Mhubiri 9:10 Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Kusali au kumbukumbu kwa ajili ya wafu sio wazo la kibiblia. Maombi yetu hayana mwelekeo kwa mtu anapokufa. Ukweli ni kwamba, wakati wa kifo, hatima ya milele ya mtu imethibitishwa. Aidha anaokolewa kwa njia ya imani katika Kristo na yuko mbinguni ambako anapata mapumziko na furaha katika uwepo wa Mungu, au yuko katika maumivu katika Jahannamu. Hadithi ya mtu tajiri na Lazaro mwombaji hutupa mfano mzuri wa ukweli huu. Yesu alitumia hadithi hii kwa uwazi kuwafundisha kwamba baada ya kifo watu wasio na haki wanatenganishwa milele na Mungu, kwamba wanakumbuka wakikataa injili, wakiwa katika maumivu, na kwamba hali yao haiwezi kurekebishwa (Luka 16: 19-31).
Mara nyingi, watu ambao wamepoteza mpendwa wanahimizwa kuombea wale waliofariki na familia zao. Kwa kweli, tunapaswa kuombea wale wanaoomboleza, lakini kwa wafu, hapana. Hakuna mtu anayepaswa kuamini kwamba mtu anaweza kuomba kwa ajili yake, na hivyo atasababisha aina fulani ya matokeo mazuri, baada ya kufa. Biblia inafundisha kwamba hali ya milele ya wanadamu imedhamiriwa na matendo yetu wakati wa maisha yetu duniani. “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa…., haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake"(Ezekieli 18:20).
Mwandishi kwa Waebrania anatuambia, "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu" (Waebrania 9:27). Hapa tunaelewa kwamba hakuna mabadiliko katika hali ya kiroho ya mtu inaweza kufanywa baada ya kifo chake-ama yeye mwenyewe au kupitia juhudi za wengine. Ikiwa ni bure kuomba kwa ajili ya wanaoishi, ambao wanafanya "dhambi inayosababisha kifo" (1 Yohana 5:16), yaani, dhambi ya daima bila kutafuta msamaha wa Mungu, sala ya wale waliokufa itawafaidi aje, kwa kuwa hakuna mpango mwingine wa wokovu baada ya kifo?