House4Sale Nyumba mbili (pamoja) zinauzwa na bank, Tshs.30 milioni, Kihonda, Morogoro

Hizo nyumba hata waniuzie laki tano tano sinunui ni kununua mikosi tu..
 
Dalali tapeli kaulizwa maswali magumu hadi kaamua kuingia mitini! hahaahaa Bongo sihami!!
Hizi sikukuu zina mambo! Hakuna tofauti na wale wa tuma kwa namba hii jina litakuja Hanuni Hacheki Umelizwa.
 
Ukiona hivyo kuna janjajanja nyingi ya kitapeli huenda ni white elephant hizo
 
.

ANGALIZO:
Malipo ya Dalali ni 10%
Kuona ni 100,000.
(Unalipa wewe MNUNUZI)

Tafadhali Wasiliana nami iwapo tu unaridhia taratibu zangu.

+255714591548

___________jj/mpg


Ukihitaji kukagua taarifa mapema tafadhali.
Si muda mrefu kuna mtu atajishika kichwa baada ya kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali
 
Dalali kaona mmeshavuruga dili lake
 
Kama wewe ni Mhitaji piga simu punguza kuandika Tamthilia na ujuaji katika vitu usivyovielewa.
huna ujualo ni ww ndie unaleta ujuaji kwa vitu usivyovijua vinafanyikaje..ww hiyo bei uliyotaja milion 30 kwa nyumba mbili nzuri kama hizo huoni mushkeli au lengo ni kuwapata wajinga wenye tamaa za haraka.! nyumba zilizo chini ya benki kuuzwa kwa order ya mahakama tu ikiwa sambamba na kuteuliwa kwa kampuni iliyosajiliwa na mahakama kufanya kazi za minada ndio itakayouza nyumba kwa niaba ya benki tena itauzwa kwa mnada wa wazi kwa wanunuzi kupandiana dau..ww uliona wapi benki wanatumia dalali uchwara wa mtaani asiye na vibali vya mahakama..kisheria benki hairuhusiwi kuuza nyumba bila kibali cha mahakama na mtu au kampuni lazima iwe imesajiliwa na ina vibali vyote kisheria kuendesha mnada..je,ww mleta uzi unatambulika kisheria na unavyo vibali kukuruhusu kufanya huo mnada.. je,unayo order ya mahakama na barua ya benki kukutambua ww kuuza hizo nyumba ambazo ni mali ya benki kwa sasa.? au ww dalali na mwenye nyumba mnataka kuuza nyumba ili kuiwahi benki alafu msala mnawaacha wengine si utapeli tu huo.!
 
Hizi nyumba labda wanilipe fedha wao,siwezi kununua nyumba za hovyo kwa hiyo hela.
 
Ahsante kwa madina safi kabisa.Huyu anayejiita dalali ana nyuzi za kutosha humu kuhusu uuzaji wa nyumba na majibu yake yamejaa nyodo nyingi . Hii ni red flag kwetu.Tuwe macho la sivyo tutapigwa.
 
%10? M 30? Mali ya bank? Nyumba ina deni inamaanisha dalali amewazunguka bank,, kwakuwa bank hawajui taratibu za kuuza nyumba za wadeni wao? Hapo Kuna mchezo Kati ya dalali na mwenye nyumba
Janja Janja
 
Acha utapeli hapa wewe... Umeambiwa ukweli unaleta ngonjera... Wapige wa huko huko Moro...
πŸ˜πŸ˜„πŸ˜πŸ˜πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜πŸ˜
 
Hiloooo tapeli linaona aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…