Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Kuna lugha ya biashara na kama huijui basi bora uwe mfugaji uongee na mbuzi tu [emoji1] [emoji1787]
 
Ahahah sura ngumu Tena jamani mkuu. Anatakiwa akija mteja anasimama na kutabasamu huku akimkaribisha. Lugha ni kibebeo kikubwa kwenye bihashara, inafuatia nyenzo.
Linawezekana sana
Kuna mama ana duka la nguo na mbaba mmoja nae ana duka la nguo na manukato na vinginevyo

Sasa yule baba anauza sana na wateja hawaishi kwake
Yule mama hasira anaapa eti yule baba ni mchawi
Lakini ukiwaona huyo mama ni mvivu kakaa tu hata ukiingia dukani hachangamki

Ila huyo baba anaijua biashara yake ukiingia na 20,000 unataka kitu utatoka amekupa na mafuta uzuri ya wife, na hata ulikuwa hautaki ila anakuambia hata kama huna chukua tu utaleta

Hakuna anaemdhulumu kwa ubunifu wake na maneno matamu
 
Aisee acha tu mkuu watu hawawazi kuwa wabunifu ni kuigana igana tu. Acha tu tuishi nao hivo hivo
Kati ya hayo maduka 4 unaweza kukuta wewe uliyakuta hayo 3 ulipoweka lako ndio yakawa 4,mjasiriamali mwingine kaona asogee muwe 5 unaanza kuleta zako 😄
 
Hivi kuwa na duka nako umeona umebuni..!!
 
Ebu jaribu kutofautisha maduka ya kariakoo na huku uswazi. Kule kuna mwingiliano mkubwa wa watu tofauti na uku mtaani ambapo watu wakipita unawahesabu kabisa.

Unakuta wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi shida ndio inapoanza apo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Pole, tafuta eneo lenye mzunguko hapo mtakesha mnavunja nazi tu
 
Umeandika kitu kizuri Mkuu, Kama una la kuongezea Fanya hivyo Tafadhali
 
Mkuu umeshindwa kua mbunifu unaanza kuja huku kulalamika ,

Sasa nani atakayekupa msaada wa malalamiko yako humu

Cha msingi ukipata mpinzani wa biashara unachotakiwa ni kua mbunifu zaidi na sio kuja kulalamika tu
 
Ulikuwa unanyanyasa wateja ndo maana wamekukimbia. Ukuenda stand daladala zimepanga foleni na hawachukuani weee unataka uwe na stationary peke yako Kijiji kizima.
 
Kwani location zingine huzioni mpaka un'gan'ganie sehemu ambayo watu umetukuta tunafanya biashara the same ambayo wewe unayotaka kufanya. Nyie ndio mnaoleta chuki na ushirikina. Why usitafute location nyingine
Mzee najua maumivu unayopitia kwasababu hata mimi nilishapitia hayo😭😭😭
 
Kwahiyo mkuu tunaotegemea hiyo biashara ya duka la mangi tunafanyaje
 
P4 ni rahisi sana kujibia mtihani
ila ukiingia mtaani sio rahisi kiivyo....kuna mengine mengi tu
 
Huyo alieiga ana akili sana ukitaka kuanzisha biashara nenda kaanzishe ambako biashara hizo zipo sababu wateja wanajua kuwa sehemu fulani kuna wauza simu sehemu fulani kuna wauza vitenge hivyo yani inakua rahisi kupata wateja
 
Huko ni kuleta uchonganishi kama vipi rudisha kodi yangu nihame
Sijui unatumia Nini kuwaza!unatakiwa ujue principle za biashara,mkiwa wengi wenye biashara zinazofanana ndio mtavutia wateja wengi Kwa kuwa wanajua vitu flan vipi mahali Fulani,ndio maana uliwa Dar utasikia mtu anataka spea ya gari anaambiwa naenda Ilala/karume mtu anataka nguo special ataelekezwa kko,anataka mtumba ataelekezwa karumeau Tandika,bro Mungu ndio mtoa riziki hata uwe peke Yako unaweza usiuze na mkawa wengi ukauza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…