Upweke ndio unaumiza sana hata uwe na nini duniani lakini upweke ogopa sana ndio chanzo cha unconscious mind ni namna binadamu alivyoumbwa lazima afarijiwe na umri ukiwa unazidi kwenda upweke unaleta tishio sana katika nafsi zetu tutambue upweke ni hatari mno inaweza pelekea ukawa na urahibu wa pombe, madawa, sigara, umalaya na tambua mtu yoyote mwenye urahibu mfano wa umalaya ni mtu mpweke, ni mtu mwenye stress nyingi aidha ni visasi vya kukataliwa zamani hivyo ana amini anawakomoa kisa ana vipesa, uoga wa maisha kwa mabinti akiamini kwenye kuhongwa,tamaa ya maisha mazuri, umasikini aliopitia mhusika, uoga,ugumu wa maisha,kutaka asivyo na uwezo navyo, shinikizo la ndani na nje nk
ndio maana yeyote mwenye tabia za umalaya sio mtu mwenye furaha wachunguze vizuri, ataonyesha yuko poa kwa nje lakini sivyo anaigiza amini hilo hivyo inabidi wafanye umalaya wakiamini wanajifariji kumbe sivyo bado wanaumia upweke unawatesa.
Tazama wazungu wanavyojiua/Ya kwa risasi siku hizi ni upweke ndio chanzo wapo wanaoishi na wanyama kujifariji, wapo wanaokesha mitandaoni kuperuzi, lakini bado upweke unawatesa.
Harakati za maisha zina mengi yanayoumiza kuna wakati unahitaji mtu wa kuongea nae yale yanayosumbua roho yako lakini hayupo, tambua hakuna asiye na mipango ya mbele pale inapogoma au mambo kwenda sivyo unahitaji faraja ndipo hapo mapenzi uchukua nafasi hapa sasa ndipo unahitaji kupenda, kupendwa, kusikilizwa nk.
Tazama magerezani kesi nyingi za mauaji ni za mapenzi. wauaji wengi walikuwa na stress za upweke wa mapenzi zilizotokana na usaliti wa kihisia kwa wenza wao.
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app