Kumbe na mimi ni mkongweeeee aisee
Me huu wimbo niliupenda
" Aidaaama yoyoyoooo
Aidaaaama ,aidamaaaa yoyoyo eeeh aidamaaaa
Wawili wakipendanaaaaaaa,aidamaaaaaaa,shetani hana nafasiiiiiiiii "
Dah baada ya miaka 23 nikaenda JKT 835 KJ KABUKU na katika chenja kamanda akaaanzisha wimbo huo ambapo wakati naimba mwili wote ukawa unasisimka.Huu wimbo kwa kiasi kikubwa sana ulinisaidia nisitoroke mafunzo maana ulikuwa unaamsha morali yangu huku nikiwakumbuka watoto wenzangu niliocheza nao karakata miaka hiyo.Niliwakumbuka sana kina sofia,watoto wa siwa tajiri ambao tulikuwa tunajimix nao,nilimkumbuka mchumba wangu wa utotoni ZAWADI,Rafiki yangu Rama,rafiki yangu Philipo,Mudy kidinyo,kaka yake mudy anaitwa hamisi(Huyu nikaja kukutana nae Azania sec).
Ni miaka mingi sana hapo nikiwa nasoma shule ya vidudu Otagaya Nursery school na watu kama kina Irene,Husna,rama.Ngoja niishie hapa kwanza kwa leo!