Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Amina
Amina kadala
Sinowea(hata sijui ilikuwa ndyo nini)
Amina tumpepe tumpempe
Amina magereza magereza
Amina dush dushi karanga dushi

Mwingine
Shilingi ya Nyerere katikati kuna mwenge
Zunguluka nyuma utamkuta mwenyewe
Sobisobi sobi samwela sobisobi sobi samwela

Utoto wa zamani raha sana
 
Namtafuta rafiki rafiki rafikii
Rafiki yako naani naani naanii
Rafiki yangu Meendee Meendee Meendee
Huu mti gani, wa mchongoma
Nikiukata haukatiki
Hata kwa panga, haukatiki
Hata kwa shoka, haukatiki.
Hao watoto wenu wa ushuani wanaosoma st anne maria sijui mary....huku kwetu uswazi kama kawa, juzi nimewasikia wanaimba ukuti ukuti saa mbili usiku umeme ulikuwa umekatika.....hawakuacha mpaka uliporudi nikasikia HUOOOOOOOOOOOOOOOO!
 
Nataka kuzi-document kwa ajili ya watoto wa ndugu zangu walioko nje
 
Mimi mpaka leo najiuliza uhusiano wa nyimbo moja na tukio lililotokea huko US:

Mvua ikinyesha tulikuwa tunacheza kwenye mvua na kuimba, "Mvua njoo, katarina usije.....mvua njoo, katarina usije". Tuko wadogo, nadhani tulipokea/rithi hiyo nyimbo toka kwa wakubwa zetu; na ni miaka mingi nyuma, miaka mitatu minne nyuma tukashuhudia "Hurricane Katrina" na maafa aliyosababisha US; mvua inanyesha, moto unawaka!

Katarina/Katrina ni nini?
 
kioo kiooo alikivunja nani...
simjui simjui wamwisho akamatwe....

bonus track
Kinyuliii nyulika, mwanangu mwana wa jumbe
kavaa nguo mbili ya tatu kajitanda, aliye juu aondoke...

hizo mbili mkuu zinakamilishwa na matukio kadhaa ya vitendo.

ila ukitaka wa kizungu.
by shoo i love you bebiiii, the bebi to the shoooo.... etc
huu sikuunasa vizuri maana mtaani kwetu english tulikuwa hatuijui sio watoto tu bali hadi wazazi,dada na kaka zetu hata waalimu wenyewe walikuwa hawaijui.
 
Mimi mpaka leo najiuliza uhusiano wa nyimbo moja na tukio lililotokea huko US:

Mvua ikinyesha tulikuwa tunacheza kwenye mvua na kuimba, "Mvua njoo, katarina usije.....mvua njoo, katarina usije". Tuko wadogo, nadhani tulipokea/rithi hiyo nyimbo toka kwa wakubwa zetu; na ni miaka mingi nyuma, miaka mitatu minne nyuma tukashuhudia "Hurricane Katrina" na maafa aliyosababisha US; mvua inanyesha, moto unawaka!

Katarina/Katrina ni nini?
Katrina ilipiga tena miaka si mingi, ilijurudia baada ya kuacha majanga makubwa
 
Hao watoto wenu wa ushuani wanaosoma st anne maria sijui mary....huku kwetu uswazi kama kawa, juzi nimewasikia wanaimba ukuti ukuti saa mbili usiku umeme ulikuwa umekatika.....hawakuacha mpaka uliporudi nikasikia HUOOOOOOOOOOOOOOOO!
Ushuani watoto pia wanachelewa kuongea, Huku kwetu Kwamtogole msuto unaanza ukiwa na mwaka mmoja. Ukifisha miaka miwili wewe ni mtaalamu hata matusi unayajua.
 
Mimi mpaka leo najiuliza uhusiano wa nyimbo moja na tukio lililotokea huko US:

Mvua ikinyesha tulikuwa tunacheza kwenye mvua na kuimba, "Mvua njoo, katarina usije.....mvua njoo, katarina usije". Tuko wadogo, nadhani tulipokea/rithi hiyo nyimbo toka kwa wakubwa zetu; na ni miaka mingi nyuma, miaka mitatu minne nyuma tukashuhudia "Hurricane Katrina" na maafa aliyosababisha US; mvua inanyesha, moto unawaka!

Katarina/Katrina ni nini?
[emoji1] [emoji2] [emoji3] [emoji12]
 
Ushuani watoto pia wanachekewa kuongea, Huku kwetu Kwamtogole ndiyo inaanza ukiwa na mwaka mmoja. Ukifisha miaka miwili wewe ni mtaalamu hata matusi unayajua.
kuna katoto nilikua nacheza Nako kwa kukarusha juu Na kukadaka. Nakarusha tena Na kukadaka. Nilipo acha kakaniambia "acha us*nge nirushe tena" nikabaki hoi
 
Mdelemaaa mdelema iki waniwela mdelema
kadete aka wiza mdelema giti ulu kasumba kane mdelema...!!

Bhagh'wise sulagi machimu ngongo kwashilile sulagi....!

Kama sio msukuma wa Nassa sio rahisi kuelewa nyimbo hizi...
 
Back
Top Bottom