Nyumba yetu inazidi. Rais onyesha uwepo wako, Uwezo Wako Anza na Wale Marrionates Wote Wawili Pale Wapumzishe. The Drama King wa Pinga Chanjo Apuuzwe

Nyumba yetu inazidi. Rais onyesha uwepo wako, Uwezo Wako Anza na Wale Marrionates Wote Wawili Pale Wapumzishe. The Drama King wa Pinga Chanjo Apuuzwe

Ni kweli mkuu Ila kwenye zile nafasi zake kumi angevuta watu wa maana na kuwapa nafasi hizo Kama alivyofanya mtangulizi wake, siamini kabisa Kama angekosa watu wapo wengi mno sema timu ya ushauri labda sijui ilikula maharage ya wapi yalee
Kwenye zile nafasi 10 unajua zimebaki ngapi kukamilisha?
 
Naam
Wanabodi,

Wajameni, ni mimi tuu au na wengine, naona kama

Nyumba yetu inazidi makelele, jee tumshinikize Mama aonyeshe uwepo wake, kwa kuonyesha uwezo wake kuwadhibiti na kuwatuliza hawa watoto wake wasio na adabu, wanaoparurana mchana kweupe na Mama yupo anawaangalia tuu?!. Mama eeh, anza na wale marrionates wako wote wawili pale mahali, wapumzishe. The Drama King, "Pinga Pinga Chanjo" Apuuzwe tuu.​

Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa huja na zile makala zangu kwa maslahi ya Taifa.

Angalizo
JF ilipoanzishwa ilitarajiwa iwe ni home for the great thinkers, na great minds to discuss ideas.

Ila ikajikuta kwenye society kuna simple minds ambao ndio wengi, wata discuss people, kuna ordinary minds wata discuss events, na kuna great minds ambao ni wachache, hawa wata discuss ideas.

Hili ni bandiko kwa ajili ya great minds, hatujadili watu, wala matukio, tunajadili ideas, hivyo hakuna jina la mtu yoyote litatajwa humu, nakuomba na wewe usitaje jina la mtu yoyote.

Japo mimi sio great thinker, lakini naweza kuandika na kufikisha ujumbe maalum kwa hao great thinkers. Kwenye bandiko hili nimesema Marrionates tuu bila kuwataja, wala pale wapi au drama King.

Kuna nyumba baba na mama ni wakali, sasa siku ukisikia watoto wanapiga makelele huku wanatukanana, then ujue wazazi wamesafiri, watoto wamebaki na house girl, hivyo wanamdharau!, wanapiga makelele kama nyumba haina wazazi.

Dunia nzima sasa iko kwenye vita vya Corona, mpaka ugonjwa wa Corona, bado hauna kinga, wala tiba, kama ulivyo ugonjwa wa ukimwi, ila ukigundulika mapema kuwa umepata maambukizi virusi vya ukimwi, na kabla hujaanza kuathirika, ukitumia vidonge vya ARV, uta fubaza virusi hivyo, hivyo kuvizuia visikuathiri, na ukizingatia masharti, utaendelea kuishi kwa muda mrefu.

Tangu mtu anapoambukizwa virusi vya ukimwi, kwanza unachukua muda mrefu kugundua, na kuna wengine wao ni ma carriers tuu wa virusi hivi wakivibeba kwenye miili yao, na kuwasambazia wengine lakini wao hawaathiriki. Tangu virus hivyo vya HIV kukuingia hadi kupata ukimwi, sometimes takes ages. Na hata ukiwa na ukimwi, na ukaanza kuugua, sometimes you take ages hadi kufa.

Virusi vya ukimwi vinashambulia mfumo wa kinga mwilini, hivyo kufa ni taratibu, lakini virusi vya Corona, vinashambulia mfumo wa upumuaji, usipo wahiwa hospitali, kifo ni fasta!. Mtu mlikuwa nae jana tuu mkila na kucheka nae, kesho yake unaambiwa kafa!. Lazima utashituka na kupingwa butwaa, bumbu wazi.

Kinga pekee ya uhakika ya ukimwi ni kuzuia ukimwi usikupate, na kinga pekee ya uhakika ya Corona ni kuzuia Corona isikupate.

Katika kukabiliana na janga la Corona, sasa kumepatikana chanjo ya Corona, hii chanjo sio tiba na sio kinga ya asilimia 100% kwa 100% kama chanjo ya ndui, polio na pepopunda ambazo zinachomwa kwa watoto wote dunia nzima. Chanjo ya Corona ni kujikinga wewe ili hata ikitokea ukapata maambukizi ya virusi vya Corona, hiyo chanjo mwilini mwako itakusaidia kwa chanjo hiyo kuuwezesha mwili wako kutengeneza kinga ya kivikabili virusi hivyo.

Hivyo Corona ni vita na mapambano ya vita hii yanaongozwa na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yetu, huku akisaidiwa kisiasa na viongozi wakuu wote, lakini kiutendaji na utekelezaji akisaidiwa na makamanda wawili fulani, Waziri na Naibu Waziri.

Kwa vile vita hii alipoingia, Taifa lilikuwa chini ya CinC mwingine ambaye hakuamini kwenye chanzo. Wale makamanda wasaidizi wawili, waliunga mkono msimamo wa Amiri jeshi wa wakati huo na kuwaaminisha Watanzania, jinsi chanjo hazifai na kuzibeza kwa sauti kubwa tena hadi kuongoza kwa mifano jinsi ya kupiga nyungu kwa mtindo wa ku dramatize.

Sasa tuna CinC mwingine, anayeamini kwenye chanjo, ilikuwa ni busara ya kawaida tuu, wale wasaidizi wawili walio ibeza chanjo, wangepumzishwa, na kuteuliwa wasaidizi wengine wawili kuitetea chanjo.

Kitendo cha wasaidizi wale wale walio icheza ile ngoma ya mpiga ngoma aliyetangulia na waliowaaminisha Watanzania kuwa chanjo hazufai, sasa baada ya kuingia kwa mpiga ngoma mpya, amebadili beat na tune, halafu wacheza ngoma ni wale wale, dancing to the new tune and new beat with dramatising kuwa chanjo ni nzuri, haijakaa poa!.

Ndio maana ninashauri ili kuimalizia all this bickering going on kuhusu chanjo ya Corona, kwanza hawa marrionates wote wawili pale mahali, despite the fact, they are very good dances, ambao wanadance well with every changing beats, wapumzishwe. Kuna vitu unaweza kutumia dramas na comedy kuhamasisha, waachiwe dramatist na comedians, and not politicians. Kitendo cha comedians cum politicians wa marrionates type who can dance every beats and changes with every tune, kuiifanya hii chanjo kuonekana kama ni drama fulani au ni comedy fulani. Chanjo ya Corona ni something very serious na kinahitaji some very serious people kumsaidia CinC kuhamasisha watu wachanje sio hao comedians wote wawili hapo, Mama kwanza onyesha uwezo kuwa you are very serious and no nonsense lady kwa kuwaweka pembeni, choose some serious people, hawa comedians aliwarithi achana nao, watakuaibisha!.

Na mwisho ni yule drama king aliyepewa kichwa na naniliu, sasa masikio yamezidi kichwa, analeta zile dharura za Kisukuma kudharau wanawake, ameonyesha dharau kubwa kwako na kwa mteule wako!. Amefikia kulitukana, na kulidhalilisha kabila lote zima kisa tuu tumetofautiana na shemeji yake. Huyo ni attention seeker, kadri anavyo shughulikiwa ndio kwanza mnampa umaarufu. Sishauri ashughulikiwe kikamilifu kwa ule mtindo wa kilisulisu, zikimkosa mbili mtu unatoa maelezo!. Dawa ya kuwashughulikia attention seekers ni kuwa ignore, just scrap him ile jeuri ya kubebwa na homeboy wake, reduce him to an ordinary man, abaki kuwahubiria tuu neno la Mungu na sio kuwahutubia Watanzania kila Jumapili akitokea mimbarini kwake, mimbari iwe ni kwa yaliyo ya Kimungu, akifanya ya Kaisari mimbarini kwa yaliyo ya Kimungu, then ni Mungu mwenyewe utamshughulikia kwa kutumia mimbari yake kufanya ya Kaisari.

Jumatatu Njema.

Paskali
 
Rais ana mamlaka ya kumwondoa Waziri wa afya na kuteua mwingine. Pia Rais ni Mwenyekiti wa chama chake, akiwa kama Mwenyekiti anayo mamlaka ya kuufuta uanachama wa mwanachama yeyote hata kama mwanachama huyo ni Mbunge.

Nashauri ili nidhamu irudi Serikalini, Madam President atumie rungu lake kwa hao wawili wanaosigana hadharani.

Madam akiendelea kukaa kimya sisi wenye akili zetu tutamwona ni kama mtu aliyeshindwa ku exercise her duty calls.
 
Based on opinion by the majority. Madam anapaswa kufumua marionattes wote aliowakuta ambao hakuwatea yeye. Ni angevunja baraza la mawaziri akaweka wapya, Vitengo vingine vyote hata kila cha wasiojulikana kinahitaji new commander aliyelelewa ndani ya mfumo wao wenyewe.

Kuweka marionattes wapya kutasaidia utiifu, Mama lazima aonyeshe anajali uwajibikaji kama mtu hawajibiki asisubiri ajirekebishe atolewe tuna watu milioni 60 kweli replacement inakosekana.

Hii sinema inayochezwa sasa nadhani kuna mtu au kikundi cha watu kina engineer hizi sinema swali la kujiuliza jee ni kwa faida ya nani na itawasaidia nini?

Nimefuatilia Kenya kidogo kila Raisi anayechukua madaraka anakuwa akili kubwaaz sana. Hivi hili sisi kwetu si la kujifunza kweli.

Naunga mkono hoja. #2025Kisimakinapunguamaji
 
Pascal Mayalla
Mpiga ngoma ni mpya hawezi piga exactly kama mtangulizi wake kuna midundo anaingiza ala mpya na mingine anaendelea nayo.

Lakini usisahau hadhira haijabadilika hivyo huwezi badilisha muziki moja kwa moja kuna baadhi ya midundo itavutia watu na mingine itawachukiza hivyo itahitaji muda kidogo kuizoea.

Hivyo kwenye hii midundo isiyovutia watu unahitaji vitu kama wachezeji wanaodemka haswa ili kuweza kuipoteza hadhira kidogo isiwaze sana midundo mipya iloingizwa bali i focus zaidi kwenye hawa wademkaji wanaodemka haswa.

Its a matter of time u need to be more than a great thinker.
#the art of state engineering #
 
Serikali inatakiwa kummaliza huyo taperi kwa risasi nyingi za kichwa, haiwezekani hailetee dharau serikali,Ni wakati Sasa azimwe kabisa, ana chuki binafsi na Rais aliyepo Sasa, na ana ukabila wa Hali ya juu na udini pia
No. Nakataa, hiyo siyo njia sahihi ya kushughulika na wakosoaji wa Serikali.
 
Ni kweli mkuu Ila kwenye zile nafasi zake kumi angevuta watu wa maana na kuwapa nafasi hizo Kama alivyofanya mtangulizi wake, siamini kabisa Kama angekosa watu wapo wengi mno sema timu ya ushauri labda sijui ilikula maharage ya wapi yalee
Hata Dorothy ni wa nafasi kumi za Rais na aliteuliwa na mtangulizi hayati, huyu mama hakuwa na nafasi 10 make nafasi nyingi zilikuwa ameshateua mtangulizi wake na zile chache zilizobaki ndo alitumia kuwapoza akina Bashiru na Polepole baada ya kuwatumbua.
 
Makali ya kisu kilichonolewa vema kwa ajili ya baba yao kayashika mama yao, wao wameshika mpini. Unatarajia damu itavuja katika viganja vya nani, kama mama yao akijaribu kuwanyang'anya hicho kisu?
 
Back
Top Bottom