Sindano za sumu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2022
- 296
- 738
Kumbe kama hatuwezi badili chochote ata tukae miaka 100 mbele utamlaumu mwalimu tu.Still tunatumia katiba ya mwaka 1977 ambayo iliundwa wakati Nyerere akiwa Rais na katiba hiyo ndo ambayo imetengeneza na kusimamia mifumo yote ya kiuongozi ya sasa sasa unasemaje hausiki
Ccm hawawezi badilisha katiba ya sasa sababu inawafaidisha sana na hata wakibadilisha itakua ni katiba mpya jina ila maudhui ni yale-yale ya katiba ya zamani
Huwezi badilisha kitu/jambo ambalo linakufaidisha ndo kilichotokea mwaka 2014 kwenye katiba ya warioba
Mimi niliamini ktk kuchuja mazuri na mabaya ya mwalimu kama haya ya katiba, muungano umeyaweka upande wa mabaya ya mwalimu basi ungekuja na mawazo jadidi ya nini kifanyike tutoke hapa na sio kulia na mtu ambae vizazi na vizazi tutapita yeye haji kuinuka tena.