Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Yes.... womanity haijui hio

Waalaah wakiacha hizo party wanazoandaaga clouds kuzunguka nchi yote halafu wana mziki ndo wanakuwa wanaimba live, wangeandaa tamasha hili la nyimbo za zamani na watuachie tuimbe na kucheza wenyewe. Mbona mngeburudika hahahahaha maana nyimbo zote ningesema na marede yote ningecheza hadi mpira wa tobo bao ningecheza. Hahahahahaa bado zile sarakasi za kuning'inia kwenye bomba halafu unabiringita unatokelezea upande wa pili bila kuachia mikono. Hii niliifanya sana kutokana na kukua na kaka zangu.
 
Huo wa baishoo huku kwetu uswazi tulikuwa tunaimba hivi

Bai shoo I love you baby the baby tuthesa thesa tu Ze yona the yona tothem them to the yona
Therewaa tu three fo Kata kona
[emoji23] hata kwetu pia
 
Jieleze jielezee jieleze jieleze jieleze jieleze nshajieleza maamaa..
Mimi apa ni Juma mama yangu ni Aminaa baba yangu ni Hamisi nshajieleza maaamaa..[emoji23][emoji23]
Hapo unawekwa kati ujieleze miaibu kibaooooo[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ha ha ha kwa baba Taibali break ya saa nne tubavuka barabara kununua Sun Vita! Nimekaa moja ya mtaa off Malik sikutajii.
 
Old School Re-union...

Yeah, that would be great and funny, enzi zile majibu ya darasa la saba unayasubiria utasema umefanya interview ya Visa ya US unasubiri kama utapata visa au laah.

Jina limekaa vizuri.
 
Aisee Kasie kiboko....kibunzi nishaisahau. Sasa kuna ile....
Mali ya mdimu mali ya mdimu....
Saagaaa saaagaaa sagaaaaa....
Kubwikaaa....kubua...kusagaa cha kwanza cha pili cha tatu.....
 
Amina rabi Aminaaa,
Amina rabi Aminaaaa,
Hilo shipa la mzee ali, dakitari kalishindwa,
kalitandikia jamvi, alikate kachumbari,

wale watoto wa tabata kimanga na mawenzi, huu wimbo ulitushika sana miaka hiyo.
Wazee w kula daku.... hahahaha
 
Tumpeleke hosipitali
Asije kusema kwa baba yakee...
Yesa yeesa yesa
Waaaaaaaa........(sasa hapo kwenye WAAAAA ndo utam ulipo manake mnakutanisha viuno wakaka na wadada)
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee Kasie kiboko....kibunzi nishaisahau. Sasa kuna ile....
Mali ya mdimu mali ya mdimu....
Saagaaa saaagaaa sagaaaaa....
Kubwikaaa....kubua...kusagaa cha kwanza cha pili cha tatu.....
Hahahahaaa kibumzi rahaaa ikifika wakati wa kitajwa wachumba unakimbiaa kwa aibu uliyemtaja asikuone wakati anatajwa hahahahahahah
 
Katika zooote huu wimbo unanikumbusha mbali sana daaah!! Husna wera ayuu!!??
 
Bilinge bayoyo bilinge bayoyo
Bilinge bayoyo bilinge bayoyo
Tunamuomba Bujibuji aje hapa tumuone maringo yake bingilibingili mpaka chini!
Nilikua siupendii huu mchezo eti mtu anaingia kati anakata viuno yaan ilikua wakianza nasepa, bora nikacheze goroli tu.
 
Kama Dada wanipenda,kaninulie zeze,nikilala kitandani,zeze lanibembeleza,ahah amina,kusemasema kubaya,utamsema mmeo, aliyekupa hiyo mali
Sio utamsema Mkweo aliyekuzalia Mumeo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…