Nyumba ipi naweza kuikamilisha kwa 7M nikahamia kati ya hizi?

Nyumba ipi naweza kuikamilisha kwa 7M nikahamia kati ya hizi?

Kwa hiyo bajeti na hilo lengo la kuhamia nakushauri ujenge ile ramani ya kwanza ila usijenge yote, ikate nusu kama inavyoonekeana kwenye picha niliyoambatanisha alafu unaacha matoleo utaendeleza kulingana na upatikanaji wa pesa kisha utamalizia na nyumba itakamilika
Kwa gharama za wapi ndugu, wakati maeneo karibu na mchanga roli la mchanga kubwa wanaita mende ukiwapa lak4, utapata mchanga wa kujenga hiyo nyumba ya 2 na unabaki, utafyatua matofali mwenyewe. Hapa itategemea kiwanja kipo wapi. Mleta mada usipoeleza site wapi, kila mtu atatoa ushauri wa pale anapoishi na utakuchanganya
 
Utabakiwa na 5.5M,masoni mpe 800000,cement mifuko 60,900000,mondo mm12 16@352000,maji laki 200000,mchanga laki 500000 ,kokoto laki 300000
 
Hiyo laki saba uweke hayo madirisha ,then utabakiwa na m 2
 
Tuseme ni bati 40*22500=900000,utabakiwa na 1.1,nunua mbao za 400000,mpe fundi 600000 akuezekee
 
Mtafute fundi achimbe msingi ,nunua kokoto kabla ya kuanzia na tofali chino anaanza na kazege ,SI lazima Sana uweke mondo,unaweza kuweka mondo baada ya kozi za msingi kukamilika,unapofunga beam,jamvi achana nalo ,piga ring beam kwenye msingi na linta,hata hiyo nyumba umepanga Haina jamvi!
 
Shida no mchoro wako ndio unatisha.

USHAURI:Jenga kwa umechopata

-Jenga Bila kuweka mkanda wa chini
Weka ratio kali tu
- Jenga Chumba na ukumbi tuuu
Laza bati Mfumo wa banda
  • Tumia bari nyeupe
  • Kibarua kaa mwenyewe.

Wiki Moja tu upo kwako,usitishwe
7m kwa banda tu inatosha, Finishing mbele ya safari.
 
Shida no mchoro wako ndio unatisha.

USHAURI:Jenga kwa umechopata

-Jenga Bila kuweka mkanda wa chini
Weka ratio kali tu
- Jenga Chumba na ukumbi tuuu
Laza bati Mfumo wa banda
  • Tumia bari nyeupe
  • Kibarua kaa mwenyewe.

Wiki Moja tu upo kwako,usitishwe
7m kwa banda tu inatosha, Finishing mbele ya safari.
Kwamba Kibarua ajilipe mwenyewe, daaah
 
Anza na chumba kimoja tu utakamilisha aka post.

Ogopa fundi akikwambia tuanze mengine tutajua mbele kwa mbele.
 
Kwanza kabisa picha linaanza, una jiko, vyoo na bafu ndani.
Halafu hiyo ramani haionyeshi septic tank, wala water tower.
HIVYO VITU VIWILI (SEPTIC TANK NA WATER TOWER/TANK) haviwezi kupungua 5m.
Tuwe tunaangalia ramani, halafu tujue kama imekamilika.
 
7m labda vyumba viwli vitakuwa vikali sana vya kisasa tena self

Vikiwa vitatu vitakuwa vya kawaida

Vikiwa vinne Hela ya Rangi utakosa[emoji1]

Vikiwa sita Hela ya Rangi, tiles, bati, grill utaikosa

Vikiwa Saba utaishia kwenye Renta

Vikiwa nane utaishia kozi 4.

Vikiwa Tisa utaishia msingi.

Vikiwa kumi utaishia kwenye tofali na mchanga tu site

Vikiwa 11 vitaishia kwenye karatasi

Vikiwa 12 vitaishia kichwani kwako.

Yote haya kwa 7m.tena ukiwa Dar[emoji1]
Vikiwa 13 ataishia bar[emoji38]
 
Back
Top Bottom