Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

We bibie ukianzisha bendi ya taarabu utaimudu vizuri sana. Kipaji unacho. Hongera sana kwa kujaaliwa hicho kipaji. Ni ushauri tu......

Achana na mimi, jibu hoja zangu kwa hoja.
 
Kwani kabla ya Nyerere kilikuwa hakitumiki rasmi? ni nani alikudanganya, nilikuwepo kabla ya Uhuru na ndiyo lugha ikitumika Tanganyika.

Siyo kila kitu kinachotumika kinatumika rasmi, wala kiswahili kilikuwa hakitumiki sehemu zote Tanganyika kabla ya uhuru, kuna watu wengi tu walikua hawajui kiswahili. Hata kama ulikuwepo kabla ya uhuru usitutishe, ulikuwa kijijini kwenu na inawezekana ulikuwa hujawahi kusafiri kwenda mikoa mingine.
 
pamoja na kwamba nimemsamehe NDUGU NYERERE makosa yake mengine yote , lakini naapa kwamba HILI LA KUTUACHIA CCM SITAMSAMEHE MILELE !

Ulitaka atuachie nini mkuu? Hivi wewe ukiwa na watoto ukawalea kwa maadili mema lakini kwa wendawazimu wao tu wewe ulipoondoka wa kaanza kuwa wehu, unataka jamii ikihukumu wewe baba Yao kwa makosa yawatio wako?
 
Acha ubishi bhana! Nani alituunganisha watanzania wote na kutumia lugha ya Taifa?

Yaani hivi ndo ulivyokaririshwa kweli Mkuu!? Duuh!

Hivi weye unazifahamu Dictionaries ngapi za hicho Kiswahili zilizotungwa hapo Tanganyika au Zanzibar...kabla hata yule Nyerere wenu hajazaliwa!?

Nyerere wakti anafika D'salam/Mzizima kwa mara ya mwanzo...alikuta tayari Watanganyika na Wazanzibary wakiishi kwa umoja,amani na upendo...na Kiswahili tayari kilikua kikitumika takriban maeneo yoote ya hiyo Afrika Mashariki na kati, kabla hata yule Nyerere hajazaliwa!

Nyerere angewezaje kuunganisha ati nchi nzima...wakti hata kuunganisha ile family yake chovu na kabila lake ameshindwa,mpaka anaingia kaburini!?

Au haya nyinyi hamuyafahamu/hampendi kuyasikia!?

Msitafute tukwambiani mangi...khalaf mtasema yakua ati twamkashif yule "Baba yenu wa Taifa"!

Au weye Mkuu,unafikiri Nyerere alikuta vita vya makabila wakti anafika Mwambao wa hiyo Tanganyika!?

Makabila mangi mno yaliokua yakipigana na kuuana hapo Tanganyika...hao wana asili/utamaduni wa kufanza hivyo for Centuries...na wamerithishana kwa generations mpaka kesho!

Nina rafiki yangu wa karibu mno na ni msomi wa hali ya juu...kabila lake nalihifadhi jina hapohapo Tanganyika! Basi hurejea hapo nyumbani kutoka Finland anakoishi kila mwaka...ati kuja kuhudhuria tamaduni za kucheza ngoma za kinyama/kishenzi...yaani kwa kutumia mapanga,pinde,mishale,marungu na mikuki...na kutoana damu/ngeu,kuziniana wake zao na kunywa pombe kupindukia! Duuh!

Mara kadhaa hurejea pale Finland akiwa na majeraha yake kutoka huko kwenye hizo "sherehe" za kinyumbani! Daah! Teeh! Teeh! Teeh!

Sasa,jamii/makabila kama hayo...yamefaidika vipi na kuwepo kwake yule Nyerere madarakani kwa ile takriban myaka-30!?...na khasa ukizingatia takriban hayo makabila yoote yenye unyama/vituko hivyo yanatokea jirani na huko huko atokeako yeye Nyerere mwenyewe!? Daah!

Ndo maana nikakwambia yakua...acheni kumpa yule Nyerere sifa za urongo/exaggeration!

Nyerere hivyo vyoote...yaani amani,upendo,lugha,umoja,ustaarabu,tamaduni,kusafiri na hata kuzungumza lugha kadha za kigeni/multi linguists na mangineyo mangi mno mema...yeye aliyakuta! Yaani haya tumerithi toka kwa Wazee Wetu!!

Punguzeni kupotosha jamii na Walimwengu! Daah!

Ahsanta.
 

Mpaka leo kuna ambao hawajui Kiswahili Tanzania hii.

Elimu ilikuwa duni wakati wake, mawasiliano duni, maendeleo duni. Leo hii Kiswahili kinakuwa haraka kuliko wakati wowote ule. Unalijuwa hilo?

Kiswahili ni lugha kuu aliyoikuta Nyerere ya mawasiliano Afrika Mashariki. Kikwete kaifanya kuwa ni lugha ya Afrika, unalijuwa hilo? hata kule kisipoongewa sasa kinafundishwa.
 
Huoni umemerekebisha?? mwanzo uliandika alikuja akitokea Butiama, sasa hivi umesema alikuja akitokea Tabora. .
Ninaposema katokea Butiama namaanisha alipozaliwa, chukuwa darsa kiduchu kutoka kwa Ritz

Nyerere, kwa mara ya kwanza kufika Dar ni mwaka 1952 alikuja kwenye mkutano wa TAA kama mjumbe kutokea Tabora.

Na mtu aliyempokea ni Aziz Dossa.

Mwaka 1954 ndiyo alikuja rasmi Dar na kupokelewa na Abdulwahid Sykes pamoja na wazee wa Dar.
 
Last edited by a moderator:

Hao waliokuwa mjini (Dar) walifanya nini kuunganisha Tanganyika Territory dhidi ya mkoloni kabla ya ujio wa Nyerere mjini?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Upende usipende mwl.Nyerere alitoa mchango mkubwa sana kutuunganisha kwa kutumia lugha ya kiswahili.
 
Hahaha!!!! Ritz kumbe weye ni mkwaya au ? Nyerere alitoa mchango mkubwa sana kwenye kiswahili mpeni tuzo.
Nuruyamyonge.

Ebu msome kiduchu Nyerere mwenywe ambae mnasema kawaunganisha watanzania wote kwenye kiswahili.
Nadhani umejionea mwenyewe amekiri kuwa kiswahili hakijui vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Nuruyamyonge.

Ebu msome kiduchu Nyerere mwenywe ambae mnasema kawaunganisha watanzania wote kwenye kiswahili.

Nadhani umejionea mwenyewe amekiri kuwa kiswahili hakijui vizuri.

Yule alikuwa msomi ikitumia falsafa kama uwezo wako ni mdogo huwezi kumuelewa Nyerere.uwezo wake huo wa unyenyekevu uliwafanya wazee wampe uzee wa heshima mwl.
 
Last edited by a moderator:

Kwa jinsi Nyerere alivyokuwa mjamaa na aliyetaka umoja isingekuwa rahisi kuruhusu vyama vingi kipindi kile.Kwa kweli jamaa wa CCM wanatupelekesha mno na wananchi tunatia pamba na pilipili machoni.Siku ya ukombozi tunaisubiri kwa hamu.
 
Yule alikuwa msomi ikitumia falsafa kama uwezo wako ni mdogo huwezi kumuelewa Nyerere.uwezo wake huo wa unyenyekevu uliwafanya wazee wampe uzee wa heshima mwl.
Teh teh teh!!! msome tena hapa chini kiduchu.
Hakuna aliyekataa kuwa alikuwa siyo msomi hawa wazee walikuwa waungwana sana pamoja nyie kuwatukana kuwakejeli lakini angalia alivyokuwa wanaishi na hawa wazee, wala hawa wazee walikuwa hawaitaji sifa walikuwa wanaishi nae kama kijana wao tu, haya maneno Nyerere kayesama mwaka 1985 wakati wengi hawa wazee walikuwa wameishatangulia mbele ya haki, sasa hizi falsafa unazotuambia alikuwa anamwabia nani.
 

Hili la Kikwete kuifanya lugha ya Afrika silifahamu!!,,najua kiswahili kimeanza kukubalika Afrika lakini siioni role ya Kikwete katika kufanikisha hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…