Wewe ndio hujui hata kusoma, acha kuwatusi wenzio. Hapo kuna au za aina mbili, kuna nyekundu na ya bluu. Hiyo nekundu inatenganisha adhabu mbili ambazo ni "atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu" au/na "kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi". Kwa tafsiri hii mchezaji anaweza kupewa adhabu mojawapo ama zote mbili, kutegemea maamuzi ya kamati husika itakayotoa adhabu hiyo (hizo). Lakini "au" ya bluu inatenganisha zile adhabu mbili za mwanzo na hii ya mwisho ambayo ndiyo ya kufungiwa kucheza soka kwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja au miaka miwili.
Kwa tafsiri sahihi ya sheria/kanuni hii, Juma Nyoso alitakiwa aidha alipe faini ya milioni mbili (ama kiwango chochote ambacho wangeamua, ndani ya sheria) AU afungiwe michezo mitatu hadi kumi (wangeamua wenyewe), AU angelipa faini hiyo PAMOJA na kufungiwa michezo mitatu hadi kumi. Endapo wangeona anapaswa kufungiwa kucheza kwa kipindi cha mwaka mmoja au miwili, ina maana adhabu ya faini isingekuwepo tena maana hazihusiani hata kidogo.
Kama utashindwa kuelewa kwa ufafanuzi huu, basi kaa tu pembeni uache kutukana watu.
Kuhusu kosa la Nyoso, hakuna anayekataa kuwa siyo kosa. Hata hivyo katika sheria, ukitoa maamuzi kwa kutumia sheria ambayo si sahihi maamuzi yako yanabatilishwa. Mfano wa kwanza ni hiyo tafsiri niliyotoa hapo juu. Kosa la pili ni hilo la kamati ya adhabu kuwa chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa timu inayolalamika, uliona wapi suala hili likawa sahihi kisheria? Tatu, ni malalamiko ya Mbeya City kuhusiana na vitendo vilivyofanywa na wachezaji wa Azam mbele ya mwamuzi, ambavyo vimefumbiwa macho (hili watajua namna ya kulalamika wenyewe)
Kwa kifupi, kosa lilitendeka na adhabu inastahili kutolewa. Hata hivyo adhabu stahiki ndiyo inastahili kutolewa tena kwa kufuata principles sahihi za utoaji adhabu, na hakuna excuse ya kufumbia macho offenders wengine hata kama wanatoka kwenye timu ambayo ndiyo inaonekana kama wanaifadhili TFF