NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

Binafsi sikuumizwa na alichofanya Slaa, bali NILISIKITISHWA. ni mtu aliyejitoa kutumiwa na "maadui" zake ili "kummaliza" yule waliyetofautiana naye. Hapo tu ndio namwona SLAA HANA MAANA. Slaa alituthibitishia kwamba yeye ni mtu mwenye hekima na busara, anafanya mambo baada ya kufikiri sana. na ANA MSIMAMO. lakini baada ya kutofautiana tu na chama chake, akasusa kila kitu na kuacha misimamo yake yote ya mwanzo. sasa mtu wa aina hiyo anaweza kuja na jipya lipi, zaidi ya kuuthibitisha tu huo UNAFIKI wake?

Narudia tena, Kama Slaa angeendelea na misimamo yake ya kupigani HAKI, na kubaki nje ya mfumo na kuachana na vyama. hapo ningemuelewa. au hata kama angebaki kimya tu, pia ningemuelewa kwamba hapa kuna GREAT MAN ametofautiana na wenzake, ameamua kuachana nao na kukaa kando. lakini kujaribu kuwamaliza? huo kwanza ni ubinafsi na ni kuwasaliti watanzania mamilioni ambao wana imani na siasa za upinzani, hata kama hawakubaliani na CHADEMA. lakini wana imani na upinzani kwa ujumla.
 
NAJARIBU TU KUTAFAKARI "YULEYULE ALIYEYAPINGA YALEYALE NA KUMTUKUMU MTU YULEYULE LEO HII KALALA KITANDA KILEKILE CHA WATU WALEWALE HUKU AKITAFUNA KIPANDE CHAKE CHA MKATE PASIPO KELELE WALA MAKEMEO!!!"
UNAFIKI MTUPU!!!
 

Umefafanua vizuri sana; watu hawataki kukubali kuwa wao ndio waliogeuka na hadi hivi sasa hawataki kukubali kuwa walifanya makosa.
 
Ni kweli hayuko ccm, lakini unapokuwa balozi kwa uteuzi wa mwenyekiti wa ccm, hasa mwenyekiti mwenyewe akiwa ni Magufuli, automatically ww ni mwanaccm.

Duh.. hii ni reasoning ya ajabu sana. Huwi mwana CCM kwa vile umekubali kuwa Balozi. Huku ni kutokuelewa mgawanyo wa utendaji serikalini. Hivi kila mtu anayefanya kazi serikalini ni mwana CCM kwa vile tu amekubali kufanya kazi serikalini? au hii ina apply kwa vile tu mtu kateuliwa na Rais? Tutengeneza hoja vizuri. Ili mtu awe mwana CCM kuna masharti yake. Unachotakiwa ni kunionesha kuwa Dkt. Slaa katimiza masharti hayo. Kwa mfano, siyo kila mtu anayepinga CCM ni mpinzani au mwanachama wa CHADEMA. Na siyo kila anayeunga mkono CHADEMA ni "mwanachadema". Katiba zote za vyama vya siasa zina ibara inayoitwa "Masharti ya Uanachama". Pitia hii itakufunulia kidogo kama kweli Dkt. Slaa ni Mwana CCM kwa vile tu ameteuliwa na kushika Ubalozi.
 
Kama ''abstract'' ni hiyo ya MM, nachelea kusema kitabu kitaongelea migogoro zaidi kuliko demokrasia aliyosimamia kwa nguvu. Tuna migogoro ya kutosha! Nahitaji kusoma kitu tofauti.

Kwa kweli uamuzi wa kusoma kitabu hiki ni wa mtu mwenyewe na wala hauitaji ushawishi. Kitabu hiki ni cha maisha ya kisiasa ya Dkt. Slaa; kinaanzia toka kuzaliwa kwake na safari yake ya kitaaluma hadi alipofikia. Kwa ufupi ni kuwa kitabu hiki kiliandikwa kabla ya Dkt. Slaa kuteuliwa kuwa Balozi. Hivyo, hakihusiani na hakideal kwa kiasi kikubwa na yaliyotokea baada ya kuteuliwa Ubalozi.
 
Lowasa ilitumika kama sababu tu, ili aitumie kukisaliti chama,

aliyemteua yeye kuwa balozi ndio huyo huyo aliyemrusisha lowasa ccm, tena kwa kumlazimisha arudi na si kwa hiari yake.

Maana ingekuwa ni mfumo mwingine uliomteua at least hoja yake ingeleta sense,

Lakini pia kubadilika kwa mitazamo yake kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini ni ushahidi mwingine.
 

Mzee tofautisha kufanya kazi serikalini na kuteuliwa na mwenyekiti wa ccm kwa nafasi ya uwakilishi. Nasisitiza tena, unapochaguliwa na Magufuli kwa nafasi ya uwakilishi ww automatically ni mwanaccm, na ndio maana unasikia Slaa anasema yote waliyopiga kelele wapinzani yametekelezwa, huku katiba mpya haijapatikana na demokrasia inayumba vibaya. Nipe tofauti alichoongea Slaa na wanachoongea Makada wa ccm.
 
Kwa kweli kwa hili siwezi kukusaidia. Inawezekana ama huelewi mfumo wa utendaji kazi na utumishi serikalini au unataka kuendeleza ligi isiyokuwepo. Dkt. Slaa hakuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kufanya shughuli za CCM. Lakini pia inawezekana huelewi mgawanyo wa shughuli za chama na shughuli za serikali. Balozi wa nchi yetu haitwi "Balozi wa CCM Italia!"
 

Huenda unadhani unaongea na mtu asiyejua lolote hivyo unadhani ninayokuambia nakuambia kwa bahati mbaya, au nina uelewa mdogo wa mambo ya serikali na mipaka ya ccm ndani ya serikali. Kwa taarifa yako Magufuli hajui tofauti kati ya serikali na ccm, na hata kama anajua haheshimu hizo tofauti, hasa kwa watu anaowapa vyeo vya fadhila kama hao mabalozi. Ndio maana nakuambia ukitaka kujua ukichaguliwa na Magufuli unakuwa mwanaccm automatically bila kadi, sikiliza anachoongea sasa hivi baada ya kupewa ubalozi.
 
Siyo lazima kununua kitabu hicho kwani maisha yataenda tu bila ya kijitabu hicho!
Pia kukimbia kwake "choo" sebuleni" na leo analala pamoja na kinyesi chenyewe kunaondoa hadhi na umaarufu walau kidogo alioupata. Na kuwa kumsikiliza Delila wake na kumbu kumbu ya ulaji mihogo vitamtesa sana kwani wenye KUTAFAKARI,KUKUMBUKA NA KUCHAMBUA mambo na watukio watahitimisha kuwa Slaa ni binadamu kama wengine na usaliti ni sehemu ya maisha.Yeye si wa kwanza na hatakuwa wa mwisho. "GODS BITS OF WOOD" -O.SEMBENE na kina SOUNKARE wataendelea kujidhihirisha.
 


Hadithiii ndeefuuu.. Ujinga mtupu!

Nyie ni matapeli wa kisiasa tu kama walivyo matapeli wengine!
 
Kinyesi kimemfuata chumbani sebuleni backyard?
Mama junior hujambo habari za sweeden, sisi huku bado tunasubiri ahadi ya shule yetu uliyotuahidi kabla ya kukimbilia ughaibuni.

Huku kwetu Ibwera umasikini umezidi maisha ni magumu kuliko wakati wa JK, tunashindia mihogo ukipata tutumie angalau kidogo.

Mpao obashule bona okwo omumahanga
 
Ujinga tu. watu wenye akili tupo tunawekeza kwenye viwanda na biashara kubwa, we upo busy unawekeza kwenye majungu tu.

We mzee bado una mentality za kimasikini
 
Katika kitabu cha NYUMA YA PAZIA Dkt. Slaa anaelezea kwa kina matukio mbalimbali ambayo yalitokea hadi kufikia Lowassa kukaribishwa CHADEMA na kwa nini hakuwa tayari kusimama jukwaani kumnadi Lowassa na akabakia na utimamu wa kimaadili na akili.
Huyu bwana ni muongo sasa Lowasa amesharudi na yuko CCM tayari unafikiri zile siri kama zipo za alichokifanya lowasa atakizungumzia tena humo, sijui kama watakutana uso kwa uso
 
All in all tutai- miss sana CDM ya Dr. Slaa, jiwe mjanja sana aliona atumie kila namna kumtoa Dr. kutoka CDM,
 
Laana ya tamaa; kweli wazee achaneni kuoa uzeeni. Bado anaamini kua Lowasa ndo kilimuondoa CDM? Mwezie Lipumba alisharudi na yeye pia atarudi. Yaani Dr Slaa anadhani kua kilichokua kinatendeka alikijua yeye na Fina pekee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…