Nyumba yetu inazidi. Rais onyesha uwepo wako, Uwezo Wako Anza na Wale Marrionates Wote Wawili Pale Wapumzishe. The Drama King wa Pinga Chanjo Apuuzwe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa huja na zile makala zangu Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa na gazeti la Nipashe la kila siku za Jumapili.

Wajameni, ni mimi tuu au na wengine, naona kama

Nyumba yetu inazidi makelele, jee tumshinikize Mama aonyeshe uwepo wake, kwa kuonyesha uwezo wake kuwadhibiti na kuwatuliza hawa watoto wake wasio na adabu, wanaoparurana mchana kweupe na Mama yupo anawaangalia tuu?!. Mama, hata kama mwanzo alikuwepo baba mkali, watoto wakawa na adabu kwa kumuogopa baba, sasa baba hayupo, na wewe ni mpole sio kama baba, hizi kele za watoto wako, ni ukosefu wa nidhamu, wengine wamefikia kukudharau wazi wazi, hata kama wewe ni mpole vipi, angalau anza kuonyesha uwepo wako na uwezo wako kuidhibiti nyumba yako, watoto kwa kuwaadabisha watoto wako, wawe na adabu, anza na wale marrionates wako wote wawili uliowakuta pale mahali, na ukawaacha na kuamua kuendelea nao, wapumzishe, au vinginevyo na wewe kama unapenda ze comedy, then tuendelee nao. Na yule, Kibwetere, "The Drama King", wa "Pinga Pinga Chanjo" yeye apuuzwe tuu!.​


Angalizo
JF ilipoanzishwa ilitarajiwa iwe ni home for the Great Thinkers, (GT) na great minds to discuss ideas.

Ila ikajikuta kwenye society kuna simple minds ambao ndio wengi, wata discuss people, kuna ordinary minds wata discuss events, na kuna great minds ambao ni wachache, hawa wata discuss ideas.

Hili ni bandiko kwa ajili ya great minds, hatujadili watu, wala matukio, tunajadili ideas, hivyo hakuna jina lolote la mtu yoyote litatajwa humu, nakuomba na wewe, mchangiaji, jitahidi usitaje jina la mtu yoyote.

Mimi Sio Great Thinker
Japo mimi sio great thinker, lakini naweza kuandika na kufikisha ujumbe maalum kwa hao ma great thinkers. Kwenye bandiko hili nimesema Marrionates tuu bila kuwataja, wala pale wapi au Kibwetere drama King bila kumtaja ni nani, hivyo uwezo wako kubaini hao marrionates na Kibwetere, ndio mwanzo wa safari ya wewe pia kuwa a GT. Kwa wasiopenda story ndefu, unaweza kuishia hapa...
Mama Onyesha Uwepo Wako, Onyesha Uwezo, Pumzisha Baadhi ya Comedians Uliowakuta.
Ndio maana ninashauri ili kuimalizia all this bickering going on kuhusu chanjo ya Corona, kwanza hawa marrionates wote wawili pale mahali, despite the fact, they are very good dances, ambao wanadance well with every changing beats, wapumzishwe. Kuna vitu unaweza kutumia dramas na comedy kuhamasisha, waachiwe dramatist na comedians, and not politicians. Kitendo cha comedians cum politicians wa marrionates type who can dance every beats and changes with every tune, kuiifanya hii chanjo kuonekana kama ni drama fulani au ni comedy fulani. Chanjo ya Corona ni something very serious na kinahitaji some very serious people kumsaidia CinC kuhamasisha watu wachanje sio hao comedians wote wawili hapo, Mama kwanza onyesha uwezo kuwa you are very serious and no nonsense lady kwa kuwaweka pembeni, choose some serious people, hawa comedians aliwarithi achana nao, watakuaibisha!.

Mama Onyesha Uwepo Wako, Onyesha Uwezo, Usiruhusu Kudharauliwa na Wadharau Wanawake!.
Na mwisho ni yule drama king aliyepewa kichwa na naniliu, sasa masikio yamezidi kichwa, analeta zile dharura za Kisukuma kudharau wanawake, ameonyesha dharau kubwa kwako na kwa mteule wako!. Amefikia kulitukana, na kulidhalilisha kabila lote zima kisa tuu ametofautiana na shemeji yake. Huyo ni attention seeker, kadri anavyo shughulikiwa ndio kwanza mnampa umaarufu. Sishauri ashughulikiwe kikamilifu kwa ule mtindo wa kilisulisu, zikimkosa mbili mtu unatoa maelezo!. Dawa ya kuwashughulikia attention seekers kama hawa ni kuwa ignore, just scrap then ile jeuri ya kubebwa na homeboy wake, reduce then to nothing as an ordinary men, abaki kuwachunga kondoo wake kwa kuwahubiria tuu neno la Mungu pale mimbarini kwake, na sio kuwahutubia Watanzania kila Jumapili akitokea mimbarini kwake. Dini zinafundisha mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na mpeni Kaizari yaliyo ya Kaizari, mimbari iwe ni kwa yaliyo ya Kimungu tuu, akifanya ya Kaisari mimbarini kwa yaliyo ya Kimungu, then ni Mungu mwenyewe utamshughulikia kwa kutumia mimbari yake kufanya ya Kaisari. Chanjo ni ya Kaizari.

Jumatatu Njema.

Paskali
 

Nashangazwa sana na watu naowategemea kama ww yan unataka kutuambia shida unayo iona ww ni hao watu tu na sio izi toso
Ni nan ataeweza kutupigia kelele haya maumivu ya tozo hao unao wategemea kupitia hii platfom ilitakiwa wakiingia bas wakute malalamiko ya tozo na sio mambo haya ya ajira za wanasiasa
 
Kinachouma zaidi licha kulipa Tozo na Kodi bado kuna Mbwa wanatufanyia mambo ya ajabu ajabu.

Tunawalipa mishahara ya Ubunge kwa Tozo zetu.Halafu wanachekewa tu.

Tupie kelele izi tozo tupigiwe au tusemewe na hawa kina pasco kelele za tozo vipato havijaogezeka ila tozo ndio zipo juu
 
Kuna namna ya ukweli, lakini alitakiwa afute kila asiekuwa wake na aweke wake, kwa ujumla sio hao wawili tu Kuna wengi walitakiwa mpaka Sasa wawe wamepmzika Ila ndio hivyo hatujui lengo la kuwaacha hata Sasa❣️
Kuwafuta kazi hao wakat ulifanya nao kazi ukiwa naibu Raisi πŸ˜ŠπŸ˜€ Yani kimsingi hayo mashambulizi ni kuonyesha kuwa Serikali iliyopo madarakani ni Sawa na iliyopita so inatakiwa iondoke waje wapya kuanzia Raisi mpak mjumbe wa nyumba kumi
 
Kuna namna ya ukweli, lakini alitakiwa afute kila asiekuwa wake na aweke wake, kwa ujumla sio hao wawili tu Kuna wengi walitakiwa mpaka Sasa wawe wamepmzika Ila ndio hivyo hatujui lengo la kuwaacha hata Sasa❣️
Wakipumzika wengine atawatoa wapi?

Wabunge wetu ndio hawa akina babu Tale Kinanasi, Kigwangalla, Tabasamu, Kibajaj yaani wote ni full comedy!
 
Kwanini huyo Drama King apuuzwe? nae anatakiwa kushughulikiwa ili iwe fundisho kwa wengine wanaopingana na maamuzi ya chama chao kwa public.

Suala la kuwaondoa hao wawili na kuwaacha wengine ambao nao tumeanza kuwaona wakivaa barakoa, na kusisitiza mbinu za kisayansi zitumike wakati hapo kabla nao walikuwa wapiga nyungu kwa mbwembwe utakuwa ni uonevu.

Kinachogomba hapa kwa hao "marrionates" kuonekana hawafai ni kwasababu wamebebeshwa mzigo wa kuongoza hiyo wizara, sababu naamini hata kama wasingekuwa wao, provided mama bado anaendelea nao, basi hata kama wangekuwepo wengine kwenye hiyo wizara nao wangeonekana hawafai.

Hapa ndio maana hata mama mwenye nyumba anaogopa kuwashughulikia, kwa sababu ukiangalia kwa undani hata yeye ni sehemu ya tatizo, kwani hakuna rekodi yoyote inayoonesha alipinga nyungu wakati wa mwendazake, kukaa kimya maana yake nae alikubali akiwa kama msaidizi.

Hapo ukiangalia kwa makini utangundua hii serikali yote ni fake, kwasababu wote wamebadilika misimamo yao wakti hapo kabla wote walikuwa na msimamo tofauti na walionao sasa, so kuliko kuwaondoa hao wawili pekee, kwangu naona kama mama hawezi ku step down, basi atleast cabinet yote ivunjwe aanze upya.
 
Wakipumzika wengine atawatoa wapi?

Wabunge wetu ndio hawa akina babu Tale Kinanasi, Kigwangalla, Tabasamu, Kibajaj yaani wote ni full comedy!
Ni kweli mkuu Ila kwenye zile nafasi zake kumi angevuta watu wa maana na kuwapa nafasi hizo Kama alivyofanya mtangulizi wake, siamini kabisa Kama angekosa watu wapo wengi mno sema timu ya ushauri labda sijui ilikula maharage ya wapi yalee
 
Ni kweli mkuu Ila kwenye zile nafasi zake kumi angevuta watu wa maana na kuwapa nafasi hizo Kama alivyofanya mtangulizi wake, siamini kabisa Kama angekosa watu wapo wengi mno sema timu ya ushauri labda sijui ilikula maharage ya wapi yalee
Zile nafasi 10 zilishajazwa na mwendazake!
 
Sense of maturity...
Kukiri kosa na kukubali mitazamo ya wengine katika kujenga sio udhaifu.
Mama akubali tulikosea apige chini au wao Kama waungwana wajiwajibishe kutokana na kauli na misimamo yao ya awali tuanze upya, maana ni hatari mpaka sasa karibu wiki ya tatu hatujaweza kufikia watu 500k waliopatiwa chanjo ukilinganisha na idadi ya watanzania karibu 60m.
Kuongeza nguvu kwenye kampeni na elimu ya hatua za kujikinga na chanjo kwa kutumia media na vyombo tofauti vya mawasiliano hasa social media.
Kiundwe kikosi kazi kujibu hoja na changamoto mbalimbali zinazotokana na chanjo kitaalamu sio kwa brabra inaweza kujumuisha watu kutoka sekta tofauti tofauti ila hasa wataalamu wa afya.
Kuunganisha taifa kuondoa itikadi, mitazamo,milengo au mawazo kutokana na dini, siasa au makundi tofauti katika kupambana na kuelimishana kuhusu covid na masuala mengine yenye maslahi ya kitaifa
 
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒβœŒοΈβœŒοΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…