Nyie watu Tumechoka na Ujinga wenu CCM - Tanzania siyo Backyard ya Familia zenu!

Nyie watu Tumechoka na Ujinga wenu CCM - Tanzania siyo Backyard ya Familia zenu!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Leo siandika kama mtu mstaarabu... naandika kama raia aliyekasirishwa Nchi hii imegeuzwa ya familia chache huku viongozi wetu wanafanya maamuzi ya kijinga

Unajua kinacho umiza zaidi? bado wanapewa madaraka juu juu na CCM eti waendelee kuihujumu Tanzania. We serious?

Unampa mtu aliyeshindwa hata kuongoza kijiji madaraka ya kitaifa? unampa mtu anayetishia watu kwa bastola, mtu anayepiga raia wasio na hatia, nafasi ya kuwa boss wa usalama wa taifa au jeshi la polisi?

Matukio ya kihuni na kinyume cha sheria:

Polisi kutekwa na kupigwa watu wanaodai haki yao — seriously? Ni polisi au ?

Mikutano ya wapinzani kuvunjwa kinyama, wakati mkutano wa CCM unalindwa kama Vatican.

Tundu Lissu, the real warrior, wanataka kumkamata wakidhani watazima mapambano. Hiyo ni kama kumwaga petrol kwenye moto! Hamfufui mtu mmoja, mnawasha kizazi kizima cha mapambano!

CCM, mnawezaje kuwa Mnadhani ku-control polisi, TISS na JWTZ kutawafanya mkae milele? Mnadhani kupora uchaguzi na kuharibu Katiba ni tiketi ya kuishi ikulu maisha yote?

Hakuna damu iliyomwagika bure hapa, na msijidanganye kwamba Watanzania wote wanaogopa virungu na risasi zenu za buku mbili.

Na kwa haya mliyopanga 2025, kutumia nguvu, kuiba kura, kutisha wananchi...
Mnaandika death warrant ya mfumo wenu wenyewe.

Wananchi wameamka. Hamtaki kuamini?

Hii nchi siyo ya baba zenu wala babu zenu. Tanzania ni ya WATU WOTE. Siyo ya mabeberu wa Magogoni wanaotumwa na mafisadi wenye viwanda vya unga.

Msipojifunza leo, mtajifunza siku mkikimbilia exile mkilia kama mapanya.

Tundu Lissu siyo wa kumkamata hovyo. Kila jaribio lenu linamfanya more powerful than ever. Mnajidhalilisha na kujidamge wenyewe huku dunia ikiwatazama kama clowns wa East Africa.

Na kwa taarifa yenu, sio kila mtu anashindwa, sio kila mtu anaogopa. Kuna mamilioni wako ready ku-ride or die kwa haki yao!


---
Tunawaangalia.

Na Mungu, Historia na Hasira za Watanzania ziko against y'all.

#Hatudanganyiki

#Ta
nzaniaSiyoFamiliaYenu

#FreedomOrDeath
 
Kuwa makini Tu .hasira hasara.



Subiri wakati WAko .utaongoza utavyoona.
 
Back
Top Bottom