Nyumba yetu inazidi. Rais onyesha uwepo wako, Uwezo Wako Anza na Wale Marrionates Wote Wawili Pale Wapumzishe. The Drama King wa Pinga Chanjo Apuuzwe

Ni kweli mkuu Ila kwenye zile nafasi zake kumi angevuta watu wa maana na kuwapa nafasi hizo Kama alivyofanya mtangulizi wake, siamini kabisa Kama angekosa watu wapo wengi mno sema timu ya ushauri labda sijui ilikula maharage ya wapi yalee
Kwenye zile nafasi 10 unajua zimebaki ngapi kukamilisha?
 
Naam
 
Rais ana mamlaka ya kumwondoa Waziri wa afya na kuteua mwingine. Pia Rais ni Mwenyekiti wa chama chake, akiwa kama Mwenyekiti anayo mamlaka ya kuufuta uanachama wa mwanachama yeyote hata kama mwanachama huyo ni Mbunge.

Nashauri ili nidhamu irudi Serikalini, Madam President atumie rungu lake kwa hao wawili wanaosigana hadharani.

Madam akiendelea kukaa kimya sisi wenye akili zetu tutamwona ni kama mtu aliyeshindwa ku exercise her duty calls.
 
Based on opinion by the majority. Madam anapaswa kufumua marionattes wote aliowakuta ambao hakuwatea yeye. Ni angevunja baraza la mawaziri akaweka wapya, Vitengo vingine vyote hata kila cha wasiojulikana kinahitaji new commander aliyelelewa ndani ya mfumo wao wenyewe.

Kuweka marionattes wapya kutasaidia utiifu, Mama lazima aonyeshe anajali uwajibikaji kama mtu hawajibiki asisubiri ajirekebishe atolewe tuna watu milioni 60 kweli replacement inakosekana.

Hii sinema inayochezwa sasa nadhani kuna mtu au kikundi cha watu kina engineer hizi sinema swali la kujiuliza jee ni kwa faida ya nani na itawasaidia nini?

Nimefuatilia Kenya kidogo kila Raisi anayechukua madaraka anakuwa akili kubwaaz sana. Hivi hili sisi kwetu si la kujifunza kweli.

Naunga mkono hoja. #2025Kisimakinapunguamaji
 
Pascal Mayalla
Mpiga ngoma ni mpya hawezi piga exactly kama mtangulizi wake kuna midundo anaingiza ala mpya na mingine anaendelea nayo.

Lakini usisahau hadhira haijabadilika hivyo huwezi badilisha muziki moja kwa moja kuna baadhi ya midundo itavutia watu na mingine itawachukiza hivyo itahitaji muda kidogo kuizoea.

Hivyo kwenye hii midundo isiyovutia watu unahitaji vitu kama wachezeji wanaodemka haswa ili kuweza kuipoteza hadhira kidogo isiwaze sana midundo mipya iloingizwa bali i focus zaidi kwenye hawa wademkaji wanaodemka haswa.

Its a matter of time u need to be more than a great thinker.
#the art of state engineering #
 
Serikali inatakiwa kummaliza huyo taperi kwa risasi nyingi za kichwa, haiwezekani hailetee dharau serikali,Ni wakati Sasa azimwe kabisa, ana chuki binafsi na Rais aliyepo Sasa, na ana ukabila wa Hali ya juu na udini pia
No. Nakataa, hiyo siyo njia sahihi ya kushughulika na wakosoaji wa Serikali.
 
Ni kweli mkuu Ila kwenye zile nafasi zake kumi angevuta watu wa maana na kuwapa nafasi hizo Kama alivyofanya mtangulizi wake, siamini kabisa Kama angekosa watu wapo wengi mno sema timu ya ushauri labda sijui ilikula maharage ya wapi yalee
Hata Dorothy ni wa nafasi kumi za Rais na aliteuliwa na mtangulizi hayati, huyu mama hakuwa na nafasi 10 make nafasi nyingi zilikuwa ameshateua mtangulizi wake na zile chache zilizobaki ndo alitumia kuwapoza akina Bashiru na Polepole baada ya kuwatumbua.
 
Makali ya kisu kilichonolewa vema kwa ajili ya baba yao kayashika mama yao, wao wameshika mpini. Unatarajia damu itavuja katika viganja vya nani, kama mama yao akijaribu kuwanyang'anya hicho kisu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…