Nyumba anayodai Polepole imevunjwa siyo makazi yake ya kibunge, analaghai Umma akishirikiana na aliowakuza awamu iliyopita

Polepole walau anasimamia anachoamini, wangapi walikuwa karibu na JPM na leo wanamkana waziwazi hao unawaitaje? Mtu kama Nape ambaye alifikia hatua ya kutembea kwa magoti kuomba msamaha huku akimuita baba lakini leo hii anajimwambafai dhidi ya JPM (thanks to technology).

Wapinzani nchi hii ni highly hopeless na hawapaswi kuaminiwa kwa sababu hawana uwezo wa kuisimamia kweli bali maslahi binafsi.
 
Watanzania baadhi ni wavivu wa kufikiri huropoka tu bila kufikiria
 
Ama kweli hii ni JF mpya...nimetafuta like nilichokiona kwenye Heading sijakiona kabisa kwenye COntent!
Halafu kumbe Wabunge Wana Makazi ya Kibunge Dodoma...!?
Anyway huu ni Utopolo tu.
Ukweli unabaki palepale tatizo ni CCM
Sio utopolo ni makolo kabisa.
 
Hivi huyu Polepole umemfahamu juzi baada ya DIKTETA kumpa uKatibu Mwenezi wa CCM? You are not informed kwa kweli.

Je unamkumbuka Polepole wa Bunge la Katiba/ Tume ya Warioba? Kama angekuwa ni mtu wa msimamo asingekubali kufanya kazi na Magufuli. Ila Polepole ni mmoja kati ya wale ambao Nyerere aliwaita "Malaya wa siasa".

Sasa hivi siyo kwamba anamtetea Magufuli bali anatetea tumbo lake
 
Lakini pia kaongea Dar mara kesho yake anadai alikuwa Manyara na anarudi Dodoma ndo anakuta pamevunjwa je Hana majirani? Hawa watu wanapeana michongo ya kututawala Kwa kupanua magoli , tushtuke uhuni huu.[emoji23]

Nakutumia pm inakataa mbona umefunga
 
Mnapokuwa pamoja sio lazima mkubaliane kila jambo, na pia sio lazima kila mkitofautiana basi ujiuzulu. Pia kuna uwajibikaji wa pamoja, mnapokuwa kwenye vikao mnatofautiana lakini uamuzi ukipitishwa wote katika kanati ni lazima muusimamie hata kama wewe binafsi ulikuwa huuafiki. Je wewe na mkeo huwa mnakubaliana kila kitu?

Jadili au jibu hoja za sasa za Polepole .
 
Unajua maana ya UNAFIKI? nani manafiki kati ya Polepole na SAMIA
Bora Samia Ana endelea kuishi UNAFIKI WAKE.
Alafu Samia wakati yupo makamu hakuwa na maneno mengi.
Kama huyo muenezi na itikadi mstaafu.huyo alikuwa anatembea na ilani ya chama,wanatekeleza,
Huku watu wanakamatwa,wnafungwa,wanauliwa,wanatekwa n.k
ebu nenda kaangalie post za pole pole instagram.uone alikuwa je
 
jibuni hoja anazouliza polepole!!,achani kurukia vitu ambavyo havina mantiki,kuibiwa nako kwa kujadili.
 
Swala sio ku fake tukio,kununua wapinzani,kuwa kwenye serkali iliyopita..nk,,
Hoja za H.Polepole ni za kujibiwa.
 
Nakushukuru mkuu. Ubarikiwe sana
 
Swala sio ku fake tukio,kununua wapinzani,kuwa kwenye serkali iliyopita..nk,,
Hoja za H.Polepole ni za kujibiwa.
Mnaamini kwenye kujibu hoja nyie ? Mbona Tundu lisu alipohoji juu ya mkataba ya madini mlimminia risasi kama jambazi?????
 
Pole Pole Ni mmoja wa watu waliokua na nguvu na Ushawishi Mkubwa awamu iliyopita alipanda cheo haraka akawa Mwenezi wa CCM..Maovu na uonevu uliofanyika Yumo anajua anahusika au aliratibu....leo nae analia kwa style ile ile....
Ajitulize mana matendo ya serikali zote ni yale yale na kama hakukemea maovu asitudanganye sasa....

Sio yeye Tu wako watu wengi wameumiza sana watu....
 

Kinachotia moyo ni kuwa mawazo mengi mitandaoni si misimamo rasmi ya vyama.

Ieleweke CDM kama chama hakijawahi kujilaumu kwa kuwa na yeyote aliyekuja au kuondoka katika wakati wowote.

Chama makini kina agenda za kudumu si marafiki wa kudumu.

Kuna tofauti ya hoja za Polepole na Polepole kama mtu.

Kwamba anadai ananyamazishwa? Hata sisi tunanyamazishwa.

Kulitambua hilo halimlazimishi awaye yote kuchukua hatua yoyote. Hata kwenye kulazimishwa kwake, kuyatambua madhila ya kunyamazishana si muhani.
 
Polepole hana hoja yeyote zaidi ya kuwa ni fungu la kukosa. Muache afurahie uhuru wa maoni ambao Rais SSH ameturudishia baada ya Magufuli kutunyima miaka 5
 
Justice is a two way traffic, kama vile ambavyo unaruhusiwa kupita wewe wakati wa kwenda, basi ndivyo inavyotakiwa upishane na mwenzako apite anaporudi, lakini sio umkatalie kupita kwasababu ya sura yake! this is immaturity.
 
Hilo la Katiba mpya kuwa "ajenda ya kitaifa" si kweli. Inapaswa kuwa ajenda ya kitaifa lakini hadi sasa imebaki kuwa ajenda ya kundi flani tu. La muhimu ni kujibidiidha ili iwe hivyo ie ajenda ya kitaifa, japo najua "wasiopenda kushaurika" watakemea.
 
Justice is a two way traffic, kama vile ambavyo unaruhusiwa kupita wewe wakati wa kwenda, basi ndivyo inavyotakiwa umuache mwenzako apite wakati wa kurudi, lakini sio umkatalie kupita kwasababu ya sura yake! this is immaturity.

Ifahamike kuwa pana watu wasiotutakia mema katikati ya urojo rojo kama hizi:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

(Hiyo ikiwa kabla zile ya siku 100)
 
Ifahamike kuwa pana watu wasiotutakia mema katikati ya urojo rojo kama hizi:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

(Hiyo ikiwa kabla zile ya siku 100)
Naona bado unaendelea kutazama sura za watu, unakosea brazaj.

Haki za nchi hii hazimilikiwi na kikundi fulani cha watu, ni za watanzania wote bila kuwabagua kwa namna yoyote, au kuwahukumu bila kuwafikisha mahakamani. Yeyote anayenyimwa haki yake lazima tumpiganie kwa umoja wetu ili siku tukidai haki zetu, wawepo wakutusikiliza.

Vinginevyo ukiendelea kuleta hii segregation ya kuwatenga baadhi, na hii mentallity yako ndio inayofanya ionekane madai ya Katiba Mpya ni kikundi fulani cha watu, sio watz wote, tubadilike, nadhani utakuwa hujui hata maana ya haki tunayoipigania kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…