Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Posts
33,637
Reaction score
8,947
Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

by RAIA MWEMAin HABARI

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya kuyatathmini maisha yake.

Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka aliyowahi kuyasema Mwenyekiti Mao wa China kumhusu Josef Stalin, mtawala wa pili wa Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin.

Nami nikayatumia maneno hayohayo kuanzia makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was "a great leader who made great mistakes," as one ruler once famously said of another.(“Julius Nyerere alikuwa “kiongozi mkubwa (adhimu) aliyefanya makosa makubwa,” chambilecho mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo mtawala mwenzake.)

Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake. Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki sifa.

Watu wa kale wasema: “Kheri ya mja ni ulimi wake na shari ya mja ni huohuo.” Kwa ulimi wake Nyerere aliwahi kutamka maneno ya maana na mengine ya kibahaluli. Baadhi ya maneno yake yalikuwa kama lulu na baadhi yalikuwa kama utumbo kama pale, kwa mfano, aliposema kuwa hakuna watu waitwao Waswahili. Nilimsikia akiyasema hayo alipotoa hotuba katika ukumbi wa London School of Economics alipokuwa ziarani London kabla ya kuuacha urais.

Yote hayo yaonyesha kwamba Nyerere alikuwa mja, mtu kama watu wengine. Hakuwa Mungu, hakuwa malaika. Wala hakuwa mtume na hata hakuwa mpigaji ramli. Na si kila alichokitamka kilikuwa sahihi. Lakini binadamu yule alikuwa na ulimi uliowalaza wengi na kuwafanya waache kufikiri kwani alikuwa na kipaji cha kuwafanya waamini kwamba kila alilolisema lilikuwa la kweli kabisa na hivyo hapakuwa na haja ya kumfanya mtu mwengine alifikirie. Ilikuwa nadra kumpata mtu aliyethubutu kumpinga au kumkosoa, hasa kadamnasi. Walikuwapo waliochelea kukiona cha mtema kuni na wengine waliridhia kuwa vibarakalla vya kuitika tu ‘hewala bwana.’

Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima.

Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na Tanganyika basi Tanganyika kutakuwa shuwari lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea kutafutana asili zao.

Tangu wiki iliyopita waandishi kadhaa wa Bara wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu; na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa Wazanzibari.

Wakoloni walipowaona wanaowatawala wanaungana kuwapinga, basi walitumia mbinu ya kuwagawa wazidhoofishe nguvu zao ili waendelee kuwatawala.

Mbinu kama hiyo inatumiwa siku hizi na baadhi ya viongozi wa CCM wa Bara pamoja na baadhi ya waandishi wa huko huko Bara ‘walioshtushwa’ na mwamko wa kisiasa uliowafanya Wazanzibari wawe na ujasiri wa kuujadili kwa mapana na marefu Muungano wa Tanzania.

Ujasiri huo umewafanya wengi wao waseme kwamba ama wanaupinga muundo wa sasa wa Muungano au hawautaki kabisa na wanataka Zanzibar iwe dola huru yenye mamlaka yake kamili.

Huo si mwamko wa leo au wa jana; tumekuwa tukiugusia miaka nenda miaka rudi lakini tukionekana kuwa ni wazushi na wazandiki. Sasa mambo yanajidhihiri yenyewe. Matokeo yake ni kwamba waliokuwa wakijidanganya sasa wamegutuka na hawajui jinsi ya kulizuia hilo wimbi la uzalendo Wakizanzibari minghairi ya kutumia hoja finyu za kikabila na udini.

Mmoja amefika hadi ya kuandika kuhusu ‘Waarabu’ na ‘watu Weusi’ kana kwamba hao wanaonasibishwa na uarabu ni wa rangi aina ya pekee iliyo tofauti kabisa na ya Wazanzibari wasio na asili ya Kiarabu. Mwandishi huyohuyo alitishwa na sura rahimu ya Sheikh Farid Hadi Ahmed, mmoja wa viongozi wakuu wa Uamsho.

Aliandika kwamba baada ya kuiona picha ya Sheikh Farid yalimjia mawazo kwamba Uamsho si jumuiya ya kidini na wala si ya Wazanzibari na kwamba Sheikh Farid ametumwa (hakusema na nani) kuwafitinisha Wazanzibari. Alichotaka kusema mwandishi huyo ni kwamba kwa vile Sheikh Farid ana asili ya Kiarabu basi Uamsho inataka kuurejesha usultani.

Ni uchambuzi uchwara, tena wenye kutumia lugha ya kibri. Unashtua kwa vile ni ‘uchambuzi’ wa hatari unaofanana na simulizi za Wahutu wa Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Hizi fitna za ‘Upemba’ na ‘Uunguja’, za ‘ubwana’ na ‘utwana’ na za ‘ugaidi’ wa Uamsho ni fitna zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya uongozi au ya uandishi.

Hila wanazotumia ni kwanza, kuwafitinisha Wazanzibari kwa kutia fitna za kikabila na za kidini. Kwa mfano, wanawatisha wahafidhina wa CCM/Zanzibar, wale wenye kusherehekea kaulimbiu ya ‘Mapinduzi Daima’, kwa kuwaonya ya kuwa Uamsho ina “msukumo wa kiarabu” na kwamba kusudio lake ni hatimaye kuyapinga Mapinduzi na kuirejesha Zanzibar katika ‘utumwa’. Maneno ya kijinga kabisa.

Hila yao ya pili ni kuwagonganisha vichwa Waunguja na Wapemba kwa kutumia hoja zisizo na mshiko wowote wa kimantiki. Wanasema wamewapata Wapemba wengi wenye kutaka Muungano uendelee kama ulivyo. Wamewahoji na matamshi yao kusambazwa na magazeti fulani nchini. Huu ni mfano mzuri wa propaganda ya kitoto.

Hila yao ya tatu ni kutumia lugha kuparaganya mambo. Ingawa Uamsho ni jumuiya kamili wao badala yake wanasema kuwa hiki ni kikundi. Sio kundi bali ‘kikundi.’ Na wanaishtumu jumuiya hiyo kuwa ‘inawatumia’ baadhi ya vijana kufanya vitendo vya kihuni vya kuchoma moto makanisa. Hakuna ushahidi wa hili.

Nne, wanajaribu kuwatisha Watanzania na hasa wakuu wa dunia hii kwa kuifananisha Jumuiya ya Uamsho na mitandao ya kigaidi ya Al-Qa’eda, Boko Haram na Al-Shabab. Bila ya shaka wenye kueneza fitna hii hawajui walisemalo na wanajikashifu si mbele ya Watanzania wenzao tu bali hata machoni mwa balozi za nchi za Magharibi.

Sijui kama wanaelewa ya kuwa maofisa wa baadhi ya balozi za Magharibi wameshakutana na viongozi wa Uamsho katika juhudi zao za kuitathmini Jumuiya hiyo na wanayaelewa makusudio halisi ya Uamsho.

Kwa hakika, kinyume na wanavyoandika baadhi ya waandishi wa Bara, Jumuiya ya Uamsho haikuzuka juzi. Imekuwako kwa muda wa takriban miaka 10 sasa. Jumuiya hii ni kama mwavuli ambao chini yake kuna jumuiya mbalimbali za Kiislamu, pamoja na ile ya maimamu.

Uamsho imekuwa ikiendesha harakati zake kwa msaada wa taasisi za nchi za Magharibi. Ilikuwa miongoni mwa waangalizi rasmi wa Uchaguzi Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.

Kati ya wafadhili wa Jumuiya hiyo katika harakati hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa uchaguzi uliopita.

Wenye kujuwa mambo watakwambia kwamba kuna tofauti kubwa kama ya mbingu na ardhi kati ya jumuiya ya Uamsho na mtandao wa Al-Qa’eda au kundi la al-Shabab. Huwezi kabisa kuzifananisha falsafa zao au makusidio yao. Hata Boko Haram nayo licha ya mbinu inazozitumia inatofautiana sana na al-Qa’eda.

Huko Zanzibar mafatani hawa wana washirika wanaojulikana. Nao ni wale wanaochomwa na kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Ndiyo maana wakaruka harakaharaka kuwatupia lawama za machafuko ya hivi karibuni viongozi wa CUF waliomo kwenye SUK na kutaka watimuliwe kutoka serikalini. Na ni wao waliohusika na vipeperushi vilivyotolewa wiki iliyopita kuwafitinisha Wapemba na Waunguja.

Na ni haohao wenye kujaribu kuwachimba waasisi wakuu wa Maridhiano yaani Rais mstaafu Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.

Inasikitisha kuwaona baadhi ya Wabara wenye kujigamba kuwa ni wasomi wakitaka mijadala ya kisiasa ipigwe marufuku katika majukwaa ya kidini. Hawaelewi kwamba ni dhima ya dini za Ukristo na Uislamu kuzungumzia na kuyatafutia ufumbuzi mambo yanayoyagusa maisha ya kila siku ya waumini wa dini hizo. Na mambo hayo yawe yepi kama si ya kisiasa?

La kutisha ni kuwa ‘wasomi’ hao wanamtaka Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua za kimabavu wakuu wenzake walio serikalini kwa kisingizio kuwa ati wanaunga mkono harakati za Uamsho.

Ulimwengu haukufunga macho wala haukuziba masikio. Unawaona na kuwasikia. La ajabu ni kwamba wanasiasa na waandishi wenye kuchochea hisia kama hizo wamesahau ni nyakati gani tulizo nazo na ni ulimwengu gani tulio nao. Katika ulimwengu wao wa leo Wazanzibari wanasema hawakubali tena kugawanywa kwa propaganda za kikabila au za kidini.

Inatisha kwamba kuna wanasiasa na waandishi waliosahau kwamba siku hizi kuna Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) na mahakama nyingine mahsusi za kimataifa, mithili ya ile Mahakama Maalumu ya Sierra Leone. Mahakama kama ile ya Sierra Leone inaweza kuundwa mara moja na Umoja wa Mataifa kuwatia adabu wenye kupalilia fitna zinazoweza kuzusha mauaji ya kimbari.

Ni hiyo Mahakama Maalumu ya Sierra Leone iliyomhukumu Charles Taylor, rais wa zamani wa Liberia, kifungo cha miaka 80 baada ya kupatikana na hatia ya kuishushia nakama Sierra Leone.

Dhana waliyonayo baadhi ya wasomi na waandishi wa Bara ni kwamba viongozi wa Uamsho ni mijitu isiyosoma. Kuna mmoja aliyepandwa na jeuri na kuandika kwamba mbali na kujua kusoma Qur’an viongozi hao ni watu wasiojuwa kuandika wala kusoma.

Ukweli ni kwamba viongozi wa Uamsho ni wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na wana shahada za juu za uzamili katika fani mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote — za dini na dunia.

Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur’an pia alisomea taaluma ya hali ya hewa.

Baadhi yao walisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako walivutiwa na hotuba za kidini za Professor Malik, mtaalamu wa fani ya hesabati, ambazo ziliwashajiisha na kuwafanya wawe na mwamko wa Kiislamu. Wengine walisoma kwenye vyuo vikuu vya nje vikiwemo vile vya Sudan, Saudi Arabia na Qatar.

Ni wazi kutokana na ripoti na taarifa zao kwamba baadhi ya wasomi na waandishi wetu wa Bara wanawadharau Wazanzibari. Nadhani hizo dharau zao ndizo zinazowafumba macho wasiweze kuona nani hasa aliyechochea fukuto hili la upinzani dhidi ya makandamizo ya walioshika hatamu za utawala wa Muungano.

Maandishi yao yamebainisha wazi kwamba hawaamini ya kuwa Unguja na Pemba si majimbo wala koloni za Bara. Inakirihisha kuona namna wengi wao wanavyozitapika hadharani chuki zao (na udini uliowapamba) bila ya hata staha na uvumilivu wa kimaadili.
 
Mkuu umeandika hoja nyingi lakini kuhusu Nyerere; alikuwa binadamu kama tulivyo sisi, kwa hiyo isingewezekana asifanye makosa ukizingatia ilikaa madarakani miaka zaidi ya 20. Lakini mema mengi aliyolitendea Taifa letu yamfanya kuendelea kuwa nuru na alama sahihi ya utu wema na uongozi kwa ajili ya watu. Makosa machache ya Nyerere kamwe hayatafanya wema wake usahaulike katika mioyo ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla.
 
Mkuu

Unaweza kumpenda na kuandika utakavyo maana hakuna lilokuathiri katika familia yako. Kwa hao wanaohangaika kwa zaidi ya miaka 50 ,walioteswa , kuuliwa, kunajisiwa, kuchukuliwa kwa nguvu mali zao , kunyimwa haki zao , kuhama nchi yao waipendayo , Nyerere anabaki ni Mfitini mkuu
 
Unaweza kumpenda na kuandika utakavyo maana hakuna lilokuathiri katika familia yako. Kwa hao wanaohangaika kwa zaidi ya miaka 50 ,walioteswa , kuuliwa, kunajisiwa, kuchukuliwa kwa nguvu mali zao , kunyimwa haki zao , kuhama nchi yao waipendayo , Nyerere anabaki ni Shetani na Mfitini mkuu
Pole Mkuu. Naona mumeanza kujipanga upya kumchafua Mwl. Hata hivyo haitegemewi Nyerere apendwe na kila mtu
 
Hana agenda nyingine zaidi ya kumchafua Baba wa Taifa; Jemadari Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mwiteni hata St. mtu aliyeliteka taifa jengine na kuwaadhibu raia zake kwa zaidi ya miaka 50 na bado wanateseka . Hata hitler bado kuna watu wanampenda au hujui ???
 
Unaweza kumpenda na kuandika utakavyo maana hakuna lilokuathiri katika familia yako. Kwa hao wanaohangaika kwa zaidi ya miaka 50 ,walioteswa , kuuliwa, kunajisiwa, kuchukuliwa kwa nguvu mali zao , kunyimwa haki zao , kuhama nchi yao waipendayo , Nyerere anabaki ni Shetani na Mfitini mkuu
Mkuu yawezekana unayasema yana ukweli flani ndani yake, lakini hatuwezi kumtwisha Nyerere zigo lote hilo, kumbuka nchi ina taasisi. Zanzibar ina serikali yake, kwa nini unamsema Nyerere

Akina nani hao walioteswa, kuuliwa, kunajisiwa na mali zao kuchukuliwa kwa nguvu na Nyerere alihusikaje? Kwa jamii zilizo staarabika siyo vizuri kuyatumia makosa madogo madogo ya serikali zilizopita kwa faida za kisiasa nk. Lakini ukumbuke kujenga Taifa kama ilivyo Tanzania siyo kazi ya mchezo. Ndiyo maana Tanzania unaweza ukakuta Mkristo anaitwa Juma, Hamis n.k ama Muslam anaitwa Walliam na wanakuwa comfortable kabisa. Unaweza ukafikiri ni jambo dogo lakini viongozi wa kwanza wali- invest hekima na busara. Kwayo huenda hao unaowasema walikuwa wanakwamisha juhudi za ujenzi wa Taifa.
 
uloleta hii mada kifupi tukwambie tu kuwa unafeli sana,hautofanikiwa na huu mkakati wako,uzanzibar wako peleka huko huko,kwani nani unahisi anautaka huu muungano/sie pia hatuutaki,wafia dini bwana,umuache mzee wetu apumzike kwa amani,binafsi sitosita kusema kuwa katufanyia makubwa sana watanganyika,hata kama ana makosa aliyafanya ndio hayo yalifanya ubinadamu wake ukamilike,usipokuwa na makosa basi wewe si binadamu ni malaika,so kifupi nenda kafie mbele ya safari...
 
Nyerere ameshafariki tangu 1998 hiyo ni miaka 18 bado mnateswa na fikra zake mpaka leo?
 
Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

by RAIA MWEMAin HABARI

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya kuyatathmini maisha yake.

Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka aliyowahi kuyasema Mwenyekiti Mao wa China kumhusu Josef Stalin, mtawala wa pili wa Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin.

Nami nikayatumia maneno hayohayo kuanzia makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was "a great leader who made great mistakes," as one ruler once famously said of another.(“Julius Nyerere alikuwa “kiongozi mkubwa (adhimu) aliyefanya makosa makubwa,” chambilecho mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo mtawala mwenzake.)

Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake. Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki sifa.

Watu wa kale wasema: “Kheri ya mja ni ulimi wake na shari ya mja ni huohuo.” Kwa ulimi wake Nyerere aliwahi kutamka maneno ya maana na mengine ya kibahaluli. Baadhi ya maneno yake yalikuwa kama lulu na baadhi yalikuwa kama utumbo kama pale, kwa mfano, aliposema kuwa hakuna watu waitwao Waswahili. Nilimsikia akiyasema hayo alipotoa hotuba katika ukumbi wa London School of Economics alipokuwa ziarani London kabla ya kuuacha urais.

Yote hayo yaonyesha kwamba Nyerere alikuwa mja, mtu kama watu wengine. Hakuwa Mungu, hakuwa malaika. Wala hakuwa mtume na hata hakuwa mpigaji ramli. Na si kila alichokitamka kilikuwa sahihi. Lakini binadamu yule alikuwa na ulimi uliowalaza wengi na kuwafanya waache kufikiri kwani alikuwa na kipaji cha kuwafanya waamini kwamba kila alilolisema lilikuwa la kweli kabisa na hivyo hapakuwa na haja ya kumfanya mtu mwengine alifikirie. Ilikuwa nadra kumpata mtu aliyethubutu kumpinga au kumkosoa, hasa kadamnasi. Walikuwapo waliochelea kukiona cha mtema kuni na wengine waliridhia kuwa vibarakalla vya kuitika tu ‘hewala bwana.’

Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima.

Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na Tanganyika basi Tanganyika kutakuwa shuwari lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea kutafutana asili zao.

Tangu wiki iliyopita waandishi kadhaa wa Bara wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu; na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa Wazanzibari.

Wakoloni walipowaona wanaowatawala wanaungana kuwapinga, basi walitumia mbinu ya kuwagawa wazidhoofishe nguvu zao ili waendelee kuwatawala.

Mbinu kama hiyo inatumiwa siku hizi na baadhi ya viongozi wa CCM wa Bara pamoja na baadhi ya waandishi wa huko huko Bara ‘walioshtushwa’ na mwamko wa kisiasa uliowafanya Wazanzibari wawe na ujasiri wa kuujadili kwa mapana na marefu Muungano wa Tanzania.

Ujasiri huo umewafanya wengi wao waseme kwamba ama wanaupinga muundo wa sasa wa Muungano au hawautaki kabisa na wanataka Zanzibar iwe dola huru yenye mamlaka yake kamili.

Huo si mwamko wa leo au wa jana; tumekuwa tukiugusia miaka nenda miaka rudi lakini tukionekana kuwa ni wazushi na wazandiki. Sasa mambo yanajidhihiri yenyewe. Matokeo yake ni kwamba waliokuwa wakijidanganya sasa wamegutuka na hawajui jinsi ya kulizuia hilo wimbi la uzalendo Wakizanzibari minghairi ya kutumia hoja finyu za kikabila na udini.

Mmoja amefika hadi ya kuandika kuhusu ‘Waarabu’ na ‘watu Weusi’ kana kwamba hao wanaonasibishwa na uarabu ni wa rangi aina ya pekee iliyo tofauti kabisa na ya Wazanzibari wasio na asili ya Kiarabu. Mwandishi huyohuyo alitishwa na sura rahimu ya Sheikh Farid Hadi Ahmed, mmoja wa viongozi wakuu wa Uamsho.

Aliandika kwamba baada ya kuiona picha ya Sheikh Farid yalimjia mawazo kwamba Uamsho si jumuiya ya kidini na wala si ya Wazanzibari na kwamba Sheikh Farid ametumwa (hakusema na nani) kuwafitinisha Wazanzibari. Alichotaka kusema mwandishi huyo ni kwamba kwa vile Sheikh Farid ana asili ya Kiarabu basi Uamsho inataka kuurejesha usultani.

Ni uchambuzi uchwara, tena wenye kutumia lugha ya kibri. Unashtua kwa vile ni ‘uchambuzi’ wa hatari unaofanana na simulizi za Wahutu wa Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Hizi fitna za ‘Upemba’ na ‘Uunguja’, za ‘ubwana’ na ‘utwana’ na za ‘ugaidi’ wa Uamsho ni fitna zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya uongozi au ya uandishi.

Hila wanazotumia ni kwanza, kuwafitinisha Wazanzibari kwa kutia fitna za kikabila na za kidini. Kwa mfano, wanawatisha wahafidhina wa CCM/Zanzibar, wale wenye kusherehekea kaulimbiu ya ‘Mapinduzi Daima’, kwa kuwaonya ya kuwa Uamsho ina “msukumo wa kiarabu” na kwamba kusudio lake ni hatimaye kuyapinga Mapinduzi na kuirejesha Zanzibar katika ‘utumwa’. Maneno ya kijinga kabisa.

Hila yao ya pili ni kuwagonganisha vichwa Waunguja na Wapemba kwa kutumia hoja zisizo na mshiko wowote wa kimantiki. Wanasema wamewapata Wapemba wengi wenye kutaka Muungano uendelee kama ulivyo. Wamewahoji na matamshi yao kusambazwa na magazeti fulani nchini. Huu ni mfano mzuri wa propaganda ya kitoto.

Hila yao ya tatu ni kutumia lugha kuparaganya mambo. Ingawa Uamsho ni jumuiya kamili wao badala yake wanasema kuwa hiki ni kikundi. Sio kundi bali ‘kikundi.’ Na wanaishtumu jumuiya hiyo kuwa ‘inawatumia’ baadhi ya vijana kufanya vitendo vya kihuni vya kuchoma moto makanisa. Hakuna ushahidi wa hili.

Nne, wanajaribu kuwatisha Watanzania na hasa wakuu wa dunia hii kwa kuifananisha Jumuiya ya Uamsho na mitandao ya kigaidi ya Al-Qa’eda, Boko Haram na Al-Shabab. Bila ya shaka wenye kueneza fitna hii hawajui walisemalo na wanajikashifu si mbele ya Watanzania wenzao tu bali hata machoni mwa balozi za nchi za Magharibi.

Sijui kama wanaelewa ya kuwa maofisa wa baadhi ya balozi za Magharibi wameshakutana na viongozi wa Uamsho katika juhudi zao za kuitathmini Jumuiya hiyo na wanayaelewa makusudio halisi ya Uamsho.

Kwa hakika, kinyume na wanavyoandika baadhi ya waandishi wa Bara, Jumuiya ya Uamsho haikuzuka juzi. Imekuwako kwa muda wa takriban miaka 10 sasa. Jumuiya hii ni kama mwavuli ambao chini yake kuna jumuiya mbalimbali za Kiislamu, pamoja na ile ya maimamu.

Uamsho imekuwa ikiendesha harakati zake kwa msaada wa taasisi za nchi za Magharibi. Ilikuwa miongoni mwa waangalizi rasmi wa Uchaguzi Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.

Kati ya wafadhili wa Jumuiya hiyo katika harakati hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa uchaguzi uliopita.

Wenye kujuwa mambo watakwambia kwamba kuna tofauti kubwa kama ya mbingu na ardhi kati ya jumuiya ya Uamsho na mtandao wa Al-Qa’eda au kundi la al-Shabab. Huwezi kabisa kuzifananisha falsafa zao au makusidio yao. Hata Boko Haram nayo licha ya mbinu inazozitumia inatofautiana sana na al-Qa’eda.

Huko Zanzibar mafatani hawa wana washirika wanaojulikana. Nao ni wale wanaochomwa na kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Ndiyo maana wakaruka harakaharaka kuwatupia lawama za machafuko ya hivi karibuni viongozi wa CUF waliomo kwenye SUK na kutaka watimuliwe kutoka serikalini. Na ni wao waliohusika na vipeperushi vilivyotolewa wiki iliyopita kuwafitinisha Wapemba na Waunguja.

Na ni haohao wenye kujaribu kuwachimba waasisi wakuu wa Maridhiano yaani Rais mstaafu Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.

Inasikitisha kuwaona baadhi ya Wabara wenye kujigamba kuwa ni wasomi wakitaka mijadala ya kisiasa ipigwe marufuku katika majukwaa ya kidini. Hawaelewi kwamba ni dhima ya dini za Ukristo na Uislamu kuzungumzia na kuyatafutia ufumbuzi mambo yanayoyagusa maisha ya kila siku ya waumini wa dini hizo. Na mambo hayo yawe yepi kama si ya kisiasa?

La kutisha ni kuwa ‘wasomi’ hao wanamtaka Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua za kimabavu wakuu wenzake walio serikalini kwa kisingizio kuwa ati wanaunga mkono harakati za Uamsho.

Ulimwengu haukufunga macho wala haukuziba masikio. Unawaona na kuwasikia. La ajabu ni kwamba wanasiasa na waandishi wenye kuchochea hisia kama hizo wamesahau ni nyakati gani tulizo nazo na ni ulimwengu gani tulio nao. Katika ulimwengu wao wa leo Wazanzibari wanasema hawakubali tena kugawanywa kwa propaganda za kikabila au za kidini.

Inatisha kwamba kuna wanasiasa na waandishi waliosahau kwamba siku hizi kuna Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) na mahakama nyingine mahsusi za kimataifa, mithili ya ile Mahakama Maalumu ya Sierra Leone. Mahakama kama ile ya Sierra Leone inaweza kuundwa mara moja na Umoja wa Mataifa kuwatia adabu wenye kupalilia fitna zinazoweza kuzusha mauaji ya kimbari.

Ni hiyo Mahakama Maalumu ya Sierra Leone iliyomhukumu Charles Taylor, rais wa zamani wa Liberia, kifungo cha miaka 80 baada ya kupatikana na hatia ya kuishushia nakama Sierra Leone.

Dhana waliyonayo baadhi ya wasomi na waandishi wa Bara ni kwamba viongozi wa Uamsho ni mijitu isiyosoma. Kuna mmoja aliyepandwa na jeuri na kuandika kwamba mbali na kujua kusoma Qur’an viongozi hao ni watu wasiojuwa kuandika wala kusoma.

Ukweli ni kwamba viongozi wa Uamsho ni wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na wana shahada za juu za uzamili katika fani mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote — za dini na dunia.

Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur’an pia alisomea taaluma ya hali ya hewa.

Baadhi yao walisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako walivutiwa na hotuba za kidini za Professor Malik, mtaalamu wa fani ya hesabati, ambazo ziliwashajiisha na kuwafanya wawe na mwamko wa Kiislamu. Wengine walisoma kwenye vyuo vikuu vya nje vikiwemo vile vya Sudan, Saudi Arabia na Qatar.

Ni wazi kutokana na ripoti na taarifa zao kwamba baadhi ya wasomi na waandishi wetu wa Bara wanawadharau Wazanzibari. Nadhani hizo dharau zao ndizo zinazowafumba macho wasiweze kuona nani hasa aliyechochea fukuto hili la upinzani dhidi ya makandamizo ya walioshika hatamu za utawala wa Muungano.

Maandishi yao yamebainisha wazi kwamba hawaamini ya kuwa Unguja na Pemba si majimbo wala koloni za Bara. Inakirihisha kuona namna wengi wao wanavyozitapika hadharani chuki zao (na udini uliowapamba) bila ya hata staha na uvumilivu wa kimaadili.
Makala hii ya Ahmed Rajab Mzanzibari Mzalendo ilitoka kitambo kiasi cha kuwa historia, lakini kukumbushanda ni wajibu kwa mtu mwenye kusikia. Lakini katika makala hiyo kuna chumvi mwandishi ilio mponyoka kidogo.
1."Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur’an pia alisomea taaluma ya hali ya hewa" Msellem hakusomea wala si mtaalamu wa Hali ya hewa ila anafanya kazi Mamlaka ya Hali ya Hewa
2."viongozi wa Uamsho ni wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na wana shahada za juu za uzamili katika fani mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote" Lakini amesahau kusema kuwa pia kuna wachunga Punda waliobobea.
 
mwenye kujitambua hawezi kufungwa na falsafa za kufunga mawazo za mpuuzi fulani na kuacha kuutafuta uhuru..
ushirikiano wa chui na fisi ni wa kinyonyaji tu, nafuu uwe mpweke kuliko kuzungukwa na ushirikiano na mapenzi ya fisi..
 
Mwiteni hata St. mtu aliyeliteka taifa jengine na kuwaadhibu raia zake kwa zaidi ya miaka 50 na bado wanateseka . Hata hitler bado kuna watu wanampenda au hujui ???
Mtamchukia Nyerere lakini hamwezi kubadili ukweli kwamba mnajiita "Wazanzibari" kwa sababu yake!
 
Back
Top Bottom