Nyumba hii nimeijenga kwa miaka mitatu

Nyumba hii nimeijenga kwa miaka mitatu

Sawa Baba mwenye nyumba Hongera si wengine Cha Muhimu punzi tu Mungu pekee
 
Ilikuwa Tarehe 02/09/2020 nilifanya maamuzi ya kununua eneo la makazi yangu Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mamlaka ya mjimdogo Katoro, kitongoji cha Inyala, Kata ya Nyamigota.

Baadae nilipata pesa kidogo nikajisemea kwa umri wangu huu ndio muda wa kutafakari na kuweka familia pamoja kabla sijaanza kusomesha, na mambo yatakapo kuwa yamebadilika niwe nipo kwangu nahangaikia chakula na maradhi nisiwe mtu wa kutukaniwa kwenye nyumba ya kupanga na kelele ni nyingi mno uko kwenye kupanga.

Maamuzi yangu yalikuwa haya baada ya kuamua mara moja na niliapa kwamba M/Mungu anisaidie mtoto wangu akianza shule niwemepata kwangu hii inisaidie nisiwe mtu wa kuhama hama. Maana ukiwa na makazi ya kuhama mara kule mara huku inachanganya kudumaza maendeleo ya mtoto na hili nilifanikisha.

Kingine kilichofanya nichukue uamuzi huu, ni kwasababu mimi ni mtu wa kuhama hama tena nikihama naenda mkoa mmoja au wilaya nyingine, niliona hii itanifanya familia yangu kugawanyika endapo nikikwama kwa namna moja au nyingine.

Na hapo sasa mtoto awe ndio ameanza shule unahama aisee, haya mambo yasikie tu.

Tuendelee....

View attachment 2674010
Upande wa mbele
View attachment 2674130
Tarehe 12 Nov 2021 Nilianza ujenzi na lengo la kujenga iikuwa ni chumba kimoja kwanza ajili ya kukifanya duka kwa sababu sehemu nilipokuwa nimenunua kiwanja/eneo niliona pako na mzunguko wa biashara ya duka sababu watu walikuwa wamehamia wengi na wengine walikuwa wanaendelea na speed ya kujenga kila kukicha nikaona hii kwangu ni fulsa kwa sababu hakuna mtu mwenyewe huduma kama hii kwa hapa.

Nilifanya vile kumwezesha mke aweze kujishughulisha kwa kutafutiapo mahitaji madogo madogo, hii niliona itamuongezea hali ya kujiamini na kumsaidia asiwe mpweke na kujihusisha na mavikundi pamoja na mavikoba na lengo langu, endapo nimekwama basi yeye anatoa kwenye mzunguko wake ananunua mboga mambo ya chakula yaani mahindi nimesimama kidete kuhakikisha kuwa chakula hakipungui yaani gunia za Mahindi ziwepo kuanzia 2 au 3 na bila kusahamu nyumbani kwetu nakumbuka kutuma gunia 3-4 za mahindi kwa msimu wa mavuno. Hii ni kuondoa matumizi ya hapa na pale kwa familia yangu ya zamani kwani bado nipo pamoja nao pamoja na kwamba nimejitenga niko kwangu majukumu yako palepale kama kijana anayetambua maisha ya familia zetu na hali ilivyo huko nyuma tutokapo.View attachment 2674132
View attachment 2674133
Mei 2022 niliongeza vyumba kama picha inavyoonekana, nimeendelea kupambana kadri niwezavyo ili nisije kuacha familia yangu ikihangaika. Bora wahangaikie chakula, mavazi na malazi lakini siyo wahangaikie chakula, makazi, mavazi na malazi vyote kwa pamoja itakuwa ni huzuni mno kwa usawa huu tulionao.

View attachment 2674149
Mwaka 2022 mwezi wa 8 nilipaua kama inavyoonekana hapo kwenye picha kwa uhalisia zaidi, hapo nikaanza kuvuta nguvu ili niweze kumalizia mambo mengine yaliyosalia kwa sababu kazi kubwa nimeimaliza ingawa finishing ni ngumu sana kama unahela za kuunga unga ila Mungu ni mwema.

View attachment 2674153
2023 mwezi 3 nilifikia hatua hii na Mungu ni mwema nimemaliza na kuweka SingBod kwa sasa.

Lengo langu halikuwa baya kuhusu uzi huu, ila nilikuwa nataka muone namna unavyoweza kujikwamua na wewe ili ufikie lengo walau hata kunusa nusa kiasi kwamba hutaweza kumlaumu mtu zaidi ya kusema asante kwa afya na maarifa ambayo unakuwa nayo mbeleni na hata kabla ya hapo.

Mungu aendelee kukusaidia wewe mpambanaji hakikisha hukai kwa lalamiko mimi nimpambanaji kwa hatua hiyo nimejinyima hata maisha nayoishi nimejinyima mno maana kwenye mambo ya kujirusha simo kabisa na mambo ya kuvua chupi niliacha kabisa baada ya kuona umri ukienda wakumlaumu hamna ni mimi mwenyewe ndio ntaonekana mjinga hivyo niliona kesho yangu haiko salama.

Hata hivyo kabla sijahitimisha makala hii ni kwamba hata kama utafanikiwa kufanya mambo yako nguzo kubwa ipo kwa mke ukimtumia hela ukakuta ametumia tofauti na maelekezo yako my friends 😄 🤣 jipigepige kifua sema Mungu kwanini umeyaruhusu haya. Yaani malengo lazima yatimie kwa kushirikiana kwa muda hata kama mtapishana ila hamtoki kwenye mstari wenu.

Wengi tunaanguka kwa sababu watu tunaowaamini ndio wanaoturudisha nyuma na kujikuta lawama zinakuwa nyingi mpaka wengine wanafikia kusema hataweza kuwa na mwanamke mwingine bora aishi peke yake maana unakuta mke kila siku yeye ni kuingizia hasara familia.

Amekopa mpaka kaweka rehani kitanda wanacholalia ila ukija kuangalia alichofanyia pesa aliyokopa hakuna hata cha maana na biashara haionekani.

View attachment 2674127

Credit: jumanne255.com

Ongera, umejitahidi sana. Sasa unaenda wapi na hiyo baiskeli?
 
Hongera sana mkuu. Wengine hatuna roho za kujenga cjui ni pepo gani hili... Shetan ashindwe kwa jina la yesu!
 
Hongera sana mkuu kwa hatua hiyo kubwa. Naamini utaleta changamoto kwa vijana wengine pia kufanya udhubutu kama uliofanya.

Usitishwe na 'mapovu' ya baadhi ya vijana wa jf maana walio wengi bado wanaishi kwa shemeji wakisubiri ajira. Kuna la kujifunza kwa mtu mwenye mtazamo chanya.
 
Back
Top Bottom