Sahihi kabisa, kila Taifa lililoendelea kuna muasisi alifanya kazi ya ziada, kitu alichokiweza ni kutuunganisha kwa lugha moja na kutoa dhana ya ukabila pamoja na kulinda raslimali tuu mengine yaliyobaki yeye ndio katuletea shida..Kwani Nyerere alikuwa Mungu mkuu? Au Nabii ...
Kuna mambo aliharibu sana, hasa kudumaza akili za watu wake.
Nchi hii watu wenye akili wanakaa kimya kuhofia umafia wa mifumo aliyoasisi yeye ya kudumu madarakani.
Katiba mbovu ya kifalme na yeye alilalamika hakuchukua hatua, tabia ya mtu akiharibu anahamishwa badala kupelekwa jela, watu wenye akili timam kuwa nje ya system kwa kuogopa challenges na kukaa na narrow minded people wanaojua kusifu na kuabudu...