Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Inaendelea....
Dadaaaa Kasinde kuchomachoma kubaya utamchoma mkweo alikuzalia mumeo ti kamnyanga ti kamnyanga ti stelingi midabwada....

Hahahahaaa Hahahaaa hivi tunao changia huu uzi tukisema tukutane leaders club halafu tuanze kuimba hizo nyimbo heheheeee er ntacheka nahisi hadi nijikojolee heheheheheee

Itakuwa bonge la burudani, ila saa hizi hutoruhusiwa kuchungulia chupi tukiwa tunaruka kamba.
 
Anameremetaa Anameremetaa Anameremetaa Anameremetaa dada ana Anameremetaa Anameremetaa muoneni alivopendeza Anameremetaa

Tumpambe mauaa Iyeyee mauaa Tumpambe mauaa Iyeyee mauaa

Cc Smart911
 
Hahahaha hiyo tuliimbaa... Sijui huwa kuna muunganiko gani hapoo...afuu hivyo viyange yange sivioni tena!!!
Vipi zile ndege(plane) zilizokuwa zinaachia moshi mweupe angani zikipita unaimba ndege ya urusi hyooooo
Ndege wengi wamekimbia, Dar wamejenga hadi mabondeni ambako wale ndege walikuwa wanakaa, unakumbuka mbayuwayu ikifika jioni wanakatiza mtaani kimo cha mbuzi!
Zile ndege angani tulikuwa tunadanganyana ni roketi kumbe ndege za kawaida zinapita anga la kimataifa(halina mwenyewe) mfano ndege za SA zamani zilikuwa haziruhusiwi kupita anga la Tz hivyo inabidi ziruke juuu sana kwenye anga la kimataifa, ule moshi ni hewa ya moto kutoka kwenye engine ikikutana,na hewa ya baridi angani. Mfano ukienda Makambako watu wakiongea asubuhi utaona ule 'moshi'
 
tulikuwa tunawaita vinega
 
Nasakaa mke wangu....nasaka mke wangu,haaapa hayupo haaapa hayupo...kaeeenda wapi?...kaeenda wapi?,kaeenda kusuka..kaeenda kasuka,kachukuaa... nini? na nini?,kachukuaa chanuuuo na mafutaa
 
Nasakaa mke wangu....nasaka mke wangu,haaapa hayupo haaapa hayupo...kaeeenda wapi?...kaeenda wapi?,kaeenda kusuka..kaeenda kasuka,kachukuaa... nini? na nini?,kachukuaa chanuuuo na mafutaa
Aah umeruka mstari...
Chanuo kampa nani ? Chanuo kampa nani?
Kampa msusi kampa msusi....
Mafuta kampa nani? Mafuta kampa nani?
Kampa msusi kampa msusi...
 
Kinyuunyu kinyuunyu

Hello mambo, za mwananyamala....

Ulishawahi kucheza kibumzi kibumzi
Chameemee Chameemee
Halafu kika mtu anaulizwa kimya kimya ataje mchumba ake hahahahahahhaaa hapo sasa kama kuna kavulana unakapenda mtaani unakasema.

Halafu muimbishaji anaanza kutaja.

Nilonge nisilongeee loongaaaa
Nisemeee nisiseemeeee seemaaaa
Mwenzetu Kasie. .... mchumba ake....

Asprin basi watu eeehhh yeeeyyy hapo kama kulikuwa na kaschana kingine kanampenda basi ananuna. Na ukikuta kavulana na kenyewe kanakupenda basi kanaanza uchokozi mara akuvute nywele mara akidalike mara akufinye au akutekenye....

Basi wewe unajidai banaa niniiii mii staakiiiiii ntakusemea. .... Hahahahahahhahaaa ilikuwa raha sana. Hapo kama kavulana kababe mtaani huwezi kuonewa au kupigwa lazima akutetee. Asipokuona mtaani anakuja kukuulizia kwenu na siku kwao kukipikwa maandazi basi atakuibia moja akuletee uonje hehehehehehehhee

Those were innocent pure love.
 
Back
Top Bottom