Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Nyie mnaopenda kuiga biashara za watu hebu jaribuni kuweni wabunifu, mnaleta chuki ipo siku tutakuja kuonana wabaya

Kwani location zingine huzioni mpaka un'gan'ganie sehemu ambayo watu umetukuta tunafanya biashara the same ambayo wewe unayotaka kufanya. Nyie ndio mnaoleta chuki na ushirikina. Why usitafute location nyingine
Kaka ukiendelea na hii roho utakuwa mchawi!maana umekazania sana Hilo la ushirikina ndio nyie mnaofunga biashara za watu,Sasa kabla hujafanya hivyo kumbuka mwenzio nae anatafutia watoto wake waende chooni.....mnaleta shida sana kwenye biashara nyie watu wa hivi
 
Mbongo Aisee ni mtu mwenye kichwa kigumu sana. Imagine mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna biashara kama nne zinazofanana we unaenda kuanzisha biashara hiyo hiyo, hivi hii inaingia akili kweli au mnataka watu tuanze kuitana wachawi??

Mtu unaona kabisa sehemu fulani kuna stationary na studio kama tano na wewe pia unataka unazishe stationary kisa tu umemuona fulani ana wateja wengi kwenye stationary na wewe umeamua kuleta biashara yako tuanze kugombania wateja mwisho wa siku watu tunaanza kuitana wachawi

Halafu isitoshe nyinyi mnaopangisha fremu utamruhusu vipi mtu afanye biashara the same kama wapangaji wengine wanafanya hiyo biashara, huko ni kuleta uchonganishi. Kugombanisha pasipo na sababu za msingi.

Hii kuigana igana biashara inatia hasira sana. Basi tu watu tunaamua kuishi hivo hivyo. Siku ya pili sasa wateja wamepungua sana ofisini kwangu. Itoshe kusema wabongo mnamauzi sana.
Pole sana mkurugenzi. Hata mimi nimepata changamoto kama ya kwako. Ila sijaona kama ni kikwazo kwangu.

Badala yake nimejipanga kuboresha huduma zaidi ili kuhakikisha nabakia juu siku zote. Biashara siku zote ndivyo ilivyo. Hakuna biashara ya peke yako. Na huwezi kumzuia mtu kufanya biashara aipendayo, hata kama amekuiga.

Unatakiwa kuwa mbunifu, na pia usifanye hiyo biashara yako kwa mazoea. Fanya kwa malengo ya kwenda juu zaidi katika kutoa huduma bora kwa wateja wako. Hakikisha una wateja wako wachache wa kudumu. Ongeza mashine za kisasa na pia huduma nyingine mfano miamala ya kifedha, nk. Acha kubweteka na kufikiri wewe peke yako ndiyo una haki ya kufanya hiyo biashara.

All in all, mpinzani wako ametumia udhaifu wako kukutikisa. Inawezekana hata customer care yako ni 0! Kwa hali hiyo wateja watakukimbia tu. Hivyo ukiona maji yako shingoni, hama hilo eneo. Ila siyo kukimbilia kwenye uchawi. Biashara wala haihitaji uchawi.
 
Kuna mzee mmoja hapa ddm yeye Ana Sera zake kwenye fremu zake za biashara hataki mfungue biashara za kufanana Kama Ni mpesa Ni mpesa tu Kama Ni vifaa vya umeme Ni umeme tu Kama Ni duka la dawa Ni dawa tu hvyo hvyo kwa kila biashara
 
Ubunifu gani ambao nimeushindwa mimi?? Nyie ndio mnaoleta nuksi na wanga ili sisi tulioanza tufeli ili nyinyi muendelee kuchukua nafasi yetu
Kwenye ulimwengu wa ushindani biashara dhaifu lazima ziangamie
 
P4 ni rahisi sana kujibia mtihani
ila ukiingia mtaani sio rahisi kiivyo....kuna mengine mengi tu
Kwahiyo, katika hayo mengine mengi, mojawapo ni kutaka Mtwara nzima genge la nyanya liwe la kwake peke yake? Wengine wahamie Katavi?
 
Mimi hii imenikuta bhana,watu mtaa mzima wanafanya hicho hicho,Ila kunawengine naona ni haki kabisa kucopiwa,Kuna jamaa alifungua hard ware nyumba inayofuata,alikuwa anapaki Gali mbele ya kiduka changu,anaenda kuchukua maokoto unasepa kwenye hardware yake ya mjini,alichokuwa anakosea ni alikuwa anabeba hela mkononi bila mfuko Wala bahasha,hahaa ! Alikuja kufungua mwingine nae anabiashara ya supermarket kubwa mtaa huo huo Vita iliyotekea hapo mmh
 
Kuna mzee mmoja hapa ddm yeye Ana Sera zake kwenye fremu zake za biashara hataki mfungue biashara za kufanana Kama Ni mpesa Ni mpesa tu Kama Ni vifaa vya umeme Ni umeme tu Kama Ni duka la dawa Ni dawa tu hvyo hvyo kwa kila biashara
Huyo Mzee mkamateni Kwa nguvu mumpeleke mirembe, jirani alikuwa na akili finyu kama huyo Mzee, alikuwa na frem nne Ila frem tatu zilimaliza miaka mitatu ziko wazi kozi kila mpangaji aliyetia Nia ya kupanga alikataliwa Kwa sababu anafungua Duka la takataka/mangi duka ambalo litafanana na mpangaji wa Kwanza, so Yule Mzee akaugua familiar ikampeleka Bush kutibiwa kienyeji, mwezi mmoja akiwa bush zile frem tatu zikapangishwa cha ajab mtaa ukazidi kuchangamka na wote walikuwa wanauza hakuna aliyekosa mteja.
 
Ukiangalia watu wengi wanao comment,,unakuta nae alicopy biashara ya mwenzio ,wengine ni watumishi hajawahi hata kuuza genge mwingine ndo yupo kwa shemeji yake yeye ni kula km kinda la ndege 😄,nenda sehem kaanzishe biashara yako pambana kutafuta wateja changamsha eneo alafu anakuja wanakuja km watu watatu kufanya kitu hicho hicho,utasikia kuwa mbunifu unaujua ubunifu ? Wewe ndo umeshidwa kuwa mbunifu kilaza wa kwanza
 
Ukiangalia watu wengi wanao comment,,unakuta nae alicopy biashara ya mwenzio ,wengine ni watumishi hajawahi hata kuuza genge mwingine ndo yupo kwa shemeji yake yeye ni kula km kinda la ndege [emoji1],nenda sehem kaanzishe biashara yako pambana kutafuta wateja changamsha eneo alafu anakuja wanakuja km watu watatu kufanya kitu hicho hicho,utasikia kuwa mbunifu unaujua ubunifu ? Wewe ndo umeshidwa kuwa mbunifu kilaza wa kwanza
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa una roho ya ajabu sana , kila MTU yuko huru kufanya biashara yoyote mahala anataka .
 
Daaah ungekua kariakoo ungekimbia frem yako. Kama mtaa wa Agrey mtaa mzima ni simu,kava na vifaa vya simu.
Kariakoo hupawezi kiongozi. Jaribu kufanya na ubunifu mwingine hap ulipo. Pambana
 
Wabongo sio wabunifu pia hawana jicho la kuangalia furusa zilipo that's why wageni wanatoka Asia na ulaya wanakuja kitajirikia huku.

Sisi tumekalia kuigana igana tu wakati mi-furusa mitaani iko kibao, akianzisha mama mmoja mtaani kukaanga mihogo utaona wamama wote wa mtaa nao wanaanza kukaanga yani ujinga mtu!
 
Wabongo sio wabunifu pia hawana jicho la kuangalia furusa zilipo that's why wageni wanatoka Asia na ulaya wanakuja kitajirikia huku.

Sisi tumekalia kuigana igana tu wakati mi-furusa mitaani iko kibao, akianzisha mama mmoja mtaani kukaanga mihogo utaona wamama wote wa mtaa nao wanaanza kukaanga yani ujinga mtu!
Kabisa kaka umeongea jambo la maana
 
Daaah ungekua kariakoo ungekimbia frem yako. Kama mtaa wa Agrey mtaa mzima ni simu,kava na vifaa vya simu.
Kariakoo hupawezi kiongozi. Jaribu kufanya na ubunifu mwingine hap ulipo. Pambana
Hapa sijaizungumzia maduka ya kariakoo. Bali nazungumzia maduka ya huku mtaani uwezi kuyafananisha na ya kariakoo kuanzia kodi ya pango, mwingiliano wa watu, mitaji nk
 
Back
Top Bottom