Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na Tanganyika basi Tanganyika kutakuwa shuwari lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea kutafutana asili zao..
Ukitaka kujua ''unafiki wa wa wazanzibar'' soma habari hiyo kisha sikiliza hotuba hii
Kumbuka hii makala imeandikwa na mtu tunayemjua kutoka London na siyo Gavana
Nyerere aliongelea pande zote, znz na Tanganyika
Mwandishi amechukua sehemu tu na kuifanya ndiyo hotuba ili Nyerere aonekane anawafitini wznz. Kachukua kasehemu ili kutengeneza kesi dhidi ya Nyerere
Mwandishi alifanya hivyo akiwajua wznz, na anawapata kila siku
Anafahamu uwezo wao na wapi pa kuwalaghai.
Kitu kimoja ambacho hatusikii kutoka kwa kiongozi yoyote wa ZNZ iwe chama tawala au upinzani ni neno 'vunja muungano'.
Hata mwandishi hajawahi kuandika makala ya namna hiyo.
Wote siku zote wanataka muungano, nyuma ya pazia wanazungumza kinafiki
Walikuwa na fursa Dodoma, kwa unafiki wakakataa, leo wanalaani muungano
Mwaka 2010 wakandika katiba, hakuna aliyethubutu kusema hataki muungano.
Kusema znz ni nchi haitoshi, nchi ina sifa zake.
Nyerere si tatizo, tatizo ni wznz na mambo ya kinafiki wakimsingizia Nyerere