NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

Japo Dr.Slaa alizingua lakini bado anabaki kuwa mwanasiasa makini kwa Tanzania..Binafsi nitakwenda nunua hiki kitabu...MENGINE NAJUA ILIKUWA MIPANGO YA KATOLIKI Kuweka pandikizi lao,CHADEMA walichemka sana kumpa nafasi Lowassa yakupeperusha bendera 2015 dhidi ya MKATOLIKI Magufuli.Hapo ilitakiwa asimame Dr.Slaa na hakika Leo kusingekuwa na Ccm....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kiongozi Tz aliyenivutia kushabikia siasa za upinzani kama dr W. Slaa.
Lakini tangu 'walivyomnywa' mafisadi kihuni, sina hamu tena Cdm.

Sasa huku ninakoishi mkoani Kgm ntakipataje, japo umetoa namba za simu?
Wasifu uliompatia kwenye thread hii unamstahili.
Wasiomuelewa vizuri dr.Slaa hawatakuelewa
 
Ujïnga mtupu. Amerudi Lowassa amkimbie tena. Hoja yako ya matangazo ni dhaifu haifikirishi.
 
Bila Shaka na prof lipumba naye yupo chimbo kutuletea hadithi Kama hii hasa 2015 kilichotokea niwaambie tu hiki kimetoka kimkakati zaidiii hasa ukizingatia uchaguzi upo jirani LENGO NI KUTUGAWA TU WATANZANIA
 
Usikubali kufungwa mawazo wako na hisia. Ukisoma vitu vinavyokufurahisha kihisia tu utajikuta kuwa mawazo yako yanatawaliwa na hisia. Hatusomi au kujifunza kwa watu tunaokubaliana nao tu bali hata tusiokubaliana nao au wale ambao hatuwajui kabisa kiasi cha kuweza kuchagua upande. Kuna watu humu nawasoma inaonekana na wao waliumia sana kwa Dkt. Slaa kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo hisia zao na labda akili zimeumizwa mno kiasi kwamba ukitaka "Dkt. Slaa" wanakuwa kama Manchurian Candidate. Mtu aliyekomaa kihisia, kiakili na kisiasa haogopi au hajidhanii kuwa hafai kujisomea mambo kutoka kwa mtu asiyekubaliana naye. NI suala la ukomavu tu.

Kwa wale ambao wanapanga kusoma au tayari wamesoma nina uhakika watamaliza wakiwa na ufahamu mkubwa sana kuhusu maisha na siasa za Dkt. Slaa na kwa kiasi kikubwa wataweka mitazamo yao katika mitazamo sahihi na labda hata kubadilisha mawazo yao au kuyathibitisha waliyokuwa nayo awali
 
Haya uliyoyasema ndio ukweli Wenyewe, sijui shetani gani alimpitia huyu Dr Slaa, alipambana miaka mingi kuleta mabadiliko yenye tija ktk nchi hii lakini alishindwa maamuzi ya muda mfupi tu 2015 na kupotexa mwelekeo mazima.
Mweh..Sasa kitabu kinajaribu kujibu swali hili kwa kina.
 
Ngoja nipitie copy yangu hapo
 
Mzee Mwanakijiji Gulwa na Laface77 wanadai Dr. Slaa ni mzinzi toka akiwa Padri na baada ya kuacha Upadri, ni kweli? Na je kwenye hicho kitabu chake kaelezea ilikuwaje aliacha Upadri. Jee Suala la Uzinzi ni sababu mojawapo ya kuacha Upadri?
Mweh Sasa sasa usome kitabu...na hata hapo juu hujasoma nilichosema? Ni uvivu wa aina gani huu??!!
 
Huko nyuma tulikuwa pamoja na Padre Slaa vizuri tu. Lakini alipoingia Lowasa CHADEMA, sikumwelewa kabisa Slaa. Ningeelewa kama angekaa pembeni na kuachana na siasa, akatulia. Lakini kuiunga mkono serikali ya CCM? hapo sitakaa nimuelewe kabisa - eti hana chama!! thubutu yake!! anaganga njaa tu kama wengine. Slaa amekuwa mwepesi sana.
 
Dkt. Slaa alihamia lini na Wapi CCM? Nina uhakika wa asilimia mia moja hutarudi na jibu la tarehe wala mahali.
 
i will buy and read this book as intellectual ila credibility ya Dr Slaa kwangu ishaondoka kabisa. Ila najua ni mtu mwenye fikra na historia kwa hilo kitabu chake ni muhimu kwa sie tunaopenda kujifunza.
 

Ila ni kweli kuwa, kama anaendelea kumtaja Edward Lowassa katika kitabu chake kama sababu ya yeye kuachana na "siasa za vyama" katika mtazamo uleule aliokuwa nao mwaka 2015 alipohama na kurudi nyuma.....

Basi, hakika mantiki na maudhui yote ya kitabu hicho yanakuwa "invalid" na yanakosa maana yoyote kwa sababu, tayari tena MTU huyohuyo (his nightmare) "wanalala naye kitanda kimoja hukohuko CCM!!"

Sijui atawaambia nini watu ktk hili....

Anyway, kwangu mimi kwa kulielewa hili i.e Edward Lowassa vs yeye Dr Slaa, siwezi kununua kitabu hicho unless nipewe bure labda naweza kujitahidi kukisoma hivyohivyo....
 
Watu wengi wenye hekima na busara huwa wanaacha kazi ya fasihi andishi, hasa kupitia utunzi wa vitabu ili kutambulisha yale wanayoyaamini na kutambulisha misimamo yao ktk maisha waliyoyapitia. Ndivyo ambavyo Dr. Slaa amefanya.

Naam! Tunaweza kutofautiana naye kimawazo ama kumuhukumu kwa aina ya maamuzi aliyowahi kuyafanya sehemu fulani ya maisha yake, na pengine hatukuyapenda ikijumuisha; kuacha ukasisi, kutengana na mwandani wake wa awali, kuoa mke mwingine, kutengana na mambo ya kisiasa, kukubali "offer" ya ubalozi ambayo anaihudumu mpaka sasa.

Yote hayo ni mapito ktk maisha yake, na kuendana na umri alioufikia, ndipo hasa ni wakati stahiki wa kuja na "Bibliography" yake. Na sehemu ya nukuu ktk uzi huu ni kwamba; "Umpende, usimpende,....." Yeye ameshafanya jambo muhimu sana ktk fasihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…