DiasporaUSA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 23,382
- 29,639
Kumbe hata baadhi ya maaskofu wa kanisa katoliki ni mafisadi.
Ngoja nitafute hicho kitabu ili kuelewa zaidi.
Ngoja nitafute hicho kitabu ili kuelewa zaidi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sifa ya ukigeugeu inawahusu hata wakina Lisu na wenzao waliotuaminisha kwamba Lowasa ni fisadi halafu baadaye wanageuza maneni na kutufanya sisi kama mazombie. Eti ufisadi ni mfumo.Wewe na huyo slaa wote vigeugeu, sisi vijana tumewapuuza
Na hakuna chama kisichopenda kuambiwa ukweli kama Chadema.asante kwa dibaji nzuri,nitachukua nakala yangu leo
Chadema hawawezi kununua hata uwape bure,kuna ukweli mchungu humo
Amen!!!Kuna mambo mengi mno KWENYE SIASA yanayohitaji utulivu wa kutosha kuyaelewa
Dk Slaa katika hatua za awali alikubaliana na wazo la LOWASA kujiunga na CHADEMA
Tulipomuuliza kwenye kamati kuu kwanini alikubali kujiunga kwa Lowasa kwenye chama, akatujibu kwamba Lowasa alisema atakuja na mtaji ambao kwa wakati ule Dk alisema hakuuona
Pili alisema alidhani Lowasa atakuwa mwanachama tu lakini hatakuwa mgombea urais
Tatu ,alisema Lowasa atoke hadhani kwa watanzania ajisafishe kwanza kuhusu tuhuma za ufusadi ambazo yeye(Dk slaa)ana ushahidi nazo.
Sisi tulimuita Lowasa mbele ya Dk slaa( katibu mkuu) wetu kipindi hicho na Lowasa akatolea ufafanuzi kila jambo kwa ufasa.
Katika hatua hiyo Dk Slaa akaridhika lakini baadaye hatukumuona bali tulichoona ni barua ya kumkaimisha Salum Mwalimu nafasi yake.
Maoni yangu ya ujumla ni kwamba Dk Slaa alikuwa sahihi kusimamia kile alichokiamini lakini alichoghafilika kidogo ni kuharibu kazi kubwa aliyoipigania kwa miongo miwili mizima yaani robo ya umri wake kwa kukwazwa tu kwa mara moja.
Lazima katika haya mapambano tupime baina ya masilahi mslapana ya jamii na taasisi tunazozisimamia ukilinganisha na masilahi yetu. Nadhani Dk amesimamia masilahi yake zaidi kuliko masilahi mapana ya jamii ya wapenda mageuzi makububwa ya mfumo wa kiutawala.
Kitabu cha Dk mambo mengi ameyasema kwa ukweli kufurahisha watu fulani wa makundi fulani na ndio maana nasema ni wakati wa watanzani kupima wanasisa vizuri bila kujali vyama vyao.
Dk Slaa hawezi kuwaona viongozi wa CHADEMA kama viongozi waliodalalia chama chao. Mwanzoni
kiongozi kama Mbowe,Tindu Lisu,Mnyika walikuwa hawkubaliani kabisa na swala la LOWASA kujiunga na CHADEMA lakini sisi wajumbe wa Kamati kuu ndio tuliowalazimisha baada ya kuona uwezo na nafasi ya Lowasa kukiletea chama ushindi
Hatukukjbsliana kirahisi ila tulipata nguvu ya kuwashawishi baada yakuona kwamba katika hatua za awali Dk Slaa aliunga wazo hilo mkono.
Kwahiyo Dk kushutumu vio gozi wenzake ni kujitetea kusiko na mashiko yoyote.
Lakini mwisho wa siku yote ni historia CHADEMA ipo na itaendelea kuwepo bila kujali mawimbi yanayoikumba,
tukumbuke dr Slaa anatumiwa na chama chake kipya, ccm kuiua CHADEMA.
uchaguzi mwakani atarudishwa kukitetea chama cha ccm,
Moja ya Mjumbe wa kamati kuu aliyekwenda na ujumbe wa kamati ndogo ya kamati kuu kwenda kuongea na Dk Slaa kuhusu uamuzi wake huo.
Jambo kubwa alilolalamika ni kwamba hamkubali LOWASA lakini tatizo kubwa lilokuwa dhahiri ni kwamba alishafanyiwa maandalizi yote ya kuwa mgombea Urais kwanini ghfla tu Kamati kuu inafanya mabadiko ya mgombea.
Tulimpa facts zote lakini hakutaka kutuelewa.
Katika kikao Cha kamati kuu alipewa facts zote kwanini ni muhimu kumkubali Lowasa licha ya upungufu ambao uitajwa kwa LOWASA na kwamba yeye hawezi kukipa chama ushindi au upinzani ambao ungefanana na wa LOWASA pamoja na upungufu ambao LOWASA alisemekana anao.
Kamati kuu ilimuambia Demokrasu ni kuhusu watu na watu wanasema nini kwa wakati huo.
Mwaka 2015 LOWASA alikuwa ni mwanasiasa anayekubalika kwa jamii ya makundi yote kuliko mwanasiasa yoyote kwa kipindi kile hususani kwa wagombea Urais waliokuwa wametia nia.
Tulimueleza Dk kuanza kutafakarifu udhaifu wa Lowasa ambao kwa maeneo mengine umeongezewa chumvi ilihali wananchi wanampenda hakutusaidii kupata ushindi au kutoa upinzani wa kutosha kwa mgombea wa CCM.
Na mimi binafsi nilimuambia Dk Slaa hata kama LOWASA hatashinda Urais lakini atakuwa Katibu mkuu wa Chama kikibwa sana nchini.
Naamini uwezo wa Dk Slaa ni Mkubwa sana kwahiyo angesimama kwenye nafasi ya ukatibu mkuu kipindi kile cha uchaguzi tungepata idadi kubwa ya wabunge na madiwani kuliko tuliopata sasa
Lakuni hata kura za uais huenda zingekuwa nyingi kuliko zilizopatikana kwa matangazo ya Tume ya Uchaguzi
Kwahiyo nadhani kitabu chake anataka tu kuwaaminisha wananchi kuhusu uhalali wa uamuzi wake lakini kama hakuwa na mbegu ya ubinafsi hakupaswa kufanya uamuzi ule aliofanya.
Yote yamepita ,
CHADEMA tunapaswa kusonga mbele kwani haya tunayopitia ndio kanuni za mchakato wa safari tunayotaka kwenda
Kwavyovyote vile safari lazima ifike mwisho
Sasa...unaonekana hutaki kujua na naombea mtu asikupe kitabu Cha bure.. Sasa mtu una maswali mengi na umepewa mahali pa kupatia majibu...hutaki! Oh "mpaka nibembelezwe na kupigiwa ngoma". Sasa si Bora uendelee na kukaa hivyohivyo?
Utajifunza nini kwa mtu ambaye yeye mwenyewe haaminiki tena?.....Ni ngumu sana unless, tuanze na matengenezo (restoration) kwanza...
Huo ni msimamo wangu
Yaani, kuna kisa humo ukikisoma utajua kuwa vita hii ya ufisadi haipiganwi kwa suti...Kumbe hata baadhi ya maaskofu wa kanisa katoliki ni mafisadi.
Ngoja nitafute hicho kitabu ili kuelewa zaidi.
Kwa hiyo tunajadili kitabu cha Lowasa?
Pili, usijifanye hukuisoma paragraph ya pili kwamba wapo ambao hawakuunga mkono ujio wa Lowasa upinzani nda ndio maana HAWAKUYASALITI YALE WALIYOYAAMINI NA KUYASHIKILIA kwa kufanya kile alichokifanya huyu unaempigia kijitabu chake chepuo.
Hoja ya msingi ipo wazi na inafubaza juhudi zako za hii promosheni.
Mwanakijiji ni Mnyakyusa wakati Dr. Slaa ni Muiraq!! Hawa ni watu wawili tofauti.
Pascal.. kama mtu kauoa na asimfanye mkewe kuwa kila kitu hiyo siyo ndoa tena. Unamnyoshea kidole Dkt. Slaa kwa vile kampa kipaumbele mkewe na watoto wake? Mwanamme usipompa nafasi ya kwanza mkeo.. unampa nani?Japo sijakisoma hicho kitabu ila kuna vitu Dr. Slaa hawezi kusema, kwa vile mimi nilibahatika kukaa nae mahali akiwa na mkewe Josephine, just the three of us, Josephine ndio kila kitu kwa Dr. Slaa, kule kujidai kususa kwa sababu ya kugombea urais it's all just lies kwa sababu msimamo naujua from horses mouth, kwa vile yalikuwa maongezi ya off the record, sio ustaarabu kusema walisema nini ila mimi humu nilisema haya kuhusu Chadema, hakuna akiyeamini ila ukweli ni huu.
Mbona mnarudia maneno kama mmekariri; Dkt. Slaa yuko CCM?Mkumbushe Dr Willibrod Slaa alisema hawezi kukaa na Kinyesi (ENL) CHADEMA
Akakimbilia CCM, sasa Kinyesi kimemfuata huko huko CCM
Biashara hiyo ilishachina zamani sana.M. M. tunashukuru kwa taarifa hizi nzuri. Pamoja na hayo mimi nashauri ufanye pia mabo mawili yafuatayo:
MOJA: KAMA INAWEZEKANA, kitangazwe pia kwenye TV kama kilivyotangazwa cha Mh. Dr. Reginald Mengi "I CAN I MUST I WILL"
MBILI: Kisambazwe kwenye sehemu nyingine nyingi kama kilivyosambazwa hicho nilichokitaja hapo juu, MLIMANI CITY ikiwa ni sehemu mojawapo.
Nahisi mambo haya mawili yakifanyika, nakala nyingi zaidi zitauzwa.
Ubarikiwe na nikutakie siku njema sana.
Yaani, watu kama hawa wamezoea kupikiwa, kutafuniwa, kulishwa halafu waambiwe ni kitamu!Kamata kitabu kamanda!
Unataka usomewe kila kitu?
Hivi hajafikia umri wa kustaafu huyo babu?Hivi Dr Slaa hajatumbuliwa kwenye Ubalozi?
Mwanakijiji Slaa anakula, tukiwa tunakula Africa hatuongei tukiongea ni kwa ruhusa ya baba au mama. Huyu (sijasoma na sitasoma kitabu hicho) ameandika kusifia Jiwe, most likely, ANAKULA, HARUHUSIWI "KUONGEA"
Wahi nakala yako bosi; ni nakala chache tu zimechapwa kwa ajili ya kuweka rekodi katika usahihi wake.Siasa za 2015 hasa ule usiku wa kumpokea Edward Lowasa na Dr. Slaa kuwekwa pembeni ndio ulikuwa mwanzo wa dhoruba Baharini......
Nahitaji hiyo nakala Mzee Mwanakijiji
Wasiliana na Tumbo atakufanya utaratibu...ARUSHA KINAPATIKANA WAPI?