Bepari2020
JF-Expert Member
- Nov 7, 2020
- 2,072
- 2,453
Kuna mambo vijana hawafahamu kwa either kutokupata undani wa mambo.
Nyerere hakutaifisha mali ya mtu binafsi, Nyerere alitaifisha mali za Indians ambazo walipata mikopo toka serikalini (serikali wa wakoloni waangalizi) enzi ya Muingereza.
Indians walikuja kama wapagazi na technicians wa kujenga central line kumalizia kipande cha Tabora kwenda Mwanza. Baada ya Indians kumaliza kazi, walipewa uraia wa Uingereza na serikali iliyokuwa inakusa kodi kwenye ardhi ya Tanganyika ikawapa baadhi kufungua biashara na walitakiwa kurejesha mikopo. Wengi hawakurejesha.
Kutaifisha ilikuwa kisheria kama mkuu serikali kurejesha mali zilopatikana kwa fedha ya serikali ambayo hawakuwa wamerejesha. Ndio maana Indians hawakuweza kuishitaki serikali maana haikuwa imevunja sheria na hata waliokuwa wanaishi kwenye nyumba walizojenga kwa mikopo, nao walinyang'anywa ila wakapewa haki ya kuishi kwa kupangishiwa.
Nyerere alikuwa smart kuliko vijana wanavyodhani.
Ila tupeni scenario ya Kenya (Muingereza) nimefika Kenya na kuishi kwa muda kwenye makazi ya watu
Congo ya (Belgium)
Zambia (Muingereza) nimefika Zambia na kuishi kwa muda mfupi
Malawi (Muingereza)
Mozambique (Mreno)
Kama hali ya mataifa yaliyotunguka kiuchumi na hali ya maisha ya watu ingekuwa bora (good living standard) inge-justify Nyerere aliharibu.
Ila hao majirani wao wamechoka sana na wakiweza kupenya kuishi hapa hakuna anetamani kurejea kwao. Fika Iringa/Njombe kuna wakenya wengi wanafurahia fursa za huku kuliko msoto ambao upo Kenya.
Hamna la maana ambalo Jomo na Moi walifanya, au Kaunda alifanya, au Banda wa Malawi alifanya kuweza kum-outshine nyerere.
Ukiweza kufanya comparative analysis utaeleweka sana kuliko kukandia na kulaumu bila kuandika rejea unapokosoa au unaposifia.
Ulitaka waishitaki serikali iliyowapora mali zao kwenye mahakama hizi hizi za serikali? Kesi ya nyani apelekewe ngedere siyo?
Viwanda, biashara, na mali za watu zilitaifishwa kwa sababu za sera za Ujamaa. Hakuna cha wahindi kudaiwa madeni wala nini. Kasome kitabu (Ujamaa essays on socialism) alichoandika Nyerere mwenyewe utaelewa. Kasome Azimio la Arusha utaelewa. Na Ujamaa haukuwa Tanzania peke, ulikuwepo kwenye nchi zingine za Afrika ambako ulifeli kama ulivyofeli hapa.
Kenya ilitupiga ovateki kiuchumi zamani sana. Na mpaka leo hatujaikamata. Unaposema kuna Wakenya wanakuja kutafuta fursa bongo ni sawa na kusema kuna Waturuki na Wachina waliojaa Dar kutafuta fursa hawataki kuondoka. Kwa mantiki hiyo Tanzania ina uchumi bora kuliko Uturuki na China. Lakini siyo kweli.