Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Hahahahaaa sheki rede mpira ukienda mbali unazunguka kwenye vyumba na kuhesabu. Pia kulikuwa na rede ya chupa. Aahahahahahahhahahahaaaa
Na ila mstari kati sijui
 
Huu sio ule wa mgeni siku ya kwanza mpe mchele na panzi mtiliie kifuuni mkaribishe mgeni?
Mgeni siku ya pili mpe maziwa na samli mahaba yakizidi mkaribishe mgeni,
Mgeni siku ya tatu muonyeshe (nimesahau)
mgeni siku ya nne mpe jembe akalime akikataa muagane aende zake mgeni
mgeni siku ya tano si mgeni ana baa hata ------- katia yeye mgeni
mgeni siku ya sita---

mgeni siku ya kenda enenda e bwana nendaa akitaka tuagane aende zake mgeni
Mgeni siku ya kumi kwa mateke na magumi hapana afukuzwaye, afukuzwa yeye mgeni.

Hapana huu wako wa mchele na panza,
Siku ya tatu nyumbani hamna kitu , ni kutoka katika kitabu cha Bulicheka.
 
Nimesoma karibu page zote sijaona wimbo wa

"mabata makubwa makubwa yanaogelea, yanaogelea katika mto

Yanapokuwa yanaoga kwa kwa kwa kwa kwa,
Kwa kwa kwa kwa kwa,

Kwa kwa kwa kwa kwa"
 
Waliocheza Chidea gonga like hapa. "Fidodiido mama fidodido hana ugoko" "Chidea chide chide i love you nakupenda"

"Kideede zunguluka ukitaka inama inuka"

"Ooh mista kalumbe kalumbe kakumbe ooh"
 
Namtafuta mke wangu X2
Hapa hayupo X2
Kaenda wapi X2
Kaenda kusuka X2
Chanuo kampa nani X2
Kampa msusi X2
Pesa kampa naniX2
Kampa msusi X2

Nina ndoo yangu
Eeeeh
Yakuteka maji
Eeeeh
Maji ya dhahabu
Eeeeh
Watoto msitizame nyuma X2
Yai bovu linapita X2
Hivi mtunzi na mwandishi wa huo wimbo ni nani maana ulikiki sana mtaani kwetu. Huyi aliyetunga atakuwa ni star
 
Nimesoma karibu page zote sijaona wimbo wa

"mabata makubwa makubwa yanaogelea, yanaogelea katika mto

Yanapokuwa yanaoga kwa kwa kwa kwa kwa,
Kwa kwa kwa kwa kwa,

Kwa kwa kwa kwa kwa"
Mabata madogodogo
Yanaogeleaa yanaogelea
Katika shamba zuri na bustanii (isn't it?)
Yanapenda kutembea bila viatu bila viatu
Katika shamba zuri na bustanii
Yanapenda kulia kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwakwaa
 
Kipepeo anaruka anaruka anaruka
Anatafuta chakula chakula chakula
Chakula chake maua maua maua
 
kuna katoto nilikua nacheza Nako kwa kukarusha juu Na kukadaka. Nakarusha tena Na kukadaka. Nilipo acha kakaniambia "acha us*nge nirushe tena" nikabaki hoi
Hahahahaaaaaa huyo dogo hatari[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nzu nzu nzu eeh mama nyuki lia weee
Nzu nzu nzu we mama nyuki lia weee
Toka mbali kutafuta UA zuri kwa chakula nzu nzu nzu we mama nyukil lia wee..!
aisee! enzi za viduduu hizoo, hapo muda wa uji umefika ndo mwalimu anaanda vikombee [emoji28][emoji23][emoji28]
 
Ila tungeipata kwa audio hata vioce note ingependeza zaid maana kupata saut Yale ni majanga
 
Banchikicha,banchikicha nchikicha nchikicha
Nalikwenda,kwa mzungu
Nikalala siku Tatu,
Ya nne!,nikasikia ngongongo
Wewe nani?mimi juma, wataka nini?nataka mke,mke nani?mke wangu,......
 
Back
Top Bottom