Nyerere na Wachina waliwezaje kujenga reli ya TAZARA kwa miaka minne tu KM zaidi ya 2000?

Nyerere na Wachina waliwezaje kujenga reli ya TAZARA kwa miaka minne tu KM zaidi ya 2000?

Mradi ulitakiwa kukamilika Nov. 2019 na Des. 2019 tulitakiwa kwenda Moro toka Dar kwa treni ya umeme. Kwa sasa hata tambo hamna na haijulikani ni mpaka lini. Kama kasi itakuwa hivi inaweza kufika 2025 ikiwa bado
Hivi si walisema kufikia September 2020 tungekuwa tunapanda treni ya SGR kwenda Morogoro?
 
Achana na watu wenye yale macho!
Diet yao iliruhusu wao kula mazagazaga yote ya porini, n'ge, panzi, nyoka, kobe sijui nguchiro n.k 😀
Mturuki siyo mporipori, nafikiri ishu ni kuishi porini, hawa wanazurula sana mitaani wakitafuta vipochi manyoya.

Everyday is Saturday................................ 😎

..Wikipedia wanadai wakati ujenzi umepamba moto walikuwepo Wachina 13500 wakifanya kazi ktk mradi.

..Pia GHARAMA za ujenzi wa Tazara ambayo urefu wake ni 1860 km kwa viwango vya leo ni usd 2.67 billion.
 
Wanashinda Sana terminal pub hao jamaa
 
Wachina walikuwa zaidi ya 50000 na 65 kati yao walikufa na kuzikwa Gongo la Mboto
..Wikipedia wanadai wakati ujenzi umepamba moto walikuwepo Wachina 13500 wakifanya kazi ktk mradi.

..Pia GHARAMA za ujenzi wa Tazara ambayo urefu wake ni 1860 km kwa viwango vya leo ni usd 2.67 billion.
 
..Wikipedia wanadai wakati ujenzi umepamba moto walikuwepo Wachina 13500 wakifanya kazi ktk mradi.

..Pia GHARAMA za ujenzi wa Tazara ambayo urefu wake ni 1860 km kwa viwango vya leo ni usd 2.67 billion.
Takwimu za kibeberu, hawakuwa wachina pekee, walikuwepo wachina na vibarua wengi wenyeji.
Sasa hawa waturuki wanashindwaje nao kuongeza idadi, maana kama wapo wengi team yote na vibarua ni 5,000...200 kilometre miaka mi4, hazitandikwa taruma...
Inakumbusha zile hesabu za watu 10 hulima heka 7 kwa siku 3, je, watu watano watalima heka 5 kwa siku ngapi? 😀

Everyday is Saturday................................😎
 
..Samahani.

..Wanasema wakati ujenzi umepamba moto mwaka 1972 walikuwepo wenyeji 38,000 na wachina 13500.

..Mimi nalia na hapo kwenye GHARAMA ambapo wanasema Tazara ilijengwa kwa usd 2.67 billion kwa fedha za leo.
 
Maufuli alisema Wachina wanatupiga kwa Trilioni 16 akawakataa. Kasi ya SGR kwa sasa ni ya mwendo wa konokono. Amini nakuambia, SGR itakapokwisha itatumia mara mbili zaidi ya hizo Trlioni 16 alizotaa Magufuli. Watch the SGR space.
Pesa ndio issue,kwanza Magufuli alitaka kujenga Dar to Moro tu kwa pesa zetu wenyewe,halikuwa tatizo,lakini kabla hajaanza akabadirisha mawazo kutoka diesel locomotive kuwa High speed electric drive kuitofautisha na SGR ya Kenya.
Wakati anaanza kujenga akaja na mpango wa kuhamishia makao makuu ghafla Dodoma.Ndio ukaonekana umuhimu wa kujenga kipande cha Morogoro hadi Makutopora ya Singida.Laiti kama angeanza kujenga Reli bila kujenga makao makuu Dodoma labda ingekuwa imeishafika Tabora.
Lakini shida nyingine kwa mjomba Magufuli ni kupanua miradi mikubwa mipya kwa kutegemea pesa ya ndani zaidi.
 
Reli ya Tazara sio SGR wewe.
Sikia hili kopo la kijani yani wamepumbazwa hadi akiri zimehama haya sasa twambie Tazara ni gouge ipi Naona wakiimbiwa awamu ya tana imejenga SGR kwa mara ya kwanza wanadhani nikitu kipya kwa taarifa yako SGR ipo Tanzania kuanzia 1971!! Reli ya kati ndiyo haikuwa na SGR , Serikali ya Awamu ya Nne ilianza mradi wa ujenzi wa SGR nakupeleka mataruma kila mkoa!Sisi tunaofanya kazi Raily tunajua hivyo hamna lakutwambia!
 
Kwani sasa hivi tunajenga kwa fedha zetu za ndani au mkopo? Maana mpaka sasa tumeshakopa 3.1t. Pitia vyanzo vyako vya habari tena.
Kwani zile mikopo zilizotoka StanChart sijui Stanbic za kujengea reli zimepelekwa wapi?? Reli imekopewa mpaka huko vipande vya Manyoni Itigi,
Nilifikiri ingeanza kuchangia kwa kutoa huduma, huku Dar-Moro, tungeanza kuchangia, ila nadhani hakuna umeme wa kuisukuma au?? Itakuwa tu kama treni yetu ya Kigoma.

Ile mikopo kwani Paymaster kazishikilia tu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
hekalu la jelusalem lilijengwa kwa muda gani? kitu chenye ubora kinahitaji muda ili kidumu kwa vizazi sio kulipua tu watanzania tuache haraka usipotumia wewe hata mwanao atakuja kutumia
 
Je, kuna hujuma za muda wa kukamilika mradi unaofanywa na makandarasi?

Reli ya TAZARA ilipitia njia ngumu Sana yenye milima na mabonde mengi. Lakini mradi ulichukua muda mchache Sana.
Ilijengwa kwa miaka tokea '70 mpaka '75 tu. Yenye taaluma za zege Kama hii ya kisasa.

Kilomita zaidi ya 1800
Kwa Kasi ya mradi wa Sasa inaweza kuchukua miaka 25 Hadi 30 reli kufika kigoma.

Ni vyema Miradi ya serikali iwe na time limit sio mradi unaanza hujulikani utakamilika lini.

Wachina kupitia Exim Benki walihaidi kutoa mkopo wa tilion 16 kumaliza mradi wote. Kwanini wasiutoe tu kwa pamoja huo mkopo ili wakandarasi wagawiwe vipande uishe kwa muda mfupi uanze kuingiza pesa turejeshe Deni lao kwa wakati.
1601903591603.png
1601903616326.png
1601903642187.png
1601903681629.png
1601903745831.png
1601903783403.png
1601903818698.png
1601903844289.png
1601903861764.png
1601903896798.png
1601903925545.png
1601903957366.png
 
..wanasema Mchina alifanya survey ya reli ya Tazara kwa MIGUU na iliwachukua miezi 9.

..baada ya hapo waliingia mzigoni kama hawana akili nzuri na reli ikaisha ndani ya miaka 5!!

..Watanzania walikuwa wanafundishwa kazi na Kichina wakati ujenzi wa reli unaendelea.
 
Barabara ilijengwa na Marekani kama nakumbuka vizuri kampuni ilijulikana kama NERO T Construction company.

..mahali ambapo reli ya Tazara na barabara zinakutana wakandarasi wa Kichina na Kimarekani walitwangana makonde.😂😂
 
Mimi sina chama ila ila Rais Magufuli anakubalika sana kaka yangu.
Anakubalika na wauza mboga Yani, na nyanya chungu, wapika kimpumu na togwa, ,
Hao ni wapinga maendeleo ambao wanafurahi wafanyakazi wasipoongezwa mishahara.
 
Back
Top Bottom