi. Sawa Mfugale?
Mfugale: Nimekuelewa mheshimiwa Rais
Magufuli: Umenielewa, mueleze na Waziri kwamba hayo ni maagizo yangu wala yasibadilike, Asante sana.
MWISHO WA MAONGEZI
Kuna muda inabidi ukae kimya ili watu wasijue kichwani kwako pako wazi kiasi ganiMiradi ni maendeleo, kama hutaki miradi hamia ughaibuni.
Lakini jambo la msingi ili kupambana na Magu ilibidi kujipanga kisawasawa kama 2015.
Usione vinaelea vimeundwa, Chadema ya leo siyo ile ya 2015.
Ana mtaji mkubwa wa wajingaSafi Sana. Huyo ndio JPM, man of action.
Hiyo ni rushwa kama rushwa nyingine zilivyo!Hata mzee wa ubwabwa aliona tatizo wananchi wana njaa,akaamua kukitatua hapo hapo kwa kuwapa ubwabwa ila akaambiwa hiyo ni rushwa!
Kama ameona kuna hitaji la barabara,kwanini asifanye mawasiliano na huyo mfugale ili mkakati ufanyike na kazi ifanyike?Kwanini atumie jukwaa la kampeni?Hiyo ni rushwa, muiname muinuke hiyo ni rushwa!
Kweli maana kunakipindi maji ya ziwa yarivuka nakuja eneo la barabara hali ikawa mbaya sana usafiri ukawa kuunga paka upande mtubwi sehem ya kilomita 46Ameongea kama Rais, hata Trump yuko kwenye kampeni na bado anatoa executive order hiyo ndiyo dunia ya kisasa.chadema toeni sera mbadala za kuonyesha ubora wenu, lakini kama sera zenu anazotoa Lissu za kuvunja Muungano na kudanganya eti karume alilazimishwa ni ujuha ulipitiliza.Mtasubiri sana
Hiyo ni rushwa ya uchaguzi!Kama pameshafanyiwa feasibility study basi tayari barabara iko kwenye mpango!Na kama ina uharaka angeweza kumwelekeza tu Mfugale kwa utaratibu rasmi wa kiofisi!Lakini hii ya kusimama jukwaa la kampeni na kupiga simu kisha kuagiza barabara ijengwe ni rushwa,"rushwa"!!!!!!!!Kweli maana kunakipindi maji ya ziwa yarivuka nakuja eneo la barabara hali ikawa mbaya sana usafiri ukawa kuunga paka upande mtubwi sehem ya kilomita 46
Ni Africa tu tunaona hayo,ndio maana ikifika wananchi wakachoka basi kinanuka kweli kweli na walio madarakani wanatamani ardhi ipasuke waingie!Unayefikiri kuna usawa pole sana, Lissu mwenyewe anajua usawa hakuna kikatiba, na kwa hiyo kampeni za Lissu ni za kutimiza mkakati wa kivuli cha demokrasia nchini na kwa kujua hilo Lissu anapungua gharama za kampeni kwa kuwachangisha michango wananchi!
Siasa ni maisha ya watu, siasa ni biashara za watu na usipojua mchezo huo utaumia sana na huenda ukapoteza maisha halafu wanasiasa wakaendelea kula bata pamoja!
Watu wanakusanya tu hizo taarifa kwa ajili ya kuja kuzifanyia kazi baada ya uchaguziHiyo ni rushwa alitakiwa awe ameijenga siku nyingi, hata kutoa ajira 13000 na kutoa bima ya afya wakati wa kampeni ni rushwa pia.
Alafu shughuri zake za ujenzi zinaanza Dec, 2020.Mhh mkuu mwananchi yeye anataka barabara, hajalishi ni uchaguzi au hapana.
Sisi wananchi tunataka haki ya kuwa na barabara na sio sheria ya kuwa na barabara wakati usio wa uchaguzi.Afterall yanini kutumia hesabu mbovu wakati fika yule Magu ataendelea,tunamdanya nani.
Tokea Nyerere, Mwinyi na Mkapa,Kikwete na sasa Magufuli ulishasikia au kuona Kiongozi tokea upinzani anakabidhiwa nchi?Anaendelea kwa mujibu wa nani?Sanduku la kura ndio mwamuzi!
Tunachosema hapa,hilo hitaji la barabara alishaliona ndio maana wakati anaongea akasema wameshafanya feasibility study na vitu kama hivyo!Sasa hiyo kufanya jukwaani ni rushwa,inamaana anawaambia msiponichagua barabara haitajengwa maana pesa najua mimi nitakapozitoa!
Hii ni rushwa ya wazi wazi na haikubaliki kwenye jamii ya wastaarabu!Hatukuwahi kuona mambi haya kipindi cha Mkapa wala kikwete!
Hapa unajaribu kusemaje?Kuwa huwa mnashindwa uchaguzi ila mabavu yanawabakiza madarakani?Tokea Nyerere, Mwinyi na Mkapa,Kikwete na sasa Magufuli ulishasikia au kuona Kiongozi tokea upinzani anakabidhiwa nchi?
Katika picha halisi, ni chama kimmoja,hadi katiba mpya iliopendekezwa na tume ya Warioba.
Uchaguzi kwa sasa ni kiini macho,heri Magufuli akaendeleza kazi zake.