Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Tatu katatuka
Kapanda juu kaanguka
Kichupi chake kinanuka
.......................................

Cc womanity
Haahah huo wimbo sku ile nilikuwa nauwazaaa..haujiii

Kinanukia sambusa
Musa naye Kanusa.....
Huuu wimbo nilikuwa nautafakari nikienda kusuka kwa wamama enzi zile Kilimanjaro style utaingizwa kwenye ile miguu katkat Ndyo ulikuwa muda wangu wa kunusa!!!!

Umekumbuka nini lol
 
Haahah huo wimbo sku ile nilikuwa nauwazaaa..haujiii

Kinanukia sambusa
Musa naye Kanusa.....
Huuu wimbo nilikuwa nautafakari nikienda kusuka kwa wamama enzi zile Kilimanjaro style utaingizwa kwenye ile miguu katkat Ndyo ulikuwa muda wangu wa kunusa!!!!

Umekumbuka nini lol
Duh wewe ulikuwa hatari...kumbe kusukwa katikati ya miguu mlikuwa mnapata kadhia hivyo!
 
Kumbe na mimi ni mkongweeeee aisee

Me huu wimbo niliupenda

" Aidaaama yoyoyoooo
Aidaaaama ,aidamaaaa yoyoyo eeeh aidamaaaa
Wawili wakipendanaaaaaaa,aidamaaaaaaa,shetani hana nafasiiiiiiiii "

Dah baada ya miaka 23 nikaenda JKT 835 KJ KABUKU na katika chenja kamanda akaaanzisha wimbo huo ambapo wakati naimba mwili wote ukawa unasisimka.Huu wimbo kwa kiasi kikubwa sana ulinisaidia nisitoroke mafunzo maana ulikuwa unaamsha morali yangu huku nikiwakumbuka watoto wenzangu niliocheza nao karakata miaka hiyo.Niliwakumbuka sana kina sofia,watoto wa siwa tajiri ambao tulikuwa tunajimix nao,nilimkumbuka mchumba wangu wa utotoni ZAWADI,Rafiki yangu Rama,rafiki yangu Philipo,Mudy kidinyo,kaka yake mudy anaitwa hamisi(Huyu nikaja kukutana nae Azania sec).

Ni miaka mingi sana hapo nikiwa nasoma shule ya vidudu Otagaya Nursery school na watu kama kina Irene,Husna,rama.Ngoja niishie hapa kwanza kwa leo!
 
Kuna hii sijui tuiteje....
Nilonge nisilongeeee
Longaaaa
Mwenzenu womanity eeenheeeeee
Mchumba ake enheeeeeeeeee
Bujibuji watu eeeeeheeeeeeeeee
Ni wimbo naooo..
Kwenye kutajana hapo ndyo ilikuwa kasheshe..wakishataja unasubiri ndugu zakokwenda kukusemelea home au kusingiziwa mmefanya mchezo Mzuriii!!(huko kwenu huo mchezo mzuri ulikuwa haupo teh)
 
Dada veronikaaaa
Usilie lie
Utapata mchumbaaa
Toka umasaini
Ya kwanza baruaaaa
Yapili majibu
Ya tatu stareheeee
Ya nne harusi
Alibo libooo sukuma
(Tumpampu )x2
Alibo libooo sukuma
(Tumpampu)x2
 
Ukiona ndege imetua mrema kaingia leo x2
Kiatu ni cha bei aha
Nguo ni ya bei aha
Tena na tena cha mkoloni kinanipa shua x2
 
msingi bomoa mnakubaliana mnafungishana vidole shahid anakuja anafanya kama kutenganisha hapo huruhusiwi kuinama unapigwa teke nais ingeendelea mambo ya ushoga yangepungua
 
Kulaaaa
Mbakishie babaaaa
Kulaaa mbakishie babaaaa
Na atakayeangusha kijiti wakati wa kula anaambulia kupigwa makofi mwili mzima mpaka aende kugusa au kushika kitu mlichokubaliana ndio mnamwachia
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
mwanangu kua kua nikutume
nikutume wapi kwa mfalme
kuna ng'ombe zetu 12
mmoja kafa kaliwa nyani
nyani mkinda tumkindule
tusole visiga vya bwana chuma
bwana chuma gani simdodo
simkindu dawa kanabuba..

nadhani na kizaramo ndani humo wala tulikuwa hatujui maneno mengine maana ake nini😀
Daaaaaaahhh kitambo sana kweli
 
Kama Dada wanipenda,kaninulie zeze,nikilala kitandani,zeze lanibembeleza,ahah amina,kusemasema kubaya,utamsema mmeo, aliyekupa hiyo mali
Huo mstari wa juu ni kutoka kwenye wimbo wa T.I.D unaitwa zeze, huo mstari wa pili kama sikosei ni wimbo ulioimbwa na Ali Choki wa twanga pepeta.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli me mhenga daaaahhhh
Cc. Finyango
 
Nzu nzu nzu eeh mama nyuki lia weee
Nzu nzu nzu we mama nyuki lia weee
Toka mbali kutafuta UA zuri kwa chakula nzu nzu nzu we mama nyukil lia wee..!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
daaaahhh nakumbuka sana kuuimba huo wimbo ila melody yake tayar ishanitoka
 
->Mwanangu kuwa kuwa nikutume unitume wapi kwa mfalme.....


->Namtafuta mke wangu, hapo hayupo hapa...kaenda wapi kaenda wapi, kaenda kwa msusi

->Kunguru kasema, kila mtu kwao kwao kwao kwaaaaa

->Kula mbakishie baba, kula mbakishie baba
 
Ule wimbo wa kikojozi unaimbwajwe???

Kikojozi huyoooo
Kikojozi
Na nguo.....
Kikojozi huyo,
kikojozi huyooo,
na nguo kaitia moto,
na ndani kuna viroboto ... [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kindumbwe ndumbwee chaaalyaaa
Kindumbwe ndumbwee chaaalyaaa
Kikooojoooziii kajikojoleea na nguo kaitia motoo hiloooo.

Hahahahahhahahahahaaa looh
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hapo umechanganya nyimbo mbili tofauti
 
Hivi ule utamaduni wa mangongoti(mtaalam anayevaa kama dude la kutisha huku akitembea juu ya miti miwili kumfanya aonekanae mrefu kama giant) imepotelea wapi these days?, i relly miss it
 
Back
Top Bottom