Tetesi: Nyumba ya mjane wa Balozi John Rupia Katibu Mkuu Kiongozi (mstaafu) yadaiwa kupigwa mnada

Tetesi: Nyumba ya mjane wa Balozi John Rupia Katibu Mkuu Kiongozi (mstaafu) yadaiwa kupigwa mnada

Hizi ni nyumba za serikali walizouziana Oysterbay ?

Kama ni hivyo je ziliwekewa dhamana ya mkopo benki kwa gharama mara 100 ya kiasi walicholipa viongozi wa serikali waliouziwa ?

Sina shaka kadhia hii waliokaribu na familia ya Rupia watalimaliza

TOKA MAKTABA :

Waziri asema, "Natoa mwezi mmoja..." kwa walioko kwenye nyumba za serikali

Published on Thursday, March 10, 2016

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewapa mwezi mmoja wale wote wanaodaiwa kutokana na kukopa nyumba za Serikali walipe mara moja vinginevyo wazisalimishe serikalini.

Mbali na hilo, ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuzingatia thamani ya fedha kwa kila mradi wa ujenzi wa nyumba wanaoutekeleza nchini.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa wafanyakazi wa wizara hiyo, huku akionya iwapo hawatarejesha fedha hizo atawatangaza mmoja mmoja katika vyombo vya habari kabla ya kuwanyang’anya.

“Kama unajijua umekopa nyumba ya Serikali na umeshindwa kuilipia ndani ya mwezi huu, ondoka mara moja katika makazi hayo maana sitakuwa na muda wa kukusikiliza. Tunahitaji fedha ili ziweze kufanya shughuli nyingine za kiuchumi,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema zipo fedha nyingi ambazo bado hazijarejeshwa kupitia kwa wakopaji hao wa nyumba huku serikali ikishindwa kufanya shughuli nyingine za kuwajengea wananchi miundombinu bora na ya kisasa.

Profesa Mbarawa alisema kodi zinazokusanywa hazitoshi kuboresha miundombinu kwa ubora unaotakiwa, hivyo kila kiongozi anatakiwa kusimamia majukumu yake ili zipatikane fedha za kujenga nyumba nyingine bora.

Alimwagiza Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga kuhakikisha wapangaji wote wanaoishi kwenye nyumba za wakala huo wanalipa kodi zote kwa wakati na watakaoshindwa wahame mara moja.

“Natoa mwezi mmoja kwa watumishi ambao hawajalipa watafute sehemu nyingine ya kukaa, ili wakala apangishe nyumba hizo kwa anaeweza kulipa kwa wakati,” alisema Profesa Mbarawa.

Uuzaji wa nyumba za Serikali ulitekelezwa katika uongozi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na nyumba zaidi ya 8,000 ziliuzwa, baadhi zikiwa zimejengwa katika maeneo nyeti.
Ilidaiwa Rais Dk. John Magufuli, wakati akiwa Waziri wa Ujenzi aliingilia mchakato wa uuzaji wa nyumba hizo ambao unatajwa ulipaswa kusimamiwa moja kwa moja na TBA, jambo ambalo lilizugua gumzo.

Uuzwaji huo wa nyumba hizo, unalalamikiwa na wananchi hadi leo kutokana na mchakato huo kuhusisha nyumba za Serikali zilizokuwa katika maeneo nyeti na kusababisha watumishi wengi wa Serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi kuishi hotelini.

Kilio hicho cha wananchi kilikwenda mbali zaidi kwa kuweka matumaini makubwa kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani mwaka 2005 huenda angeweza kubatilisha uamuzi wa mtangulizi wake kwa kuzirudisha nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa bei ya kutupwa.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa mamlaka ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kukarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa serikali na si Waziri wa Ujenzi wa wakati huo.

Sheria hiyo, inaipa mamlaka ya kipekee TBA ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.
Kwa sheria hiyo, waziri mwenye dhamana anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Katika mauzo hayo ya nyumba, Serikali ilitarajia kupata Sh 60,016,556,439.00, lakini taarifa zikionyesha ilipata Sh 22,684,108,115.08.

Miongoni mwa nyumba zinazomilikiwa na Serikali hadi sasa ni 1,098 zinazosimamiwa na TBA, kati ya hizo, 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, 675 kama tied quarters, 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 kama karakana na bohari.

Katika bajeti ya mwaka 2010/2011, Wizara ya Ujenzi iliwasilisha bajeti yake bungeni mjini Dodoma na kueleza inatarajia kutumia takriban Sh bilioni 5.7 kujenga nyumba mpya ili kuokoa mamilioni yanayotumika kuwalipia kodi watumishi wanaolazimika kukaa hotelini kwa kukosa nyumba.

Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha kilichotengwa wakati huo kilitajwa kuwa pungufu ikilinganishwa na kile kilichotengwa awali, katika bajeti iliyotangulia ya 2009/2010, Sh bilioni 11.4 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo wa nyumba
 
Shukran lakini picha sizioni mie.
308750308_1265103534237022_2390742274289806053_n.jpg
 
Ukijibiwa uni tag

Hizi familia zetu akishaondoka mzee

Watoto wao ni kula tu hawazalishi

Mwishowe wao ni kuuza Mali, wanatumia

Ova
Ndio maana wazungu huwa wanataka watoto wao watafute pesa zao sio kusubiri au kuzitumia za wazazi wao kama wameshamaliza masomo yao !!
 
Biz nyingi hapa bongo zinakuzwa na pesa za rushwa, wizi na udokozi kwenye ofisi za umma. Ndiyo maana wengi wakitumbuliwa unashangaa na biz zao zinakufa.

Enzi za jiwe supermarkets nyingi zilikufa kwasabb tu mmiliki wake katumbuliwa. You can imagine, kutumbuliwa na biz kufa, wapi na wapi?
Kuchota ni rahisi lakini kudunduliza ni kazi Kweli kweli !
 
Ndio maana wazungu huwa wanataka watoto wao watafute pesa zao sio kusubiri au kuzitumia za wazazi wao kama wameshamaliza masomo yao !!
Familia nyingi zilizotisha zamani

Ukiangalia sahv wameporomoka

Wazee wakitoka toka watoto sasa

Wao hawazalisha wanatumia kile alichotafuta mzee,wanatumia tu
Bata,safari za ulaya ,dubai haziishi
Mwisho wa siku cash yote kwishney
Zinabaki properties ,hapo sasa kwenye properties ni kuuza au kuingia mikopo

Mtoto ni lazima afanye kazi ili ajue pesa zinapatikanaje sio akae kama yai !!
 
Dawa ya deni ni kulipa

Huko nyumba ya mkono ilipigwa mnada...

Nyumba ya mahiga nayo ilipigwa mnada

Tukirudi kwenye Mali za wakina rupia,sawa wana Mali ongezea na eneo la wazo wanapochimba kokoto
Je nje ya properties wana biashara gani ambayo mpaka sasa ipo???

Je wana kiwanda nk ..?

Ova
Hizi ni 1st class families, hawahitaji kufanya biashara zozote, au kumiliki viwanda, just prime properties, shares, stocks and bonds.
P
 
Kama ilitumika kama collateral bank, na wakashindwa kulipa mkopo na mama kakubali iuzwe kwa kusaini documents zote, haina tatizo, tatizo ni ww uliyeleta habari kuwa sijui balozi, mara Rupia aliwahi kuwa KMK, sijui mjane wake nyumba inauzwa na bank, hivi ulijua bank watauza tu bila kufuata taratibu zote za kisheria hatua kwa hatua?

Hapo kila step imefuatwa na ww umeleta habari hii ukitaka kuonyesha bank inaonea au ni kama unataka serikali isaidie, hilo halipo, bank haijui ww ni mjane, KMK mstaafu, si ulienda kukopa na kukubali hiyo nyumba iwe kama collateral, na ukishindwa kulipa, basi iuzwe na bank..

So hakuna tatizo kabisa, iuzwe tu na watu wengine tununue na Rupia wana fedha nyingi, kwao hiyo ni asset ndogo sana
 
Na kichwani ziwemo lakini !!
Hata kichwani ukiwa zero brain, kama baba amefanya the right investment kwenye properties, shares, stocks and bonds, watoto wanakula tuu dividends na kuishi maisha mazuri for the rest of their lives.

Hata hiyo nyumba inayouzwa, inauzwa tuu kwasababu something went wrong somewhere, it was earmarked for a huge investment kwasababu nyumba za kuishi wanazo plenty tena prime areas lakini Balozi alikubali kuishi hapo kwenye a humble house for a reason!, nalijua jumba lao la masaki, ni usipime!.
P
 
Mkuu peno hasegawa, asante kwa taarifa hii.

Nyumba yoyote inapopigwa mnada maana yake ni imetumika kama collateral for loan.

Kama nyumba hiyo ni matrimonial home, haikubaliki as a collateral mpaka both spouses wasaini.

Mke kama ulisaini nyumba itumike as collateral, mume akachukulia mkopo, baadae mume akafa bila kuulipa huo mkopo, kifo cha mume hakifuti lile deni la ule mkopo, hivyo mkopo lazima ulipwe!. Ukishindwa kulipa, ujane sio an excuse kuizuia bank to recover its debts.

Huu ni mfano mzuri wa kuwafundisha Watanzania kuweka bima, kuna mpaka bima za mikopo, ukifa kabla hujamaliza kulipa mkopo, bima ina take over na kukulipia!.

Rupia ni among the top ten giant families zenye lots of properties jijini Dar es Salaam!. Yale maghorofa yote matatu pale Uhuru Roundabout ni ya baba yao Mzee John Rupia, ambapo wakati wa utaifishaji hayo hayakuguswa!.

Hivyo hilo la hii nyumba ni dogo tuu!.
Pole Mama Anna, hili ni dogo tuu kama upepo na litapita tuu!.
P
I salute you for this!

A well informed citizen our state ever had!

"Walipe tu hamna Namna"
 
Na kichwani ziwemo lakini !!
Hata kichwani ukiwa zero brain, kama baba amefanya the right investment kwenye properties, shares, stocks and bonds, watoto wanakula tuu dividends na kuishi maisha mazuri for the rest of their lives.

Hata hiyo nyumba inayouzwa, inauzwa tuu kwasababu something went wrong somewhere, it was earmarked for a huge investment kwasababu nyumba za kuishi wanazo plenty tena prime areas lakini Balozi alikubali kuishi hapo kwenye a humble house for a reason!, nalijua jumba lao la masaki, ni usipime!.
Kama ilitumika kama collateral bank, na wakashindwa kulipa mkopo na mama kakubali iuzwe kwa kusaini documents zote, haina tatizo, tatizo ni ww uliyeleta habari kuwa sijui balozi, mara Rupia aliwahi kuwa KMK, sijui mjane wake nyumba inauzwa na bank, hivi ulijua bank watauza tu bila kufuata taratibu zote za kisheria hatua kwa hatua?

Hapo kila step imefuatwa na ww umeleta habari hii ukitaka kuonyesha bank inaonea au ni kama unataka serikali isaidie, hilo halipo, bank haijui ww ni mjane, KMK mstaafu, si ulienda kukopa na kukubali hiyo nyumba iwe kama collateral, na ukishindwa kulipa, basi iuzwe na bank..

So hakuna tatizo kabisa, iuzwe tu na watu wengine tununue na Rupia wana fedha nyingi, kwao hiyo ni asset ndogo sana
Hii taarifa ni marketing tricks kuufanya mnada wa hiyo nyumba kugeuka an article of ostentation hivyo to fetch a very high price!. Mtu kama the King Maker anaweza kutia team ili kununua nyumba ya Rupia, kama ule mnada wa mahekalu ya Lugumi yaliyo minus Dr. Shika!, mwisho wa siku ni Lugumi kazinunua mwenyewe nyumba zake na sasa anaendelea kuishi mwenyewe!.
P
 
Back
Top Bottom