Nyimbo gani umekua nazo na ukizisikia zinakukumbusha utoto au ujana wako?

Nyimbo gani umekua nazo na ukizisikia zinakukumbusha utoto au ujana wako?

Kanda Bongo Man _Muchana
Mbilia Bell - Nekei Naorobi
Chico_I need some Money
Sam fans Thomas_African typical Collection
Papa Wemba_Rail On
Yondo Sister _ Bazu
 
Umenikumbusha wimbo wake wa handsome, kama unao naomba tupia bro!!

Kipindi hiki nilikuwa tayari kijana wa 20's, "nipo na nitazidi kuwepo mpaka maisha yatopofika mwisho hapo....!!"
Enjoy mkuu... Hiki kipindi vijana wengi mlikua machekibobu😅
 
Nikisikiaga ule tintintiti nkikiki nkinkiiii kachakachakacha... Inankumbushaga mbali. Jina lake nimesahau
 
Hizi nyimbo Huwa zinanikumbusha kitambo.

Sugu -Maisha yangu.
Sugu ft balozi -Wabongo.
Sugu ft balozi &Afande Sele -Salama Alekum
Sugu ft jay dee -Mambo ya fedha.
Sugu -Nikianguka.
Sugu -Chini ya Miaka 18.

Mzee wangu alikuwa na albums za sugu side a ikiisha tuna geuza side b na betri za Panasonic pembeni.

General defao,
Baba kolza -Defao.
Famille kikuta -Defao.
Madova-Defao.

Tulikuwa tunajaribu kuiga staili zake na miondoko ya Kucheza, jamaa alikuwa vzrr kwa kudance.

Ilikuwa ikifika jioni watoto wamtaa tunashindana Kucheza nyimbo za defao na Koffi Olomide na Wenge &Awilo, Congo music's kipindi kile ilitukamata.

Dully Sykes -nyambizi. Huu nilikuwa naona wimbo kichaa,

Daznundaz -Kamanda.
Wimbo wa kumanda tulikuwa tunashindana kumeza misitari,

"Kamaandaa kamaanda eyoo,
Siku mapigo yangu ya moyo Mwisho yatapogota/
nuru itazima mfano nyota wa inavyondondoka/
Sitaweza kuamuka Tena macho yangu yatapofumba/
Safari imewadia nenda kwa baba yangu muumba/

Itakuwa huzuni kwa ndugu na masela/
safari yangu itapofikaa kwenda Hera/,
mtabaki mnaniiombea
Alezwa mapeponi kamandaa/
Alezwa mapeponi kamandaa/

Tulikuwa na pen pembeni kurudisha nyuma mashairi, kanda za tape.

Ndanda Kosovo, Fm academia -Chini ya ulinzi na binadamu.

Fainali uzeeni -African star's.

Kitendawili & Tunda -Mwinjuma Muumini.

Wimbo wa kitendawili mpaka Sasa nikiusikia Huwa napenda haya mashairi,

Dunia ni msangamano wa taabu nyingi sana/
zilizo changanyika na chembe chembe ndogo sanaa za raha/
ambazo hazikwahii kuyeyuka.

Maisha ni safari-Jaribu
Maisha ni wajibu-Timiza
Maisha ni fumbo-Fumbua
Maisha ni bahati-Ifumbate
Maisha ni mapigano-pigana
Maisha ni huzuni-Ishinde
Maisha ni tendo-lifanikishe.
Maisha ni siri-itatue
Maisha ni mtihani-Faulu
Maisha ni msibaa-Ukabiri
Maisha ni zawadii -Ipokee.


Kocha wa Dunia, Muumini.

Lucky dube -Prisoner Albums.
 
Bi shakila.

Nilikuwa na sister zangu Wanapenda taarabu ilibidi kusilikiza ili isiwe ugomvi wa redio castlle.

Bi shakila -Mapenzi yamepunguaa.
Bishakila -Macho yanacheka moyo unalia.
Bishakila -ukukataye hakwaambii Toka.

Sabah salum-Donge.
Khadija kopa,

Deborah -Chagua., tumecheza huu wimbo kama vijana wa kutumbuiza ndoa.

Azalaki awa -Gathos beevan, Tumeruka,na kuvuna jasho na wimbo huu.

Pamoja na Caz T ft Miss Sara.-Nakuhitaji,

Huu wimbo unakumbusha sherehe nyingi ziliupiga na njinsi jammaa walivyokuwa wakijibizana ilikuwa kwa uzuri sana.

Nakuhitaji Naam, Mpenzi wangu-nakuhitaji -unaniita.

Njoo kwangu utachotaka nitakupa, -utanipa.
 
Kohh kohh kohh
mshangazi pass me de weed imma about to say somethin real sh!t nigga
b0mb0..claa...aaa...aaa..ttt
#SMOKEY " ... can't be fu*** up the rotation, puff puff give 😂"

Walioangalia movie ya FRIDAY ya ICE CUBE wameelewa
 
Back
Top Bottom