Nyumba ya aliyekuwa Rais wa Tanzania yageuzwa hoteli

Nyumba ya aliyekuwa Rais wa Tanzania yageuzwa hoteli

meanwhile jiji la dar linazidi kutapaka vituo vya mafuta vya kampuni ya lake. familia ya kikwete wanakula raha.
 
Tunachosikitika ni kwamba raisi anapostaafu hujengewa nyumba nyingine kwa pesa za umma. Wakati majumba wanayo mpaka mengine yanageuzwa mahoteli.

Do you follow me?.
Nakusoma vyema, lakini mwisho wa siku itabaki tu kuwa uzembe wa wananchi ambao hawaoni hili ni tatizo.

Kwa sasa kulalamika kwamba nyumba imefanywa hoteli haiwezi kuleta impact yeyote, ni sawa na kukamata upepo.
 
Ni huruma mno kaka hawa viongozi ni maskini wakutupwa kuliko sisi wananchi...angalia mtoto wa mwigulu anasoma shule ya Feza ambayo hawana walimu tena wanakaa tu chini pale...Abdul mtoto wa samia ni saidia tu wa ujenzi kule mvuti
MBONA SIWAELEWI, AU DUNIA IMEKUWA NYUMA GEUKA HALAFU MIMI SINA HABARI!
 
Ushasema ni hotel afu bado unapiga pic za wizi wizi

Toa pess ingia ndani agiza soda piga picha kwa amani
 
Chini ya uongozi wake akishirikiaa na wazir wa ujenzi wa wakati huo bwana John Pombe Magufuli waliuza nyumba 845 za serikali kwa vigogo wa serikali.
Hii ni case kabisa najua huko mbele wazalendo watakuja kuifufua tu siku moja
😆😆😆😆
 
NYUMBA YA MKAPA YAGEUZWA KUWA HOTELI?

Nyumba ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa iliyopo Obama Drive, Sea View. jijini Dar es Salaam ambayo geti lake huwa linafungwa imeonekana ikiwa geti wazi huku ikiwekwa mabango ya Protea Hotel. Hii ni ishara kuwa nyumba hii imegeuzwa hoteli. Ikumbukwe kuwa serikali ya Tanzania Huwa inawajengea nyumba za kifahari maraisi wastafu kwa vile Huwa hawana uwezo wa kujenga nyumba zao na vipato vyao ni vidogo. View attachment 3261124 imegeuzwa kuwa hoteli

View attachment 3261124
Da, so many memories here.

Mzee Mkapa alikuwa mserikali mpaka mwzani anakataza kunywa maji kabla ya kumaliza kula. Mimi sijazoea nilikuwa naona ajabu sana.

Kuna siku nilikuwa nampelekea mchizi wangu mzigo fulani hapo, nilikuwa natoka kazini na wenzangu.

Sasa mimi nikaona jambo la kawaida nampelekea mshkaji mzigo wake tu.Kumbe kwa wenzangu wakaona big deal.

Nikamwambia dereva wa ofisini a park gari hapo nje nimpelekee mshkaji mzigo wake.

Derava akapagawa sana anauliza "Hapa si kwa Mkapa hapa, unataka ni park gari hapa?" Nikamwambia ndiyo.

Aka park.

Hapo hapo wakatoka wale askari haraka sana wanatuambia ondoeni gari hapo. Hairuhusiwi ku park gari hapa.

Dereva aka park gari mbele kidogo.

Nikamwambia yule askari nina mzigo nimetumwa.

Nikaufikisha.

Nafikiri famikia itakuwa imeipangisha hiyo nyumba kwa sababu wao wanakaa nyumba aliyojengewa rais ya Masaki.
 
NYUMBA YA MKAPA YAGEUZWA KUWA HOTELI?

Nyumba ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa iliyopo Obama Drive, Sea View. jijini Dar es Salaam ambayo geti lake huwa linafungwa imeonekana ikiwa geti wazi huku ikiwekwa mabango ya Protea Hotel. Hii ni ishara kuwa nyumba hii imegeuzwa hoteli. Ikumbukwe kuwa serikali ya Tanzania Huwa inawajengea nyumba za kifahari maraisi wastafu kwa vile Huwa hawana uwezo wa kujenga nyumba zao na vipato vyao ni vidogo. View attachment 3261124 imegeuzwa kuwa hoteli

View attachment 3261124
Nyumba aliyojengewa mkapa na serikali ilo masaki na haijageuzwa hotel

Hii ni nyumba aliyokua nayo tangu enzi na enzi

Wabongo nongwa sana
 
Nyumba aliyojengewa mkapa na serikali ilo masaki na haijageuzwa hotel

Hii ni nyumba aliyokua nayo tangu enzi na enzi

Wabongo nongwa sana

kusema hii nyumba alikuwa nayo enzi na enzi Sio kweli. Mkapa hajui hata bei ya tofali la hiyo nyumba.

Hiyo nyumba ilikuwa mali ya serikali ilikuwa inatumika kama kota ya bosi wa TPA.

Mkapa alivyokuwa Rais ndipo alijiuzia ikawa mali yake binafsi
 
Kifo hiki bwana, yani Ben aliacha vyote hivi akalala mauti. Kweli kifo kiboko Mungu alituweza.
 
Back
Top Bottom