Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Sobi sobi,sobi samwela
Nchi yetu ya Tanzania
 
Nilitiwa mkwara wa kuimbiwa kikojozi weeeh mbona sikunywa maji siku nzima ili nisijikojo lee..! Yaani niligoma kabisaa..! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mpaka mama akasema basi atukuimbii tena.. Ndo nikaanza kunywa maji..!
Cha kushangaza siku jikojolea tena..! [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Hahahaha hiyo tuliimbaa... Sijui huwa kuna muunganiko gani hapoo...afuu hivyo viyange yange sivioni tena!!!
Vipi zile ndege(plane) zilizokuwa zinaachia moshi mweupe angani zikipita unaimba ndege ya urusi hyooooo
Kunguru wa zanzibar wamewafukuza wote..! Hawa wadudu ni waharibifu sana..! Wildlife society of Tanzania walikuwa wanaweka mitego kwenye magorofa kule posta ili kuwapunguza, European union walipogoma kufund hiyo project nao wakazidi kuongezeka..!
 
Mie niliambulia vyote. Ila nilikuwa sijali.. Nikipata wasaa wa kucheza na wenzangu nilikuwa nasahau yote..!
 
Kunguru wa zanzibar wamewafukuza wote..! Hawa wadudu ni waharibifu sana..! Wildlife society of Tanzania walikuwa wanaweka mitego kwenye magorofa kule posta ili kuwapunguza, European union walipogoma kufund hiyo project nao wakazidi kuongezeka..!
Kumbe walikuwa wanapendeza Sana angani!!
 
Its complicated sijui nianzie wapi. Mnaozinga mko wawili, mnaowawinda wanakuwa wanazunguka kwenye umbo mstatili.
yeah naukumbuka sana huo mchezo Iringa tulikuwa tunaita Uki, unachora mstatili wenye njia na viduara vinne kila kona kwa ajili ya kusimama unatakiwa ukimbie mpira unaporushwa usimame kwenye duara kabla mzingaji wa pili hajadaka mpira nafkiri.

kweli nyimbo za utoto zinakumbusha mbali aisee.

Nakumbuka pia:
-Asiyejua kusoma ni mjinga kabisa
barua ikija aitembeza kutwa.

-kuku na bata walifanya harusi chumbani

- simama ka, simama ka, rukarukaruka simama ka.

- banchikicha, banchikicha, banchikachikichachikicha, nilikwenda,
nilikwenda, nilikwenda kwenda kwenda kwenda
kwa mzungu, kwa mzungu, kwa mzungu zungu zungu,
nikalala, nikalala, nikalalalala,
siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatutatutatu,
nikasikia ngongongo, ngongongo, ngongongo.
wewe nani, mimi juma, wataka nini, nataka mke, mkegani, mke wangu
kalulu pamba pambapamba.

- kofia nyekundu tarabushi inanipendeza mama, wao wao kweli,..........

- hadithi inayokuja ni ya sungura sikia........
alitoka siku moja njaa aliposikia...........

- kidalipo,
- saresare maua, asiyejua kuchagua, kabila lake mzigua.
- alisema asliema, alisema Nyerere alisema, vijana wangu wote mmelega saizi tuanze mchakamcha. mchakamcha chinja.....
-kula wali mbakishie baba (hapo mmetengeneza mchanga mlima katikakati mmeweka jiti, ole wake atakaye angusha lile jiti)
- saliapoo...
-Wakati umewadia wa salamu za wagonjwa leo tunawapa pole(huu ulikuwa unapigwa radio tanzania kila jumapili asubuhi kipindi cha salamu kwa wagonjwa) kipindi chenu chawapeni pole, pole tunawapa pole. kha niliupendaje.

- mbali ya mama na mwana ile instrument ya kipindi kisha unasikia mama na mwana nilikua sibanduki redioni kila jumamosi saa nane inapofika hadithi za adili na nduguze, unyoya wa kipanga azizi, binti chura, ua jekundu, , pete ya ajabu (mfalme wa baharini na ughaibuni) waridi, vijitabu vya hadithi vya bulcheka na mke wake, pinokyo, sungura na fisi, juma na rosa, mpigafilimbi wa mahelini, hana hela, maua ya malani, bahari nyeusi, akili kufundishwa, loh kweli hazitarudi tuliozipitia tuwasimulie wanetu ni urithi na tunu ya zamani. kweli nimekumbuka mbali sana.

- michezo ya kiboleni, ukuti ukuti, kuruka kamba, mdako, kombolea, tujipikilishe, .....
 
Uliingo bayoyo ulingo bayoyo
Dada kasie ingia kati tukuone
Maringo yako abingilibingili
Mpaka chini!
Wakati mnaimba wimbo huu mnakuwa mmekaa duara kwa hiyo anayetajwa jina anaingia kati mikono kiunoni anaanza kukata kiuno huku akirudi chini.
 
Saka mke wangu sqka mke wangu....,
Hapa hayupo hapa hayupo....,
Ameenda wapi ×2,
Ameenda kusuka ×2......
 
Baba Mdogo alipo ondoka kasema tuchole kitu kinacho itwa............

Kwenye kusahisha sas kama mwenye zamu sio mpambe wako unakula X kubwaaa
 
goodu bai goodu bai mai frend mai om is fara awe, wi ango tu sii ai shall go tu omsii mai frend guud bai guud bai mai frend.

Mwingine sijui kama umekuwa posted. zum zum zum nyukilia we, hewa nzuri kwa chakula, zum zum zum nyukilia we.
 
Kimbuka
 
kuna katoto nilikua nacheza Nako kwa kukarusha juu Na kukadaka. Nakarusha tena Na kukadaka. Nilipo acha kakaniambia "acha us*nge nirushe tena" nikabaki hoi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huu sio ule wa mgeni siku ya kwanza mpe mchele na panzi mtiliie kifuuni mkaribishe mgeni?
Mgeni siku ya pili mpe maziwa na samli mahaba yakizidi mkaribishe mgeni,
Mgeni siku ya tatu muonyeshe (nimesahau)
mgeni siku ya nne mpe jembe akalime akikataa muagane aende zake mgeni
mgeni siku ya tano si mgeni ana baa hata ------- katia yeye mgeni
mgeni siku ya sita---

mgeni siku ya kenda enenda e bwana nendaa akitaka tuagane aende zake mgeni
Mgeni siku ya kumi kwa mateke na magumi hapana afukuzwaye, afukuzwa yeye mgeni.
 
Mie ntaimba!
Mkikutana wenye akili moja wala hamna cha aibu wala ukubwa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…