Nyerere kakaa Ikulu miaka 23 haya mambo hayakuwepo

Nyerere kakaa Ikulu miaka 23 haya mambo hayakuwepo

Sio
Zama za Nyerere na sasa mambo mengi hayakuwepo. Kila zama na kitabu chake Mkuu.
Sio swala la enzi au nyakati, Bali ni sifa za kijinga tu.

Wakati wa Nyerere hata majina ya kusifu kama,, Mheshimiwa, mkuu, boss, mtukufu aliyapiga marufuku, tukawa tunaitana ndugu, au comrade na kwa wanasiasa ikawa jina la Kada.
 
Aisee hata mimi nashangaa sana. Enzi za Nyerere hakukuwa na marathon ya 334m, Tonetone, jointhechain wala mchango wa gari la mwenyekiti na mingine iliyokaa kipigaji. Zama hizi imekuwaje?
Hapa ndiyo mwisho wa kutumia akili zako? Hizo enzi za Nyerere CHADEMA ilikuwepo?
 
Mwalimu Julius Nyerere alikaa miaka 23 Ikulu lakini hatukuwahi kusikia "Nyerere marathon" "Nyerere doctors" "ngumi za Nyerere" au makorokoro mengine.

Zama hizi imekuwaje kwani?

Nyerere hakuwa kumtuma Mzee Songambele kuwa msemaji wake. Ukiona mtu kama Shekhe Mwaipopo anatamalaki, ujue kuna watu wanapwaya.

Ukiona mtu anaitisha maandamano kupinga mapanki, ujue ana strategy yake nyingine ya kula kwa upole. Taratibu watu wanaanza kuzinduka.

Mambo hayaendi au yanaenda mwendo wa konokono. Deni la Taifa linapaa. Miradi haisogei kabisa.sasa tunachofanya nini?

Ukijaribu kuuliza unaigwa ghaidiiiii 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Na wewe ndo mwisho wa kutumia akili zako kuandika uzi wa kipumbavu?

Lugha rejareja za mtaani hizi..lakini ukweli ni kuwa watanzania ndio wenye Tanzania. Na sidhani kama wataacha kuhoji.
Sababu, mida inabadilika. Ya jana sio ya leo. Akiondoka huyu anakuja mwingine. Huu mwendo mpka ukamilifu wa dahali
 
Mwalimu Julius Nyerere alikaa miaka 23 Ikulu lakini hatukuwahi kusikia "Nyerere marathon" "Nyerere doctors" "ngumi za Nyerere" au makorokoro mengine.

Zama hizi imekuwaje kwani?
Hata TV enzi za Nyerere hazikuwepo.
Hata Umeme mikoani enzi za Nyerere haukuwepo
 
Na wewe ndo mwisho wa kutumia akili zako kuandika uzi wa kipumbavu?
Ukiandika jambo kwenye mtandao kama huu mpe Mungu utukufu kwa kuumba binadamu na siyo Ng'ombe.

Usiandike jambo binadamu wenzako wakanza kushuku uwepo wako duniani kama binadamu.
 
Ukiandika jambo kwenye mtandao kama huu mpe Mungu utukufu kwa kuumba binadamu na siyo Ng'ombe.

Usiandike jambo binadamu wenzako wakanza kushuku uwepo wako duniani kama binadamu.
Acha ujanja wa mbuzi kujambia mdomo. Kubali huu uzi wako ni takataka
 
Mwalimu Julius Nyerere alikaa miaka 23 Ikulu lakini hatukuwahi kusikia "Nyerere marathon" "Nyerere doctors" "ngumi za Nyerere" au makorokoro mengine.

Zama hizi imekuwaje kwani?
Kila zama na zama zake, hata ikulu ya Butiama hatukuwahi kusikia!, uliwahi kumuona Mama Maria ana msafara, ana escort?. Nyerere aliwahi kuteua mkwe wake?, kama haitoshi na kuteua mtoto wake?. Nyerere alitunukiwa Ph.D za heshima kibao, uliwahi kusikia akiitwa Dr. Nyerere?. Enzi za Nyerere ni mambo ya kizamani, enzi hizi ni mambo ya kisasa!.
P
 
Kila zama na zama zake, hata ikulu ya Butiama hatukuwahi kusikia!, uliwahi kumuona Mama Maria ana msafara, ana escort?. Nyerere aliwahi kuteua mkwe wake?, kama haitoshi na kuteua mtoto wake?, enzi za Nyerere ni mambo ya kizamani, enzi hizi ni mambo ya kisasa!.
P
Usasa unaotakiwa kupigwa msasa. Haya mambo kayaanzisha ngosha mwenzio.
 
Back
Top Bottom