NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

Mzee Mwanakijiji Gulwa na Laface77 wanadai Dr. Slaa ni mzinzi toka akiwa Padri na baada ya kuacha Upadri, ni kweli? Na je kwenye hicho kitabu chake kaelezea ilikuwaje aliacha Upadri. Jee Suala la Uzinzi ni sababu mojawapo ya kuacha Upadri?
Mkuu nilitegemea ungejielekeza kwenye hoja kuliko kumshambulia Dr Slaa binafsi na maisha yake.

Sidhani kama maisha yako hayana doa kabisa.!
 
Mkuu nilitegemea ungejielekeza kwenye hoja kuliko kumshambulia Dr Slaa binafsi na maisha yake.

Sidhani kama maisha yako hayana doa kabisa.!
Ni kijana bado yuko emotional and idealistic.. muda tu utaamua.
 
Tuko pamoja binafsi nawaza jinsi ya kukipata sijui kama kitasambazwa mpaka huku mikoani.
Mkuu. Wale CHADEMA original lazima tukinunue tukumbushie enzi zetu kabla akina Tundu Lisu na mwenyekiti hawajakiuza chama chetu kwa CCM.
 
Bila shaka hichi kitabu kitafanya vibaya sana katika mauzo yake. Naamini hata endapo bashite angekuwa kaandika kijitabu chake, hapana shaka kingefanya vizuri zaidi sokoni kushinda hiki cha Dr.Mihogo.
 
Nyie vijana acheni dharau. Laiti kama ungejua upambanaji wa dhati wa Mzee Mwanakijiji na Mh. Dr. Slaa usineliufungua huo mlango wako wa mbele kuyanena yasiyofaa dhidi ya watu hawa.
Hawajui kuwa vitu vingi wanavyovifuata leo ndani ya Chadema mawazo ya Mwanakijiji yamehusika kwa asilimia kubwa.
 
Katika vuguvugu la ujio wa Lowasa 2015 mimi binafsi nilisimama upande wa Slaa. Lakini kitendo alichokifanya baada ya pale ya kuanza kuisapoti CCM hapo ndipo mimi nilipokosana nae.
 
Bila shaka hichi kitabu kitafanya vibaya sana katika mauzo yake. Naamini hata endapo bashite angekuwa kaandika kijitabu chake, hapana shaka kingefanya vizuri zaidi sokoni kushinda hiki cha Dr.Mihogo.
Kwa jinsi nilivyoelewa hicho kitabu hakipo kwa ajili ya biashara bali kuweka rekodi sawa kilichotokea 2015.

Dr Slaa angeondoka duniani bila kuandika kitabu nini kilitokea 2015, historia ingemhukumu sana.

Nadhani na yeye kwa sasa ametua mzigo, historia ndio itachambua iwe leo ama kesho.
 
Mbona mnarudia maneno kama mmekariri; Dkt. Slaa yuko CCM?

Mzee hoja zako kuwa na mashiko ni kazi sana siku hizi...🤣

Substance ya matendo yake ndio inayomfanya awe CCM. Siyo tu kwa kuunga mkono utekelezaji wa sera za serikali chini ya hiki chama, bali kwa kukubali na kutumikia uteuzi (tena kwa kula kiapo) utokao kwa M/kiti wa chama. Sasa usije jaribu kutenganisha chama na serikali iliyopo madarakani...

Kuwa na kadi ni legal form tuu ila substance tunaiona.

By the way, kwamba hatujawahi kuona akipewa kadi haimaanishi kwamba hana kadi!
 
Tokea siku nyingi sana hua naamini kwamba MM ndio Dr. Slaa, pamoja na utetezi mwingi wa kuwatofautisha but still akili yangu bado hua inaamini kwamba Dr. Slaa=Mwanakijiji
Hapana in watu tofauti sema marafiki sana. Ukichunguza kama ww in mkongwe hapa masjala Dr slaa alikuwa anamatatizo ya sarufi kwenye kuandika tofauti na M.M
 
Kwa jinsi nilivyoelewa hicho kitabu hakipo kwa ajili ya biashara bali kuweka rekodi sawa kilichotokea 2015.

Dr Slaa angeondoka duniani bila kuandika kitabu nini kilitokea 2015, historia ingemhukumu sana.

Nadhani na yeye kwa sasa ametua mzigo, historia ndio itachambua iwe leo ama kesho.
Hili ndilo lengo lake kuu zaidi. Lakini kubwa ni kuwa anatufungulia vikao, simu, maneno, na mikutano ambayo ilikuwa inatokea. Lakini kubwa zaidi ni kufunuliwa kwamba.... wakati watu wanajifanya wanajaribu kumualika Lowassa ndani ya CHADEMA....
 
Back
Top Bottom