Bwana Jela
Senior Member
- Nov 25, 2019
- 131
- 655
Anakubalika na wauza mboga Yani, na nyanya chungu, wapika kimpumu na togwa, ,
Hao ni wapinga maendeleo ambao wanafurahi wafanyakazi wasipoongezwa mishahara.
..wanasema Mchina alifanya survey ya reli ya Tazara kwa MIGUU na iliwachukua miezi 9.
..baada ya hapo waliingia mzigoni kama hawana akili nzuri na reli ikaisha ndani ya miaka 5!!
..Watanzania walikuwa wanafundishwa kazi na Kichina wakati ujenzi wa reli unaendelea.
Unaweza kuwa sawa mkuu, makampuni mengi ya construction Marekani ni ya Waitaliano na hata huko Italy.
Reli ya Tazara sio SGR wewe.
Uongo gani?Acha uongo kaka
Uongo gani?
😅😅😅😅
Hahahaha Siidhanii[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Hakuna post za umeme, ni internally generated electricity
Nafikiri hufuatilii hi habari vizuri, nenda pale ambapo wameshafanya majaribio uone kuna nini, non the less, vichwa(engines) za ttren tajwa zipo hapa tayari na ni za mfumo niliokuekewesha: haya, na wewe thibitisha yakoHahahaha Siidhanii
Unaweza kututhibitishia !?
Kwa Kasi ya mradi wa Sasa inaweza kuchukua miaka 25 Hadi 30 reli kufika kigoma.
TAZARA ilijengwa kwa miaka mitano(5).
Ujenzi ulianza 1970 mpaka 1974.
Kwa siye tuliokuwepo miaka hiyo Mchina alitaka kwanza ku prove duniani kwamba teknolojia yake , spidi yake na uwezo kiujumla uko poa.
Na kweli alifanikiwa kuonyesha spidi kali ambayo katika ujenzi wa reli bado haijafikiwa mahali pengi duniani.
Umbali wa mradi kutoka Dar es salaam mpaka Kapiri Mposhi ni 1,860km, hii ni sawa kwa wastani kujenga kilometa 372 kwa mwaka.
Au kwa kulinganisha ni kama kujenga reli toka DSM Mpaka Mpwapwa kwa mwaka mmoja tu.
Ni dhahiri kuwa Mchina aliweka nguvu kubwa sana ya kifedha katika mradi maana alijua dunia nzima inautazama .
Miaka hiyo Marekani ilikuwa ikiubeza mradi na kuuita "The bamboo railway" ili kuukatisha tamaa.
Lakini Tanzania, Zambia na China hawakurudi nyuma.
Uko sahihi.Kwenye hiyo link nimeona haya maneno ambayo nadhani siyo sahihi kabisa
Construction was begun in 1970 and operation commenced six years later. The line starts at the port of Dar-es-Salaam and crosses Tanzania in a south-west direction. It passes through a largely uninhabited area. Since the line opened, there has been industrial development along the line, including a hydroelectric power plant at Kidatu and a paper mill at Rufiji.
Uko sahihi.
Makala imeandikwa na mtu ambaye hayuko Tanzania.
Kidstu iko mbali sana na Mang’ula, reli inapopita.
Na paper mill iko Mufindi Soyo Rufiji.
Hivi Mkuu hujui kuwa makada wale huwa hawasomi kabla ya comments?? Na wanapojibu huwa hawajipi muda kutafakari bali kuhemkwa...Kwani tuko darasani hapa? Ameandika hapo juu takribani miaka minne. Kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 1970's na kukamilika rasmi 1975/6.
Una swali lingine?
Ndo maana hiyo reli haikatishi barabara popote toka Dar mpaka Kapiri Mposhi mwisho ila inapita chini ya barabara kama ilivyo pale Makambako na mbele tena kabla hujafika Mbeya. Wachina walichimba pale kupitisha reli yao bila kugusa barabara ya Wamarekani ambayo ilikuwa tayari inatumika sehemu ile. Wakati reli na barabara vinajengwa uhusiano kisiasa kati ya Marekani na China ulikuwa mbaya sana lakini ilikuwa lazima watimize majukumu waliotumwa na nchi zao ndo maana masumbwi yalitumika kila kazi zao zilipokutana. Kwa jumla Wachina walifanya kazi nzuri sana kwa muda mfupi maana kazi ya kujenga reli ilikuwa ngumu zaidi kuliko barabara vyote vikianzia sehemu moja na kumalizikia sehemu moja nyingine. SGR wangeachiwa Wachina ingekuwa imefika mbali na kazi nzuri maana wana uzoefu wa kujenga reli za kisasa ingawa yetu siyo ya kisasa spidi yake ni sawa na gari lolote dogo...mahali ambapo reli ya Tazara na barabara zinakutana wakandarasi wa Kichina na Kimarekani walitwangana makonde.😂😂
Wakijibu hili nitagCHADEMA mmepanga lile banda la kufugia kuku mnalotumia kama makao makuu kwa miaka mingapi?