Mkuu Geoff,
Mada yako ni sensitive sana, inagusa hisia za akina mama sana lakini ukweli unabaki pale pale ... kwamba nyumba ndogo zitaendelea kuwepo na wanaume hawawezi kuzikwepa. Japo si wote wenye nyumba ndogo lakini wengi wao wanazo na kibaya zaidi wengine wanazo zaidi ya moja.
Nyamayao,
Signature yako inajibu mada yote ... wanaume tumetawaliwa na tamaa, ndiyo maana tunasema nyumba ndogo ni inevitable. Mwanaume akitamani husema amependa, huwa hatuwezi kutofautisha kutamani na kupenda, na pia hata tukitongoza siwezi kushusha verses niseme nimemtamani Nyamanyao na anikubali, maana ataniona nina matatizo. So nitasema nimempenda, na yeye ataingia King kirahisi then baada ya hapo ni kilio na kusaga meno.
Wanao amini Biblia waende kusoma Kitabu cha Waefeso Sura ya 5, ina ujumbe mzito kwa wana ndoa, mke ameagizwa AMTII mume, while mume ameagizwa AMPENDE mke. Hivi mtu anaweza kufunga ndoa na mwanamke ambaye hampendi? Kwa mwanaume tamaa na upendo ni identical twins ambao huwezi kuwatofautisha mpaka ukae nao kwa muda mrefu sana na ku-study tabia zao. In most cases wamama huwa wanakuja kugundua hakuna upendo when it is too late, alishafunga ndoa, kazaa na watoto na sasa yamebaki mazowea!
VeraCity,
Analysis yako ni nzuri sana, lakini umesahau kitu kidogo, siyo kwamba wanaume wanajiona wana haki, bali imani (dini) na mila ndiyo imewafanya wawe hivyo. Ukisoma Biblia, yule mwana mama aliyefumaniwa akizini, alipelekwa kwa Yesu peke yake, je, huo uzinzi aliufanya peke yake? Lazima kulikuwa na mwanaume. Je, kwanini mwanaume hakushikwa na kupelekwa kwa Yesu ili wote 2 wahukumiwe?
Juzi nimesoma kwenye mtandao, nchini Sudan kwenye mahakama za sharia, kuna mama amehukumiwa kupigwa mawe mpaka afe while mwanaume akahukumiwa kucharazwa bakora. Kosa ni uzinzi, kwanini adhabu ziwe na uzito tofauti?
Something is wrong somewhere, imani (dini) na mila zinawapendelea wanaume na ndio maana wanaona ni sawa tu kuwa na nyumba ndogo, after all hata wakifumaniwa anayetazamwa kwa macho makali na jamii ni mwanamke wala siyo mwanaume, mwanaume anaweza kuonekana ni kidume while mwanamke akabatizwa jina la malaya. Why?
Mchungaji Nguli,
Pamoja na kwamba kwenye mada flani watu walikuwa wana-question imani yako kwa kuwa una ukoo na Mkuu Bluray, kwenye mada hii umeonyesha uko juu katika ulimwengu wa kiroho na kwamba unamuogopa Mungu. Ninakubaliana na pendekezo lako kwamba wanaume wanapoomba mke wamshirikishe Mungu. Bible ndivyo inavyosema kwamba mke mwema hutoka kwa Mungu, lakini mali na mambo mengineyo unaweza kupewa na wazazi wako, ila siyo mke. So wanaume wakitaka kuoa waombe Mungu awafunulie.
Sasa kwenye hili la kufunuliwa Mama Mchungaji ZD, Mtumishi wa Mungu BHT na msaidizi wake Carmel wanaweza kutoa maelekezo ya jinsi gani mtu anaweza kufunuliwa na kuonyeshwa "mke mwema", maana haya mambo mengine ni ya kiimani zaidi. Wengine imani zetu haziko deep sana.