Nyumba ya KUB Mbowe ina CCTV, zinaweza kutoa ushahidi kama alianguka au alivamiwa

Mbona povu jingi, kwani taarifa ya uchunguzi imetoka??

Mbona mna haraka subirini taarifa rasmi ya POLISI kuhusiana na tukio tajwa.

Yote tutayajua humu, acheni kuharibu upelelezi.
 
Siku Lissu anashambuliwa nyumba hiyo ilikuwa na CCTV na zilikuwa zinafanya kazi, baada ya shambulio ziliondolewa!. Kalemani was right kupinga kwasababu hizo CCTV cameras hakuziweka yeye!.
P
Maana yake wasiojulikana wanajulikana.
Asante P
 
SASA HAO WANAOSEMA ALIKUWA NA MWANAMKE NI KUWADHALILISHA TU MAMA ZETU. HALAFU WANAWAKE WA CCM WANACHEKA BADALA YA KUSIKITIKA KUDHALILISHWA. UKIWA CCM AKILI IPO CHOONI
 
Mleta mada umeweka uzi wa maana na maswali mengi mazuri.

Lakini maswali muhimu ya kujiuliza ni.
1. Chadema kinajua kuwa hawako vizuri na awamu ya tano , jee kwa nini hawawi wako very cautious.

2. Kiongozi wao Lissu kapigwa risasi kwenye mazingira kama hayo, wanayosema yamemkuta Mbowe. Jee wao kama chama kikubwa cha upinzani kwa nini hawakuchukua tahadhari zaidi ya kutegemea ya serekali tuu.

3. Tunajua chadema hawana imani na lolote watakalofanyiwa na serekali, hata mazuri yanayofanywa wao kama chama kikuu cha upinzani lazima wayapindishe. Jee inakuwajee wakaamini ulinzi wa serekali. Pili walinzi walioshaondolewa, waliweka utaratibu gani wa kumchunga kiongizi number 1 wachama chao. Jee hapo hauoni kuna ugoigoi wa usalama ndani ya chama.

4. Hizo cctv ndani ya nyumba, za serekali ziko kwa njee, chadema wana walinzi wao wanaowalipa, na wameweka cctv zao ndani na njee, haswa baada ya tukio la Lissu, kama ni kweli kavamiwa na wasiojulikana, na ushahidi wao wanao, kwa nini wasiuweke wazi, tukajionea uonevu wa serekali kama msemavyo. Hii inaelekea kama ule ushahidi wa bomu la Arusha ambao Mbowe alituambia anayo video ikionyesha polisi akirusha bomu, na mpaka leo ni miaka 6 hatujauona huo ushahidi.

5. Jee kama sio ukweli Mbowe alikuwa amelewa vibaya sana na alikuwa na mwanamke wa njee ya ndoa, basi hizo kelele zisingepungua , hatuzioni tena hizo kelele. Pili kwa nini kiongozi aliyevunjwa mguu na kujeruhiwa vibaya, anapelekwa dispensary kutibiwa baada ya kupelekwa hospitali,

Kuna jambo chadema haliko sawa.
 
Uchunguzi huru utafukua madudu yenu ya mipango ya nani apeperushe bendera ya chama. Jee kuna mikakati ya kumkata lissu asiwe mgombea . Jee kuna mkakati wa ushirikiano kati ya Chadema na ACT na mbiwe ameshakubaliana na zitto ndio awe mpeperusha bendera na Mbowe PM, na iwapo watabahatika kuunda serekali ya mseto, basi chadema watapewa wizara 3 muhimu.
 

Maswali uliyouliza hakika ni ya msingi. Bunge, Taasisi kubwa, haikupaswa na haipaswi kushabikia mambo ya udaku, yasiyokuwa na ushahidi usio na mashaka.

Labda kwa kuongezea, viongozi wa CHADEMA nao hawakupaswa kukurupuka kutangazia umma kuwa shambulio hilo ni la kisiasa kwa kuwa mazingira yake yanaibua maswali kadhaa kama ifuatavyo:-
1) Mbowe inadaiwa alishambuliwa usiku wa manane akiingia nyumbani kwake. Je, alikuwa anatoka wapi na walinzi wake walikuwa wapi?
2) Baada ya kushambuliwa alimtaarifu nani wakati majirani wamekuja kujua baadaye?
3) Kwa nini alikwenda hospitali ndogo, binafsi, badala ya kubwa ambazo yeye kama KUB angepata huduma stahiki ya madaraka aliyo nayo (VIP)?
4) Kwa kuwa ni shambulio na kujeruhiwa, kiutaratibu alipaswa kupata PF3 ya Polisi kabla ya kutibiwa au hata wakati anaendelea na matibabu, kwa ajili ya upelelezi na hatimaye mashitaka kwa waliomshambulia?
5) Daktari aliyempa huduma ya tiba alithibitisha kuwa alikamilisha na Mbowe angerejea katika hali yake njema baada ya muda mfupi. Kwa nini CHADEMA iliamua kumpeleka Dar?
6) Inatia shaka ya kumpeleka hospitali binafsi Dar wakati Muhimbili imeimarishwa na ndiyo hospitali kubwa ya rufaa hapa nchini?

Kwa kuwa suala liko mikononi mwa Polisi kwa uchunguzi, kwa sababu TU ya wadhifa wake, kwa maana hakuna jalada la malalamiko, tusubiri matokeo ya uchunguzi huo, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa majeraha aliyopata, kupelekea kupelekwa Dar kwa ndege ya kukodi, tena kwenye hospitali binafsi. Ikumbukwe kuwa gharama zote hizo zinalipwa kwa pesa ya mlipa kodi na chama chenye viongozi, akiwemo Mbowe mwenyewe, ambao huishutumu Serikali, hasa Rais, kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, na hata pale zinapotumika kwa miradi ya maendeleo.
 
Ndugu yangu Kwa ulimwengu wa leo kungangania CCTV ni kushindwa kuukubali ukweli kwamba hata wahalifu wanaenda na technology hiyo.
Kama serikali walitaka kufanya Yao lazima washughulikie hizo CCTV Kwanza
Kama ni Mbowe ndio kalewa akataka kuipakazia Serikali basi lazima acheze na CCTV Kwanza.
Mtu anayehoji CCTV basi anaowaona wahalifu hawana akili au yeye ndio Hana akili Kwa kufikiri TISS wataiacha au Mbowe ni mjinga alewe alafu achaache ushahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…