NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

Wewe na huyo slaa wote vigeugeu, sisi vijana tumewapuuza
Sifa ya ukigeugeu inawahusu hata wakina Lisu na wenzao waliotuaminisha kwamba Lowasa ni fisadi halafu baadaye wanageuza maneni na kutufanya sisi kama mazombie. Eti ufisadi ni mfumo.
 
Amen!!!
 
Sasa...unaonekana hutaki kujua na naombea mtu asikupe kitabu Cha bure.. Sasa mtu una maswali mengi na umepewa mahali pa kupatia majibu...hutaki! Oh "mpaka nibembelezwe na kupigiwa ngoma". Sasa si Bora uendelee na kukaa hivyohivyo?

Yes, ofcoz....sitaki na labda sina hamu kabisa kujua lolote kuhusu Dr Slaa....!!

Kabla ya tukio la kushtukiza la yeye kukimbia vita mwaka 2015 tena ktk dakika za majeruhi, huyu Mzee alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliokuwa role model wangu....

Lakini baada ya tukio lile la kukimbia vita tena kwa mtindo wa kuwaonesha maadui aliojiunga nao mbinu na mikakati ya kivita ya iliyokuwa kambi ya wapiganaji wenzake aliowakimbia (aliowasaliti), nilijifunza kitu kimoja, kuwa, kumbe hata baba mzazi aweza kugeuka na kuanza kula nyama ya watoto wake mwenyewe wa kuzaa.....!!

From there, alitoka kabisa moyoni na nafsini mwangu. Kwa hiyo, ili labda nirejeshe moyo wa kujifunza kwake kwa, kusikiliza chochote asemacho/aandikapo sasa na kumwamini tena, kwanza akiri kuwa alikosea na asitumie kivuli cha Lowassa kufichia udhaifu na makosa yake....

All in all sina tatizo lolote na Dr Slaa kama binadamu mwenzangu. Tofauti yetu ni kutofautiana ktk mitizamo tu....

Na ishu ya kupewa kitabu chake bure je?

Yes, nimesema hivyo...... Lakini natambua hakuna atakayetoa kitabu bure kwangu kwa sababu, atakayefanya hivyo, kwa nini anunue kitabu kwa hela yake na kunipa Mimi bure huku nikiwa nimeshasema sitakisoma na badala yake labda nitakichoma moto?

Utajifunza nini kwa mtu ambaye yeye mwenyewe haaminiki tena?.....Ni ngumu sana unless, tuanze na matengenezo (restoration) kwanza...

Huo ni msimamo wangu
 
Utajifunza nini kwa mtu ambaye yeye mwenyewe haaminiki tena?.....Ni ngumu sana unless, tuanze na matengenezo (restoration) kwanza...

Huo ni msimamo wangu

Ungekapata nafasi ya kusoma kitabu chenyewe ungejua kuwa wanaohitaji kuomba radhi kwanza na kusimama na kuomba msamaha mbele ya wapinzani wote wa kweli ni wale waliobakia na Lowassa na wakazungusha mikono naye nchi nzima. Ni wale ambao waliamua kuchukua njia ya mkato kuingia madarakani na kufanya mazingaombwe ya kisiasa. NI wale ambao waliwaaminisha wananchi kwa miaka karibu kumi kuwa nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe halafu dakika ya mwisho wanatuambia "nyekundu!". Dkt. Slaa hakuwa mmojawao. Ukisoma kitabu hiki utawajua kwa majina na utajua ni kwa nini simba na mbuzi hawawezi kukaa zizi moja na nyanya na mbigili havipandwi pamoja...
 

Walifanyaje hao unaosema walikuwa na msimamo? Waliendelea kuunga mkono upinzani uliosalitiwa na kupigwa bei?
 
Pascal.. kama mtu kauoa na asimfanye mkewe kuwa kila kitu hiyo siyo ndoa tena. Unamnyoshea kidole Dkt. Slaa kwa vile kampa kipaumbele mkewe na watoto wake? Mwanamme usipompa nafasi ya kwanza mkeo.. unampa nani?
 
Biashara hiyo ilishachina zamani sana.

Mimi nashauri,kila mfanyakazi wa serikali anunue nakala moja kwa lazima,na kila siku itengwe japo dk 20 huko maofisini ili kuhakikisha kwamba,kimesomwa na wafanyakazi wote,hata wa ikulu pia wakisome na wakielewe.
 
Mwanakijiji Slaa anakula, tukiwa tunakula Africa hatuongei tukiongea ni kwa ruhusa ya baba au mama. Huyu (sijasoma na sitasoma kitabu hicho) ameandika kusifia Jiwe, most likely, ANAKULA, HARUHUSIWI "KUONGEA"

Nimedokeza hapo juu kuwa kitabu kinahusu nini hasa... sioni namna nyingine ya kufafanua.
 
Siasa za 2015 hasa ule usiku wa kumpokea Edward Lowasa na Dr. Slaa kuwekwa pembeni ndio ulikuwa mwanzo wa dhoruba Baharini......

Nahitaji hiyo nakala Mzee Mwanakijiji
Wahi nakala yako bosi; ni nakala chache tu zimechapwa kwa ajili ya kuweka rekodi katika usahihi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…