Kumbuka, kuhamisha makundi kwa makundi ya watu kuwasomba na kuwatupa porini, ukiwaamrisha "anzisheni kijiji cha ujamaa", simba, chui, nyoka, ndio wanawangoja, hakuna matibabu wala usafiri, hakuna nyumba wala tembe. "Imagine scenario" kama hiyo, ni wangapi waliopoteza maisha yao! Halafu apewe Noble prize. Is that "scenario" noble to you? If not, huyo ndio nyerere na hayo yametokea na si ya kuhadithiwa. Nilikuwepo.
Bwana majimshindo!
Ni vizuri hata kama humpendi mtu, basi toa maelezo ya ukweli (yawe mabaya au mazuri). Na hata kama unapenda kutoa mabaya tu, basi toa hayo mabaya kwa ufasaha, ukiweka ukweli tu badala ya kuweka tungo tata ambazo zinaweza zikatoa maana nyingine.
Jinsi ulivyoandika hapo, ungekuwa mwandishi wa historia kama yule jamaa yetu, kitabu chako kingekuja kuonesha kama vile Nyerere alikuwa anawakamata watu na kuwatupia sehemu zenye wanyama akiwa na makusudi kabisa kuwa watu hao waliwe.
Nakuomba ufanye utafiti, nenda mikoani, katembelee sehemu mbalimbali ambazo vijiji vya ujamaa viliulindwa, na maeneo yaliyofanyiwa "operesheni sogea". Kafanye bila
bias.
Utagundua kuwa nia ya Nyerere ilikuwa ni kuongeza productivity, na kusogeza huduma za jamii kama shule na hospitali kwa kaya ambazo kabla ya hapo zilikuwa zinakaa mbali mbali sana. Kuna baadhi ya miji midogo hadi sasa inandelea kukua vizuri, lakini ilianzishwa kwa operesheni sogea. Na kuna sehemu ambazo wananchi walikuwa wabishi, waligoma kusogea au kwenda kwenye vijiji vya ujamaa, sehemu hizo mpaka sasa bado ziko duni, na vijiji vyao vimekaa kienyeji zaidi.
Pia utakubali rohoni kwako kuwa Nyerere hakuwa kutoa amri kwa watendaji wake kwamba wawa "mistreat" raia hasa hilo suala la kuwatupa kwenye simba. Kama ambavyo humlaumu Kikwete kwa bomoa bomoa inayosimamiwa na waziri wake, basi hata nyerere huwezi kumlaumu kama ulivyofanya.
Lazima ufahamu pia zoezi lile la ujamaa villagisation lilikuwa sponsored na WB huku wakiwa wameagizwa na Western countries kuwa "lisifanikiwe" kwa sababu hawakutaka kuwepo na "socialist island" eneo hili. Kufanikiwa kwa lile zoezi kungeleta matatizo ya kuenea zaidi kwa ujamaa, kitu ambacho Western capitalists hawakutaka. Kulikuwa na "sabotage" kubwa ya lile zoezi ili nchi za magharibi zichukulie Tanzania kama mfano wa kushindwa ujamaa (Kama una marafiki Uingereza, wanaweza kukusaidia zaidi, kwasababu mwaka 2001 MI6 wali-declassify this information na kuwa accessible to the public. Walieleza jinsi nchi za magharibi zilivyo-conspire against Nyerere and his Ujamaa).
Nataka ufahamu pia kuwa yale unayofikiri umejielimisha mwenyewe kuhusu lile zoezi (labda kwa kujisomea au kusikiliza stories), sio yote ya kweli. Hata baadhi ya waandishi wazalendo walilishwa sumu hiyo hiyo na vitengo vya "disinformation and misinformation" vya CIA na MI6. Utakumbuka kuwa vyombo vya habari vya magharibi vili-document makusudi kuhusisha njaa ya 1974 na zoezi la ujamaa vijijini ilhali tatizo kubwa ilikuwa ukame na kupanda kwa mafuta duniani.
Sina uhakika na umri wako, lakini nina-assume utakumbuka ukame uliokumba nchi za kusini kuanzia malawi, Zimbabwe, Botswana, Zambia na Namibia miaka ya majuzi. Kama ulifuatilia kipindi kile, ndio Mugabe alikuwa anaanza ku-implement mambo yake ya land re-distribution. Kwa vile watu wa magharibi hawakupenda mambo ya Mugabe, muda wote walikuwa wanakazania (kwa makusudi) ku-report kuwa njaa ya zimbabwe ilitokana na siasa mbaya za Mugabe na walikuwa hawataki kugusia mambo ya ukame. Ukame ulikuwa unahusishwa na njaa ya nchi nyingine tu.
Kwa hiyo ndugu yangu, unaposoma na kusikiliza na kuandika, jitahidi kuwa makini. Kuna vingine unaweza ukaviamini kwa vile aliyeandika au kukusimulia anataka kweli wewe uamini hivyo.
I hope umenipata.
Kila la kheri!