Nyerere alijua Katiba ni mbovu lakini hakutaka kuibadilisha. Ni wakati sasa umefika ili Taifa liendelee linahitaji Katiba Mpya

Nyerere alijua Katiba ni mbovu lakini hakutaka kuibadilisha. Ni wakati sasa umefika ili Taifa liendelee linahitaji Katiba Mpya

Sio kweli, wanaotuangusha ni viongozi wetu na CCM hawapendi mabadiliko, unaikumbuka katiba ya Warioba ilikuwa kwenye hatua za mwisho watawala wakiongozwa na CCM wakaikwamisha.
Katiba ya Warioba ilikuwa ni utashi tu Kikwete na ndio maana ilikwama kutokana na hulka ya Kikwete mwenyewe kupenda kumsikiliza kila mtu.

Lakini hakuna shinikizo wala mapambano yoyote kutoka kwa wananchi wenyewe yaliyopelekea hali hiyo kama ilivyotokea kwa Zanzibar au Kenya.
 
Nyerere alikubali kutengeneza system ya kidikteta ambayo tumeirithi, system ambayo haijaandikwa popote kwenye katiba, kwamba ili rais awe na nguvu (power) lazima avae kofia mbili ya chama na ya serikali.

Nyerere aliwahi kusema katiba hii inamapungufu mengi inampa rais nguvu kubwa ya kuweza kuwa hata dikteta lkn pamoja na kuyajua hayo hakuwahi kuchukua hatua zozote za kutatua changamoto hizo.

Mfano, Katiba inataja mihimili mitatu Serikali, Bunge na Mahakama inayojitegemea lkn wakati huo huo Katibu wa bunge na majaji wa Mahakama wanateuliwa na rais.

Pamoja na mazuri ya katiba ya sasa lkn haikidhi kabisa mahitaji mengi ya msingi ya nchi na mwananchi, hasa kwenye eneo la utawala, matatizo tuliyonayo ya kiuongozi mengi yanasababishwa na ubovu wa katiba.

Hatuwezi kumlaumu sana Nyerere labda aliamua hivyo kutokana na hali halisi ya kisiasa ya wakati huo pengine hali hiyo kwa sasa haipo.

Ni wakati mwafaka sasa umefika ili taifa letu lisonge mbele kiuchumi, kijamii na kisiasa watanzania kwa pamoja lazima tuamue kuwa na katiba mpya na sio katiba mpya tu bali iwe katiba bora.
Nahisi alishindwa kuibadilisha katiba kutokana na ukata wa pesa!
 
Hakuna Mwanasiasa asiyeipenda hiyo katiba ya mwaka 1977. Hata CHADEMA ikitokea wakapata madaraka kupitia katiba hii hii, sahau katiba ya Warioba.

Katiba ya wananchi itapiganiwa na wananchi wenyewe kama ilivyotokea Zanzibar na Kenya. Hakuna mwanasiasa wala chama cha siasa kinachoweza kutoa katiba ya wananchi.

Kwa lugha rahisi hakuna mwanasiasa anayependa kumpa nguvu na madaraka mwananchi. Ukiona chama cha siasa au mwanasiasa analalamikia katiba iliyopo ni kwasababu tu haimpi faida yeye.

Point tupu.
Wanasiasa wengi wanaolalamikia Katiba leo ni wale ambao Katiba iliyopo haiwapi nafasi ya kufanya siasa kwa haki, kushinda uchaguzi na shughuli nyingine za kisiasa.
Kilichotokea kwenye bunge la Katiba ni ushahidi kuwa wanasiasa wanatucheza shere.
Suala la Katiba ni letu wananchi, tukiamua kupata Katiba bora tutaipata.
 
Kwanini Lowassa wa CCM hakutaka katiba mpya lakini Lowassa wa CHADEMA alitaka katiba mpya?
...Ni unafiki wa kisiasa,.
Ukiwa CCM Katiba ya sasa itakupa ushindi, itakulinda baada kuondoka madarakani. Ukitoka nje Katiba iliyopo haikuhakikishii ushindi.
 
Hakuna mahali mleta uzi amesemea kuwepo kwa Katiba mpya TU ndio kutaleta maendeleo. Sijui kwa nini hili angalizo la straw man argument linapendwa sana na wafahidhina wasiotaka kusikia kabisa suala la Katiba mpya.
Umejibu kwa pupa, ndio maana hata hueleweki ulichoandika.
Kwa mfano, haya maneno umeyapata wapi kwenye andiko langu ulilo'quote:
"...... kuwepo kwa katiba mpya TU ndiko kutaleta maendeleo."

Ni "angalizo" lipi limetolewa kwenye andiko ulilo'quote'?

"...strawman man argument"? Hii ina maana gani mkuu, maana sijapata kuisikia hata siku moja!

Na "wafahidhina" ni watu gani hao, huu ni msamiati mpya?

Hukusoma kilichoandikwa, na kama umesoma umerukia tu kujibu ambacho hukukielewa; uonyesha kwenye andiko ulilo'quote' sehemu inayosema sitaki "...kusikia .kabisa suala la Katiba mpya"

Kifupi ni kwamba umejidharaulisha sana na andiko lako hili. Kuna kitu kinakusumbua ndani kwa ndani,...achana nacho, njoo tu tubadilishane mawazo humu JF, tukubaliane, au tusikubaliane, yote sawa tu.
 
Wazo la kuandika katiba mpya halijaanza leo lilikuwepo hata enzi ya Nyerere, 80s jaribio la mapinduzi na 90s wakati wa G55.

Nyerere alikuwepo enzi za Mwinyi na Mkapa aliyajua mapungufu yake sio kuyajua tu aliyasema waziwazi, alikuwa na uwezo wa kushawishi kuyaondoa lkn hakufanya hivyo. Sababu zinaweza kuwa nyingi lkn kubwa ni kutoona chama chake kinapunguziwa nguvu.
Lakini si hata "chama chake" aliwahi kukisema kuwa "sio mama yake"? Au hiyo haikuonyesha lolote kuhusu msimamo wake?

Ninaweza kukubaliana nawe kwa kiasi, kwa maana alikuwa amewekeza nguvu zake nyingi mno huko kwenye chama hicho, na kuwekeza huko kulikuwa na madhumuni muhimu, ya chama kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo. Misingi yote iliwekwa ili chama kiweze kufanya kazi hiyo..., lakini haikuwezekana.
Wakati huo huo, mbadala wake ulikuwa ni nini?
Sasa wewe jiweke katika hali hiyo kwa wakati huo! Utaacha kweli kuwa 'conflicted'?

Anyway, hizi lawama za kurudi kwa Nyerere miaka yote hiyo baada ya yeye hazisaidii chochote. Miaka zaidi ya ishirini tushindwe kufanya jambo zuri, ambalo hata yeye alikwishalisemea, na bado turudi tu kwake kulaumu, hii inaonyesha udhaifu wa ajabu sana.
 
Kwanini Lowassa wa CCM hakutaka katiba mpya lakini Lowassa wa CHADEMA alitaka katiba mpya?
Lowassa aliamini atakuwa rais kupitia ccm na katiba.ingemlinda ila alipohamia chadema akagundua ile katiba aliyokuwa anaipigia debe haitamwezesha kuingia ikulu
 
Ni kukosa weledi kutaka kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa yaliyofanyika enzi zake kwa yanayotokea leo. Ni wapi aliposema katiba haiwezi kubadilishwa? Ametoka madarakani muda mrefu, bado unatafuta njia ya kumleta leo ili uweze kutoa lawama kwake?

Hiyo katiba ilikuwepo kwa wakati huo, bila shaka kwa sababu maalum ambazo leo hazipo, bado wewe unang'ang'ania awe yeye ndiye abadilishe katiba inayofaa kwa wakati huu? Huoni upungufu wa hoja zako?
Hivi hawa wanaotawala sasa na wanaoshikilia hiyo katiba, wanatawala kwa niaba ya Mwalimu Nyerere?

Hata hivyo, tukiachana na hizo lawama zisizokuwa na msingi, tutengeneze katiba tunayoitaka, ni jambo jema, lakini pia ni kukosa dira kutegemea kwamba kuwepo tu kwa katiba nzuri ndipo tutakapopata maendeleo.

Katiba nzuri inakuwa nzuri inapotekelezwa matakwa yake; na sio lazima kuwepo tu kwa katiba hiyo ndipo maendeleo yawepo.
Wengi wanamlaumu Nyerere kwa hisia na uwezo wao mdogo wa kufikiri, wakati katiba ya mwaka 1977 inatengenezwa kuna watu walitumwa waende nje ya nchi wakajifunze namna ya kutengeneza katiba lakini waliporudi walikuja na copy and paste ya katiba ya korea kasikazini.
Marehemu sheikh Thabit Kombo aliongea akisema yeye sio mwongeaji ila kwa sababu katiba ni swala linalohusu vizazi vijavyo itabidi aongee.
Alisema walipowatuma, hawakuwatuma wakanakili katiba ya nchi nyingine bali waliwatuma wakajifunze namna gani wanaweza kutengeneza katiba itakayoendana na utamaduni wetu mwisho wa kunukuu.
Watu wengi hata katiba hawaijui wamebaki kufata mkumbo wa wanasiasa ndio maana wanazungumzia mambo ya kisiasa ila mti kama mch. Mtikila aliitumia katiba hiihii kudai haki ya mgombea binafsi maana ilikuwepo ndani ya katiba na aliishinda serikali kwenye kesi na ilipokuja iwekwe kwenye utekelezaji serikali ilisema ilikuwepo kwenye mchakato wa katiba mpya lakini leo hii ni mwanasiasa gani wa upinzani ameenda mahakamani kudai haki ya mgombea sanasana tunasikia malalamiko ya wanaojiita wasomi tusiruhusu wagombea binafsi . Nina mengi ya kueleza ila naona niishie hapa labda kasomeni juu ya tume ya Nyalali, jaji Kisanga na rasimu ya Warioba vizuri halafu jiulizeni kwanini mapendekezo yao hayakutekelezwa
 
Na jambo linaloshangaza hapa ni kana kwamba walitaka Mwalimu Nyerere ndiye aandike hiyo katiba nzuri!

Sikumbuki wakati wowote kusikia Mwalimu Nyerere akipinga kuandikwa kwa katiba nzuri, bali anahimiza na kutoa angalizo juu ya katiba iliyopo; lakini anabebeshwa lawama kwa kutokuwepo na katiba mpya, miaka zaidi ya ishirini baada yake kutoka madarakani!
 
F5D912F2-4E47-41A8-BAA0-0FC7DDF9B5E0.jpeg
 
Back
Top Bottom