Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Toa huduma nzuri, hakikisha mtu akiwa anatoka kwao anasema aloo kwa mo anatoa huduma kabambe, kuliko wale wengine. Kwetu Kuna maduka ya dawa kama 4, lkn huwezi amini Kuna duka la dawa ukienda we mwenyewe unafeel amani, basi Kila mtu anampa sifa. Na si kwamba yule mwengine hapati rizki, anapata vile vile kulingana na mola alivyompangia, na ana lugha mbovu balaa, kama ulienda unaumwa sana usipoangalia unakufa kabisa kabla ya huduma [emoji16][emoji16][emoji16] kwa jinsi alivyo na mijineno makali, hiyo ndiyo bihashara sasa, ni full ushindani.
Kuna lugha ya biashara na kama huijui basi bora uwe mfugaji uongee na mbuzi tu [emoji1] [emoji1787]
 
Ahahah sura ngumu Tena jamani mkuu. Anatakiwa akija mteja anasimama na kutabasamu huku akimkaribisha. Lugha ni kibebeo kikubwa kwenye bihashara, inafuatia nyenzo.
Linawezekana sana
Kuna mama ana duka la nguo na mbaba mmoja nae ana duka la nguo na manukato na vinginevyo

Sasa yule baba anauza sana na wateja hawaishi kwake
Yule mama hasira anaapa eti yule baba ni mchawi
Lakini ukiwaona huyo mama ni mvivu kakaa tu hata ukiingia dukani hachangamki

Ila huyo baba anaijua biashara yake ukiingia na 20,000 unataka kitu utatoka amekupa na mafuta uzuri ya wife, na hata ulikuwa hautaki ila anakuambia hata kama huna chukua tu utaleta

Hakuna anaemdhulumu kwa ubunifu wake na maneno matamu
 
Aisee acha tu mkuu watu hawawazi kuwa wabunifu ni kuigana igana tu. Acha tu tuishi nao hivo hivo
Kati ya hayo maduka 4 unaweza kukuta wewe uliyakuta hayo 3 ulipoweka lako ndio yakawa 4,mjasiriamali mwingine kaona asogee muwe 5 unaanza kuleta zako 😄
 
Nani anayetakiwa kuhama?? Aliyemkuta mwenzie au mimi?? Wewe huwezi kunikuta mimi nikifanya biashara the same ambayo unayotaka kufanya alafu uniamuru mimi nihame!!! Hilo haliwezekani kama huwezi kubuni biashara nyingine sio lazima kufanya biashara hujalazimishwa kaa nyumbani tulia
Hivi kuwa na duka nako umeona umebuni..!!
 
Ebu jaribu kutofautisha maduka ya kariakoo na huku uswazi. Kule kuna mwingiliano mkubwa wa watu tofauti na uku mtaani ambapo watu wakipita unawahesabu kabisa.

Unakuta wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi shida ndio inapoanza apo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Pole, tafuta eneo lenye mzunguko hapo mtakesha mnavunja nazi tu
 
Biashara ni kitu kinakuhitaji kuwa mpana sana wa idea.Unapaswa kufanya biashara leo huku ukiwaza kesho.
Hii ni kwasababu biashara yoyote yenye wateja ina shawishi watu wengine kuingia humo humo na huwez zuia hilo hivyo cha msingi ni kuhakikisha una grow (wewe binafsi) kwenye biashara unayofanya huku ukihakikisha biashara pia ina grow.

Uki grow wewe kwenye biashara utajikuta una namna ya ku acquire na kutengeneza loyal customers ambao utawafanya kuwa wako hata akose bidhaa kwako atakua radhi aache pesa kwako wewe ndio ukamnunulie kwa jirani (hapa kuna mengi ya kufanya).
So wenzako wanafikiri watagawana wateja na weww wanajikuta wanaambulia patupu.
WATEJA WANATENGENEZWA hawaji tuuu kama utataka biashara yako isi suffocate baada ya muda fulani.Ukitegemea kufungua biashara kila asubuh huku hujui wateja wanatoka wapi hilo ni tatizo kubwa. Hil hakuna darasa la kukufundisha , ni skills ambazo unapaswa kujifunza kwa kuisoma game ya biashara yako. Ndio maana voda wapo, tigo wapo na mwishon hallotel kaingia sokoni lakin huwasikii ma giant wakilalamika.

PIli u have to make sure biashara yako ina grow.Hapa napo kuna maelezo yake.

NB.
Kufanya biashara lazima kuambatane na kujifunza juu ya hiyo biashara yako kila siku.Sio kufungua na kufunga duka tuu.
Umeandika kitu kizuri Mkuu, Kama una la kuongezea Fanya hivyo Tafadhali
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Mkuu umeshindwa kua mbunifu unaanza kuja huku kulalamika ,

Sasa nani atakayekupa msaada wa malalamiko yako humu

Cha msingi ukipata mpinzani wa biashara unachotakiwa ni kua mbunifu zaidi na sio kuja kulalamika tu
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Ulikuwa unanyanyasa wateja ndo maana wamekukimbia. Ukuenda stand daladala zimepanga foleni na hawachukuani weee unataka uwe na stationary peke yako Kijiji kizima.
 
Kwani location zingine huzioni mpaka un'gan'ganie sehemu ambayo watu umetukuta tunafanya biashara the same ambayo wewe unayotaka kufanya. Nyie ndio mnaoleta chuki na ushirikina. Why usitafute location nyingine
Mzee najua maumivu unayopitia kwasababu hata mimi nilishapitia hayo😭😭😭
 
Hahahah iko hivyo yani. Ukija mtaa nnaoishi utacheka. Yani kila mtu anayefungua biashara ni duka la mangi, butcher, pharmacy🤣 sema maduka ya mangi ndio yamezidi 🤣🤣🤣!

Kwa haraka tu yapo kama 14 pamoja na la jumla moja ni 15 shops.
Kwahiyo mkuu tunaotegemea hiyo biashara ya duka la mangi tunafanyaje
 
Kheeeeeeeeee..!! Unapajua Kariakoo..!!?? Unajuwa kuna maduka mangapi ya nguo? KWani una hati miliki ya biashara husika kwa sehemu husika?

AU nikuulize, Dar to Mbeya kuana mabasi mangapi? Kama wote wangekuwa na roho mbaya uliyonayo kwenye hili, ingekuwaje kwenye hiyo biashara ya mabasi?

Wewe kule sokoni unakokwenda au unakotuma watu waende kununua nyanya, kuna wangapi wanafanya biashara ya nyanya..??

Hata mkiwa wengi kwenye eneo moja na biashara moja, fuata zile P nne ili uwashinde wenzio;
1. Place
2. Price
3. Product
4. Packaging

Mwanamke nyonga kwenye bia ilishawahi hamisha watu kutoka bia moja kwenda nyingine.
P4 ni rahisi sana kujibia mtihani
ila ukiingia mtaani sio rahisi kiivyo....kuna mengine mengi tu
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Huyo alieiga ana akili sana ukitaka kuanzisha biashara nenda kaanzishe ambako biashara hizo zipo sababu wateja wanajua kuwa sehemu fulani kuna wauza simu sehemu fulani kuna wauza vitenge hivyo yani inakua rahisi kupata wateja
 
Huko ni kuleta uchonganishi kama vipi rudisha kodi yangu nihame
Sijui unatumia Nini kuwaza!unatakiwa ujue principle za biashara,mkiwa wengi wenye biashara zinazofanana ndio mtavutia wateja wengi Kwa kuwa wanajua vitu flan vipi mahali Fulani,ndio maana uliwa Dar utasikia mtu anataka spea ya gari anaambiwa naenda Ilala/karume mtu anataka nguo special ataelekezwa kko,anataka mtumba ataelekezwa karumeau Tandika,bro Mungu ndio mtoa riziki hata uwe peke Yako unaweza usiuze na mkawa wengi ukauza
 
Back
Top Bottom