Nyumba ipi naweza kuikamilisha kwa 7M nikahamia kati ya hizi?

Shimo la choo la duara ukifanya mchezo 1.8M unailaza chini
 
Hiyo ya kwanza mkuu wasikutishe kabisa. Ingawa naona unaweza ukimaliza kabisa na mambo ya kupiga lipu, lakini angalau utakuwa unapiga ukiwa humo humo! Tena ijenge nyuma kabisa iwe kama banda la uwani ili ukipata pesa nzuri ndiyo ujenge mbele ile kubwa!
 
Ila ujenzi si lelemamaa mweeh[emoji848][emoji848]

Yamenikuta hadi nimefirisikaa
 
Ndg mleta mada , nakushauri fanya kile moyo wako umeamua, million 7 ni nyingi mno, lkn pia ni chache sana ukizitumia pasipo kuwa na akili, ni chagua ramani uipendayo, kisha jenga msingi na boma, chagua vyumba vya kuanzia maisha Paua, piga lipu, vilivyobaki utakarabati taratibu kadri upatavyo pesa.

Ujenzi unaumiza sana ukiwa na malengo ya harakaharaka kukamilisha jengo, ukienda taratibu hatua kwa hatua, mambo yanajipa yenyewe
 
Mkuu habari? Hakuna nyumba kati ya hizo mbili itakayokamilika kwa 7M nashauri kama umepata 7M unaweza kupata 7M nyingine. Kiwanja unacho anaza mdogo mdogo sema kipaumbele kisiwe kuhamia hivi karibuni.
 
Akitoka huko chini atakuja kuweka level ya msingi kwa kutumia mchanga, atapanga mawe ataweka DPC kisha BRC kabla ya jamvi.

Atamwaga jambi la 25C.
Tutafsirie hizo technical terms mkuu
 
Nyumba namba 1 unaweza kufikia sehem ya kukuruhusu kuishi ila finishing itakuwa bado ama utaifanya robo but unaeza kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…