NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

(Pichani kitabu kikianza kupatikana kwa Wabunge, Dodoma)

Na. M. M. Mwanakijiji

Umpende au umchukie, umkatae au umkubali, umpinge au umuunge mkono Dkt. Wilbrod Slaa Dr Willibrod Slaa anabakia kuwa miongoni mwa wanasiasa wachache Tanzania ambao alama zao katika zama na nyakati za kisiasa ni vigumu kufutika. Unaweza kumuita majina mengi na ya rangi mbalimbali ya kejeli lakini ni vigumu kupuuzia, kudharau au kutupilia mbali mchango wake katika siasa za Tanzania kwa karibu miaka ishirini na mitano. Mchango wake katika kuimarisha siasa za Tanzania akiwa miongoni mwa wabunge wa kwanza kabisa wa upinzani umeacha historia kubwa kuanzia Karatu hadi Dar, toka Tunduru hadi Tarime.

Hata hivyo, matukio ya kisiasa ya mwaka 2015 yanabakia katika historia yetu kama mafundisho makubwa kabisa ya siasa zinavyoweza kuwafanya ndugu wawe maadui, marafiki wake mahasimu, na kutengeneza kile ambacho wenzetu Wamarekani wanasema ni “strange bed fellows” yaani kuwaona watu usiowadhania wamelala kitanda kimoja. Matukio haya yalitokea taifa likiwa katika mwamko mkubwa wa uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge.

Dkt. Slaa akiwa Katibu Mkuu wa chama Kikuu cha upinzani cha CHADEMA, alitarajiwa na alipitishwa na chama chake kuwa mgombea wa Urais huku mtifuano mkubwa ukitarajiwa na hatimaye ulitokea ndani ya Chama cha Mapinduzi. Kwa baadhi ya wachunguzi wa siasa mtifuano au mnyukano uliokuwa unatokea CCM ulifanya kazi ya mgombea wa upinzani uliounganika kuwa ya afueni zaidi.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya watu wengi na kinyume na mantiki zilizozoeleka za kisiasa Edward Lowassa aliyekatwa jina lake ndani ya CCM ambako alikuwa anaongoza kwa mashabiki na kura za maoni alikimbilia CHADEMA na kusababisha chama hicho cha upinzani kulala kitanda kimoja na mtu ambaye walitumia muda mwingi kumhusisha na ufisadi nchini. Ilisemwa “yeyote” isipokuwa CCM. Dkt. Slaa akafyekelewa mbali na chama chake na kusababisha mpasuko wa aina yake ndani ya CCM na CHADEMA.

Dkt. Slaa akaamua kuachana na siasa za vyama na yeye na familia yake wakahamia Canada. Miezi michache baadaye Rais John Magufuli alimteua Dkt. Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden kitu ambacho kilitafsiriwa na baadhi ya watu kwa namna mbalimbali.

Katika kitabu cha NYUMA YA PAZIA Dkt. Slaa anaelezea kwa kina matukio mbalimbali ambayo yalitokea hadi kufikia Lowassa kukaribishwa CHADEMA na kwa nini hakuwa tayari kusimama jukwaani kumnadi Lowassa na akabakia na utimamu wa kimaadili na akili. Hata hivyo, kitabu hiki kinaenda zaidi ya nyuma ya pazia la siasa za 2015. Inatufunulia kumuelewa Dkt. Slaa kwani kwa kiasi chake kitabu hiki pia ni bibliografia (historia ya maisha) ya mwanasiasa huyu nguli, mcheshi, na msomi.

Ndani ya kitabu hiki tunaweza kukutana na mtu ambaye anatufundisha mambo mbalimbali kuhusiana na uongozi. Mojawapo ya mambo ambayo msomaji atayafurahia atakapokutana nayo ni jinsi gani Dkt. Slaa ni mtunzaji mzuri sana wa kumbukumbu. Siyo tu katika akili lakini katika nyaraka na vielelezo mbalimbali. Anataja tarehe, mahali na siku kama shahidi katika kesi nzito. Bila utata anataja pia majina mbalimbali ya wahusika mbalimbali katika ujasiri ambao utawakumbusha watu wengi ile hotuba yake ya “Orodha ya Mafisadi” ya pale Mwembe Yanga.

Kitabu hakigusi siasa tu za 2015 lakini pia kinatudokeza safari ya Dkt. Slaa kutoka upadre hadi kuwa mwanasiasa mbobezi. Wengi watashtushwa, kushangazwa na kuburudishwa na masimulizi yake ya mikutano yake na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere wakati huo Dkt. Slaa akiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu. Pia watakutana na jinsi gani Dkt. Slaa alisimamia kupinga ufisadi ndani ya Kanisa Katoliki kiasi cha kumgonganisha yeye na mmojawapo wa maaskofu waandamizi wa wakati huo. Msomaji pia ataburudishwa na masimulizi yake ya kujaribu kuinua hali na maisha ya watu wa Karatu katika kile ambacho kilimsababishia kuwa mbunge mpendwa sana wa wana Karatu na kuthubutu kufanya kitu ambacho hakikuwahi kufanywa Tanzania – Karatu kuwa Halmashauri ya kwanza ya mji kuongozwa na upinzani.

Kubwa hata hivyo, ni sakata zima la siasa za 2015 na matokeo yake katika upinzani na siasa za Tanzania. Kitabu hiki kinatoa maonyo, mwongozo, na elimu kwa wanasiasa wanaofuatia katika upinzani na chama tawala na wapinzani watarajiwa na watawala watarajia. Mwanasiasa yeyote ni lazima apate nakala ya kitabu hiki, mwanahistoria yeyote ni lazima anunue nakala yake wakati wanafunzi wa shule na vyuo watapata elimu muhimu juu ya uongozi kutoka katika kitabu hiki kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Nyuma ya pazia ni kitabu kinachomfunua mbele yetu na kutujulisha kwa undani juu ya mtu, maisha, zama na nyakati za Dkt. Wilbrod Slaa, Balozi, Baba, Mume na miongoni mwa viongozi maridadi ambao Tanzania imepata nafasi ya kuwa nao na wameacha alama zisizofutika. Umpende au umchukie, umkatae au umkubali, umpinge au umuunge mkono Dkt. Wilbrod Slaa ametupatia hazina ya maarifa ambayo wenye hekima watawahi kuipata katika nakala chache ambazo zimeshaingia nchini.

UNAWEZA KUPATA NAKALA YAKO WAPI?
Unaweza kupata nakala yako kwa bei ya jumla au rejareja. Bei ya reja reja ni shilingi 20,000/- TU na kwa bei ya jumla unaweza kupata punguzo kubwa kufuatana na mahitaji yako.
Maeneo ya posta, mkabala na Jengo la Benjamin Mkapa karibu na Mahali yanapoegeshwa magari yaendayo Sinza yenye michoro ya Rangi Nyekundu.
Mhudumu Genoveva - 0753 059 144
Au wasiliana na Erasto Tumbo kuweza kuagiza nakala zako:
0713 474707/0688 211683
Hatununui
 
Vipi ameelezea pia uhusika wa Josephine Mushumbuzi kwenye harakati zake na uhusika wake pale 2015??

Ameelezea aliendaje Canada na aliishije.
Vipi Ile press ya pale Movenpick zamani ameelezea nani aliyeilipia?

Ana sababu zipi za msingi zinazomfanya awe ni mtu mwenye msimamo na kusimamia anachokiamini?

Kwanini anaiunga mkono awamu ya tano? Na kwa tafsiri yake je upinzani usiwepo Tanzania??

Kama hayo kaelezea nanunua kitabu..
Nunua kitabu!
 
Ila ni kweli kuwa, kama anaendelea kumtaja Edward Lowassa katika kitabu chake kama sababu ya yeye kuachana na "siasa za vyama" katika mtazamo uleule aliokuwa nao mwaka 2015 alipohama na kurudi nyuma.....

Basi, hakika mantiki na maudhui yote ya kitabu hicho yanakuwa "invalid" na yanakosa maana yoyote kwa sababu, tayari tena MTU huyohuyo (his nightmare) "wanalala naye kitanda kimoja hukohuko CCM!!"

Sijui atawaambia nini watu ktk hili....

Anyway, kwangu mimi kwa kulielewa hili i.e Edward Lowassa vs yeye Dr Slaa, siwezi kununua kitabu hicho unless nipewe bure labda naweza kujitahidi kukisoma hivyohivyo....
Sasa...unaonekana hutaki kujua na naombea mtu asikupe kitabu Cha bure.. Sasa mtu una maswali mengi na umepewa mahali pa kupatia majibu...hutaki! Oh "mpaka nibembelezwe na kupigiwa ngoma". Sasa si Bora uendelee na kukaa hivyohivyo?
 
i will buy and read this book as intellectual ila credibility ya Dr Slaa kwangu ishaondoka kabisa. Ila najua ni mtu mwenye fikra na historia kwa hilo kitabu chake ni muhimu kwa sie tunaopenda kujifunza.
You are a smart person! An attitude of a true intellectual!
 
Wewe bila ya shaka Ni mtu mwenye hekima na uthubutu wa kifikra. Yaani huogopi kujitangaza utapata nakala yako. Watu kama wewe unaonekana wamepujlngua JF... Ila unanipa matumaini!
Why niogope mkuu? Mimi ni mtu huru na napenda kusoma vitabu ndiyo jambo mojawapo ninalopenda so kuogopa kusema nitatafuta copy moja ya Dr naona nikawaida sana maana najua kuna kitu nitajifunza kipya.

Siasa haijawahi kunitawala,Tz siasa zinawatawala watu , hata reasoning inamezwa huko.
 
Mweh..Sasa kitabu kinajaribu kujibu swali hili kwa kina.
Ilishakula.kwakwe yeye apambane kutumikia tu hao mashetani wenzake maccm, kumbe naye ni mnafiki tu. 2015 ilikuwa lazima kila mtu aonesha maamuzi magumu, na naamni kama asingejitoa tungekuwa tunapeperusha bendela ya Ukawa nchii hii

Sasa kapewa Ubalozi kazi ngumu sana hiyo..Inahitaji maamuzi magumu kuliko ya 2015.

Ni sawa na kusaini mkataba wa Kuzimu.
 
Huko nyuma tulikuwa pamoja na Padre Slaa vizuri tu. Lakini alipoingia Lowasa CHADEMA, sikumwelewa kabisa Slaa. Ningeelewa kama angekaa pembeni na kuachana na siasa, akatulia. Lakini kuiunga mkono serikali ya CCM? hapo sitakaa nimuelewe kabisa - eti hana chama!! thubutu yake!! anaganga njaa tu kama wengine. Slaa amekuwa mwepesi sana.
Sla alishajiharibia na sasa anajaribu kurudisha heshima aliyopoteza, ni aina ya compassion and obsession tatizo la.kisaikolojia linamuamdama. hicho kitabu hata aandike kurasa 10000, hakina maana yoyote zaidi ya kijitetea usaliti wake kwa watanzania anataka kujustify why aliondoka.

Nani alikuwa hajui mapungufu ya Lowasa??
 
Hakuna kiongozi Tz aliyenivutia kushabikia siasa za upinzani kama dr W. Slaa.
Lakini tangu 'walivyomnywa' mafisadi kihuni, sina hamu tena Cdm.

Sasa huku ninakoishi mkoani Kgm ntakipataje, japo umetoa namba za simu?
Wasifu uliompatia kwenye thread hii unamstahili.
Wasiomuelewa vizuri dr.Slaa hawatakuelewa
Saaa mbona wako naye tena Lowasa kule kule unasemaje ndugu yangu mtani wa hapo Gungu Mwandiga??
 
Soma kitabu halafu uje na maswali.. duh

Hakuna kipya kwenye hiki kitabu. Kingekuwepo kama kungekuwa na chapter aliyoi-dedicate kwa usaliti wa yote aliyoyaamini na kuyafundisha. Na hii ingekuwa ya kwanza ya kufungulia kitabu!

Wapo ambao hawakuunga mkono ujio wa mamvi upinzani lakini kwa sababu ya yale wanayoyaamini na kuyashikilia, hawakuyasaliti.
 
Sla alishajiharibia na sasa anajaribu kurudisha heshima aliyopoteza, ni aina ya compassion and obsession tatizo la.kisaikolojia linamuamdama. hicho kitabu hata aandike kurasa 10000, hakina maana yoyote zaidi ya kijitetea usaliti wake kwa watanzania anataka kujustify why aliondoka.

Nani alikuwa hajui mapungufu ya Lowasa??
Yaani bado unahalalisha ujio wa Lowassa na huoni Hindi upinzani ulivyogereshwa na kuvurugwa? Nilidhani watu wameamka...Yaani ulikuwa radhi Lowassa awe Rais wa Tanzania?
 
Hakuna kipya kwenye hiki kitabu. Kingekuwepo kama kungekuwa na chapter aliyoi-dedicate kwa usaliti wa yote aliyoyaamini na kuyafundisha. Na hii ingekuwa ya kwanza ya kufungulia kitabu!

Wapo ambao hawakuunga mkono ujio wa mamvi upinzani lakini kwa sababu ya yale wanayoyaamini na kuyashikilia, hawakuyasaliti.
Na haoni kujipinga kwenye maneno yako? Yaani unampokea Lowassa na bado unajiita mpinzani mwenye msimamo?
 
Yaaaaaaani unavyompenda Slaa hadi kero, ungekuwa jinsia ya ke pengine ingekuwa story nyingine!

Wewe na Slaa mna side na watesaji wa Lissu na wapotezaji wa Saanane, Mawazo, Azory

Kitu msichojua wewe na kibabu Slaa ni kwamba hata akishuka Shetani upinzani wakampa ticket atapata kura yetu
 
Na haoni kujipinga kwenye maneno yako? Yaani unampokea Lowassa na bado unajiita mpinzani mwenye msimamo?

Kwa hiyo tunajadili kitabu cha Lowasa?

Pili, usijifanye hukuisoma paragraph ya pili kwamba wapo ambao hawakuunga mkono ujio wa Lowasa upinzani lakini HAWAKUYASALITI YALE WALIYOYAAMINI NA KUYASHIKILIA kwa kufanya kile alichokifanya huyu unaempigia kijitabu chake chepuo.

Hoja ya msingi ipo wazi na inafubaza juhudi zako za hii promosheni.
 
Toka Gwajima amwage ukwl kuhusu huyu bwana na kushindwa kutoa ufafanuzi mpaka Leo hii huwez nishawishi lolote kuhusiana na kiumbe huyu
 
Usikubali kufungwa mawazo wako na hisia. Ukisoma vitu vinavyokufurahisha kihisia tu utajikuta kuwa mawazo yako yanatawaliwa na hisia. Hatusomi au kujifunza kwa watu tunaokubaliana nao tu bali hata tusiokubaliana nao au wale ambao hatuwajui kabisa kiasi cha kuweza kuchagua upande. Kuna watu humu nawasoma inaonekana na wao waliumia sana kwa Dkt. Slaa kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo hisia zao na labda akili zimeumizwa mno kiasi kwamba ukitaka "Dkt. Slaa" wanakuwa kama Manchurian Candidate. Mtu aliyekomaa kihisia, kiakili na kisiasa haogopi au hajidhanii kuwa hafai kujisomea mambo kutoka kwa mtu asiyekubaliana naye. NI suala la ukomavu tu.

Kwa wale ambao wanapanga kusoma au tayari wamesoma nina uhakika watamaliza wakiwa na ufahamu mkubwa sana kuhusu maisha na siasa za Dkt. Slaa na kwa kiasi kikubwa wataweka mitazamo yao katika mitazamo sahihi na labda hata kubadilisha mawazo yao au kuyathibitisha waliyokuwa nayo awali
Mkuu tudokeze like tukio la kuingia hotel ya Moven Peak kupitia uani eti kwenda kuianikaRichmond na Lowasa mmelielezeaje kwenye kitabu chenu!?
 
Back
Top Bottom