Hizi nyimbo Huwa zinanikumbusha kitambo.
Sugu -Maisha yangu.
Sugu ft balozi -Wabongo.
Sugu ft balozi &Afande Sele -Salama Alekum
Sugu ft jay dee -Mambo ya fedha.
Sugu -Nikianguka.
Sugu -Chini ya Miaka 18.
Mzee wangu alikuwa na albums za sugu side a ikiisha tuna geuza side b na betri za Panasonic pembeni.
General defao,
Baba kolza -Defao.
Famille kikuta -Defao.
Madova-Defao.
Tulikuwa tunajaribu kuiga staili zake na miondoko ya Kucheza, jamaa alikuwa vzrr kwa kudance.
Ilikuwa ikifika jioni watoto wamtaa tunashindana Kucheza nyimbo za defao na Koffi Olomide na Wenge &Awilo, Congo music's kipindi kile ilitukamata.
Dully Sykes -nyambizi. Huu nilikuwa naona wimbo kichaa,
Daznundaz -Kamanda.
Wimbo wa kumanda tulikuwa tunashindana kumeza misitari,
"Kamaandaa kamaanda eyoo,
Siku mapigo yangu ya moyo Mwisho yatapogota/
nuru itazima mfano nyota wa inavyondondoka/
Sitaweza kuamuka Tena macho yangu yatapofumba/
Safari imewadia nenda kwa baba yangu muumba/
Itakuwa huzuni kwa ndugu na masela/
safari yangu itapofikaa kwenda Hera/,
mtabaki mnaniiombea
Alezwa mapeponi kamandaa/
Alezwa mapeponi kamandaa/
Tulikuwa na pen pembeni kurudisha nyuma mashairi, kanda za tape.
Ndanda Kosovo, Fm academia -Chini ya ulinzi na binadamu.
Fainali uzeeni -African star's.
Kitendawili & Tunda -Mwinjuma Muumini.
Wimbo wa kitendawili mpaka Sasa nikiusikia Huwa napenda haya mashairi,
Dunia ni msangamano wa taabu nyingi sana/
zilizo changanyika na chembe chembe ndogo sanaa za raha/
ambazo hazikwahii kuyeyuka.
Maisha ni safari-Jaribu
Maisha ni wajibu-Timiza
Maisha ni fumbo-Fumbua
Maisha ni bahati-Ifumbate
Maisha ni mapigano-pigana
Maisha ni huzuni-Ishinde
Maisha ni tendo-lifanikishe.
Maisha ni siri-itatue
Maisha ni mtihani-Faulu
Maisha ni msibaa-Ukabiri
Maisha ni zawadii -Ipokee.
Kocha wa Dunia, Muumini.
Lucky dube -Prisoner Albums.