saidi kindole
JF-Expert Member
- Sep 21, 2012
- 310
- 792
Ni aibu kwa bunge badala ya kujadili bajeti ya nchi, linatumia siku mbili kujadili tukio la kuvamiwa Mbowe. Cha kusikitisha hawajadili namna ya kumsaidia mbunge mwenzao bali wanapiga majungu.
Jana Msukuma kasema Mbowe alikuwa anakunywa Konyagi Kubwa (Faru John) na ndio iliyopelekea kuanguka na kuvunjika. Ndugai kasema madaktari wake walimjulisha kuwa Mbowe alikua amelewa chakari.
Kibajaj akasema alianguka akiwa na mwanamke na mwanamke huyo alikimbia. Waitara amemtaja mwanamke huyo kwa jina bungeni. Yani majungu majungu tu.
Kama kuna utata kuhusu kuvamiwa kwa Mbowe, utata huo unapaswa kumalizwa na mambo mawili tu.
#Mosi; Mbowe ana walinzi wa aina mbili. Wa serikali (TISS) na wa chama (Red Brigade). Serikali ilimuondolea Mbowe walinzi mwezi uliopita kwa sababu ya issue ya Covid19 walipotoka bungeni.
Lakini hata baada ya kurudi bungeni hakurudishiwa ulinzi. Hapa kuna kitu hakiko sawa. Kwanini viongozi wengine walibaki na walinzi kama issue ni Covid19? Na kwanini Mbowe hakurudishiwa ulinzi hata baada ya kurudi bungeni?
Wanaohoji kuhusu ulinzi wa Mbowe wanapaswa kuhoji mambo mawili. Kwanini serikali haikumrudishia ulinzi baada ya kurudi bungeni kisha wahoji walinzi binafsi wa Mbowe (red brigade) walikua wapi wakati anavamiwa.
#Pili; Nyumba anayoishi Mbowe ina CCTV 24hrs. Kwnn picha za CCTV zisiwekwe hadharani? Kama alianguka ataonekana na kama alivamiwa ataonekana pia. Kwanini tunapoteza muda kusigana kwenye jambo ambalo ukweli wake ni rahisi tu kupatikana?
Nyumba anayoishi akiwa Dodoma (kama KUB) ni ya serikali with CCTV system. Hata wanaoaccess "control room" ni maafisa wa serikali. Kwanini serikali isitoe hizo picha zinazoonesha Mbowe akianguka?
Kwa ninavyoijua serikali ya CCM ingekua kweli Mbowe kaanguka usiku akiwa na mwanamke na "Faru John" mkononi, nina uhakika wangeprint hizo picha na kuzisambaza kuanzia Lupiro kule Ulanga hadi Yombo Buza kwa Abiola.
Lakini ukiona serikali inakomaa kuwa Mbowe alianguka, lakini haitaki kutoa picha za CCTV, halafu serikali hiyohiyo ilimuondolea ulinzi mwezi mmoja tu uliopita, lazima uhisi kuna kitu. WaTZ wa leo sio wajinga.!