Nyuma ya Pazia; TFF -AZAM TV Haki ya Matangazo

Nyuma ya Pazia; TFF -AZAM TV Haki ya Matangazo

Boss vyema kama hujui ukauliza...tenda ilikuwa wazi na wazabuni waliojitokeza kuomba ni pamoja na TBC 1 kupitia Startimes, Startv kupitia continental decoda , na ATN kupitia TING ...so you see..watu waliojitokeza kuweka mzigo mezani..hoja za Azam TV zikwap shawishi zaidi kuliko hao wengine...

Na kingine watu mnalia Sana na DSTV Ila kiukweli DSTV asingeweza kutoa pesa ata robo ya aliyotoa Azam TV.. zingatia alichotoa kwenye ligi za Zambia na ethiopia ambapo huko anasoko kubwa pia Kama hapa TZ.

Utasema mbona Katoa mzigo mkubwa Afrika kusini, jibu ni simple tu kule Afrika kusini DStv ni kama Azam TV kwa hapa bongo..wanawateja wengi na uhakika mkubwa wa return ..the same na Azam TV hapa ..ingekuwa Azam TV anazamnini ligi ya kenya asingetia pesa nyingi hivi..simple kwa kuwa hana return kule.

Ukijumlisha dau ambalo angetoa washindaji wote hao ..kwa.miaka kumi ijayo..isingeweza kufika dau aliloweka Azam TV ..

Sio Kweli. Tenda haikuwa Opening.

Weka Uthibitisho hapa hapa. Sote tunajua process za Tendering na Procurement method kwa mujibu wa Procurement Act 2011, Regulation 2013 na Maboresho 2016.

Ndiyo uzuri wa kujadili kwa pamoja.

Hoja ya pili hapa ni huo mkataba wa miaka 10 kwa bili 225 bila ya kujali other factors na value for money.

Je unajua vipengele vyovyote vilivyomo ndani ya mkataba.... any contract terms?

Je unajua maana ya value for money ndani ya miaka 10 ijayo? Inawezekana Azam amesaidia kuitangaza ligi na watu kupenda mpira, lakini hiyo haitoi amefanya sana biashara na haitoi uhalali wa Monopoly.

DSTV ni kama Azam kwa SA, mkataba wake hauzidi miaka 4 na anaweka mpunga wa maana.

Naomba uliangalie hili katika mtazamo chanya pasi na majungu tujadili kwa akili
 
Mosi , Napinga HOJA ya kwamba AZAM TV imekuza soka letu na kuboresha ubora VPL.
Ukweli ni kwamba VPL na SOKA letu limekuwa kulingana na NYAKATI kama ilivyo katika Muziki kwa sasa.

Pili, katika MKATABA huo, hakuna dalili yoyote ya kwamba TARATIBU za manunuzi ya Umma zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kuwashindanisha WAZABUNI . MKATABA umetolewa kwa muktadha wa UZOEFU na sio katika TARATIBU za Manunuzi ya Umma.
View attachment 1801626

Mathalani, tukiangalia Ligi ya South Africa, WAZABUNI hushindanishwa PUBLICLY na kumpata COMPETITIVE BIDDER mwenye thamani kubwa. Aidha, MKATABA unakuwa ni kati ya miaka miwili hadi mitatu tu. Kila timu inapokea Bil 4 kwa mwaka huku mshindi wa PSL akipokea Bil 6 ikiwa ni jumla ya shilingi Bil 10.

Tatu, Kuna viashiria vyote ya kwamba TFF na Wizara ya Habari na Michezo imeshawishika kwa namna moja au nyingine kwenye MOTIVE ya AZAM TV. Hivyo basi, CAG na TAKUKURU hii ni KAZI yenu . Kuanzia Wizara ya Habari na Michezo mpaka viongozi wa TFF WACHUNGUZWE kwa kusaini MKATABA wenye thamani ya Bil 225 tu kwa miaka 10 mfululizo huku other factors are not constant. Tafiti zinaonesha ya kwamba hakuna TV sponsor katika MATAIFA mengine imepewa haki ya matangazo kwa miaka 10 mfululizo bila ya KUSHINDANISHWA na WAZABUNI wengine. Je, hawa wenzetu wameyatoa wapi kwa mantiki ya Value for Money( VFM).

Nne. Halikadhalika tafiti zinaonesha ya kwamba endapo kama kungekuwa na COMPETITION ya WAZABUNI yaani Open Tendering basi the highest BIDDER angefika kati Bil 800 hadi 1 Trilioni kwa kipindi hicho cha miaka 10.

TAKUKURU na CAG,
1. Special AUDIT kwenye mlolongo mzima wa MKATABA huu ufanyike kuanzia ngazi ya Wizara hadi TFF
2. Muda wa miaka 10 bila ya kushindanisha wazabuni wengine, ni ANGAMIZO na MANUFAA ya watu wachache; MKATABA kati ya miaka 2 na 3 ungekuwa na TIJA katika THAMANI ya FEDHA na kuongeza ushindani katika other interested bidders in the near future.
3. Je Financial Intelligence kubaini MAKUSANYO ya AZAM katika haki ya matangazo kwa mwaka unaoishia inasemaje?

CAG na TAKUKURU fanyeni kazi yenu kudadavua huo UKAKASI.... kuna KAHARUFU kuanzia WIZARA husika hadi TFF.
Mwisho, mada hii haina any personal issues, ni katika kutoa FURSA ya kuhoji mambo ya msingi na kuangalia mambo yetu katika jicho la tatu; There is no FREE LUNCH , NEVER!
Lisemwalo lipo
 
Akili ndogo kama zako ndo huwa wanajadili matukio na hawawezi kamwe kusababisha matukio. Azam kaweka pesa yake unaona nongwa ety? Wapuuzi kama wewe washawahi mchefua vodacom najua klabu zilikiona cha moto. Unadhani azam asingeliweka pesa ni nani angeliweka au ndo ungekuja na uzi wa kuponda tff tena kwa kufukuza wawekezaji? Nina imani kupitia hiki walichokifanya azam huenda ligi ikaongeza ushindani kwa bonas zile sio kila upuuzi uuoneshe kwa watu au ndo unatufuta kazi ya uchambuzi ndugu?

Huo ushindani wa ligi unaongezeka vipi ikiwa Azam kapewa pin ya 10 years?

Maneno kama Akili ndogo au kutafuta kazi ya uchambuzi haina uhusiano na Mjadala huu.
 
Ela aliyotoa Azam Media si DSTV wala media yoyote ingeweze kutoa kwa soka la bongo. DSTV Kenya walikuwa wanatoa 7bn Tsh kwa mwaka, wakati Azam wamekubali kutoa 22bn Tsh kwa mwaka kwa Tz, pili bei za vifurushu vya DSTV si rafiki kwa uchumi wa watanzania wengi, wakati Azam 20k tu unaona VPL kama yote.

Kwa Vigezo gani ?
 
We we una post pumba zako hapa kwa manufaa ya nani?? Ficha ujinga wako mkuu!!
Ni aibu kubwa kutokujua mchango wa Azam TV kwenye kukuza soka letu!

Maneno kama pumba na ujinga hayana uhusiano na mjadala huu. Ninakuomba ubaki kwenye topic ili tujadili kwa mapana
 
We binafsi umefanya nini kwa miaka kumi iliyopita.bado uko VB kwa shemeji yako then unasemaje mingi sana

Alichofanya binafsi ndani ya miaka 10 iliyopita hakina uhusiano na kinachojadiliwa. Ninakuomba ubaki kwenye topic tujadili kwa maslahi mapama
 
Mwenye akili za kijinga ni yule anaepiga majungu kwa chuki binafsi na vijisababu vya njaa kama zako kuona Azam kupewa mkataba wa haki za matangazo.
Ni chuki tu ulizonazo huna jipya man.

Kwahiyo wewe unapinga watu kuhoji?

Sorry, nimekuita Mediocre Mind kwa sababu huna Mental Strength za kujadili hoja kinyume na mtazamo wako.

Matokeo yake unaishia kusema tunachuki na wivu. Ikiwa kila Mtanzania angekuwa na mtazamo kama wako, kungekuwa hakuna Sababu ya kuhoji mambo ya msingi.

Kama mimi nimepotoka, naomba utoe ufafanuzi yakinifu dhidi ya hoja iliyopo mezani.
 
Kwa maneno haya ya shombo, watu smart hawawez jadili hii mada, unaifunga mada makusudi ili uonekane unajua unachokiandika kumbe ni pumba tupu, wadhamini wa kuweke tilion 1 wako wapi Tanzania hii? Hizi ni porojo tu na fitna, tuache fitna tufanye kazi, kazi ya AZAM imeonekana ktk kusapoti ligi yetu, ndondi ma filam za ndani.
AZAM apewe haki yake afanye makubwa zaidi.
 
Kwa maneno haya ya shombo, watu smart hawawez jadili hii mada, unaifunga mada makusudi ili uonekane unajua unachokiandika kumbe ni pumba tupu, wadhamini wa kuweke tilion 1 wako wapi TZ hii? hizi ni porojo tu na fitna,tuache fitna tufanye kazi, kazi ya AZAM imeonekana ktk kusapoti ligi yetu, ndondi ma filam za ndani.
AZAM apewe haki yake afanye makubwa zaidi.

Hujaelewa vyema mada. Re read and focus kwenye topic ya msingi
 
Tenda ilitangazwa, mimi niliona tangazo kwenye mitandao ya TFF.
Ukubwa au udogo wa fedha zinazotolewa unategemea ukubwa wa uchumi wa nchi, usifananishe South Africa na Tanzania, jiulize wangapi South wanaweza kununua ving'amuzi na kulipia malipo kila mwezi, pia jiulize swali hilohilo kwa Tanzania.

Kuhusu miaka 10 ni kwamba Azam pia watatakiwa kununua vifaa, Kama camera, magari ya matangazo ambayo ni gharama kubwa, kuwapa mafunzo wafanyakazi nk.

Sasa akipata mkataba wa miaka mitatu anaweza kupata hasara maana itabidi ashindanie tenda na anaweza kukosa, kwahiyo Kuna ambo mengi Sana kuhusu huo mkataba.
 
Una miaka mingapi dogo !?? Miaka 5 nyuma hii livbi lin okiwa haielewek mdogo Angu tulikuwa tunafatilia mpira kwa redio
Azam katusaidia sana DSTV tuliwabembeleza sana watusaidie kuonyesha lig lakin waligoma walikuwa wanatakan mechi za watan tu
So usiwabeze Azam mdogo angu kisa umeikuta lig inaonyeshwa unashinda kibanda umiza jamaa wamewekeza sana ni muda wao wa kula matunda sasa
Wanachonifirahisha azam wako tayar kukuza soka letu watasapot timu zetu pia
Dstv wapumbavu sana walisema ligi yetu haina ubora wakati Kenya walikuwa wakionesha ligi yao kupitia GOTV Tenga akaamua kuwapa nafasi azam tv na imesadia sana kuongeza Thamani ya ligi yetu. Kwa mfuatiliaji wa mpira hii ishu hawezi kuongea huu ujinga.

Na walitangaza tenda Tff dstv, startimes wote wameanguka
 
Acha uchawi wewe tenda ilitangazwa afu huwez kufanisha south Africa na ligi yetu ni vitu viwili tofauti tumia busara

Okay, share hapa ilipotangazwa.
Hoja ya pili, contract duration na value for money unaizungumziaje, tunajadili Chief acha kupanic huenda ukajifunza kitu in the process
 
Next time jifunze KUANDIKA vyema.

Hoja ya msingi hapa sio habari za miaka 5 iliyopita. Hoja ya msingi Bil 225 kwa miaka 10 ni akili MUFILISI katika Karne hii.

Wewe unadhani kwanini yeye ame PIN muda mrefu hivo. Kumbuka huyu ana UZOEFU na ameshaona kuna madini kiasi gani Kwenye INVESTMENT hiyo.

Je unayo taarifa kwamba kuna kampuni nyingi sana zilianza kumendea hiyo FURSA baada ya kufanya financial analysis zao . Na walikuwa tayari kuweka mara 2 ya mzigo huo tena for less that 10 years.

Wewe unadhani hiyo PIN ya 10 years ni BAHATI mbaya ? Unadhani AZAM anashindwa kutoa 2 Bil kwa Wizara husika na TFF kuharakisha hiyo dili.

Je unajua sheria ya Restricted Tendering ? Je unajua kipengele chochote ndani ya mkataba huo. Unaimbishwa nyimbo ya hovyo na wewe unacheza.

Tafadhali, open your eyes and learn how to be skeptic.
Weee ondoa ujinga hapa mbona hawajashinda tenda ilitangazwa
 
Sio Kweli . Tenda haikuwa Opening.

Weka Uthibitisho hapa hapa. Sote tunajua process za Tendering na Procurement method kwa mujibu wa Procurement Act 2011 , Regulation 2013 na Maboresho 2016.

Ndiyo uzuri wa kujadili kwa pamoja.

Hoja ya pili hapa ni huo mkataba wa miaka 10 kwa bili 225 bila ya kujali other factors na value for money.

Je unajua vipengele vyovyote vilivyomo ndani ya mkataba .... any contract terms ?

Je unajua maana ya value for money ndani ya miaka 10 ijayo ? Inawezekana Azam amesaidia kuitangaza ligi na watu kupenda mpira, lakini hiyo haitoi amefanya sana biashara na haitoi uhalali wa Monopoly.


DSTV ni kama Azam kwa SA, mkataba wake hauzidi miaka 4 , na anaweka mpunga wa maana.

Naomba uliangalie hili katika mtazamo chanya pasi na majungu tujadili kwa akili
Kawekee wewe wako acha upuuzi
 
Back
Top Bottom